Rupia: Hazina ya Mjerumani

Habari wanabodi!!

Kuna tetesi ambazo zilishavuma sana kwa kipindi kirefu sana hapa nchini huku baadhi ya wenzetu wakijitokeza sehemu mbalimbali kuthibitisha tetesi hizo.

Inadaiwa kabla ya wajerumani kukimbia Tanganyika wakati wa Vita ya kwanza ya Dunia baina yao na waingereza na kujikuta wakishindwa vibaya katika vita hiyo walikuwa wamemiliki hazina na Mali nyingi ndani ya eneo lao lililojulikana Germany East Africa Terrirory.

Haikuwa rahisi baada ya kushindwa vita hivi kuondoka na mali zao zote kwenda nazo Ujerumani. Hivyo basi, mali na hazina nyingi inasemekana zilifinywa maeneo mbalimbali hapa nchini. Kuna ambazo zilifichwa chini ya milima, kwenye mahandaki na kwingineko kama habari zilizotufikia zilivyokuwa zikienea.

Kuna watu ambao walijaribu Mara kwa Mara kuzifikia hazina hizi lakini hakuna aliyewahi kujitokeza na kutabainisha kuwa alifanikiwa kupata hata kipande kidogo cha hazina hizo. Kuna wengi ambao pia walikuja na madai kuwa kwenye maeneo hayo kuna ushirikina mkubwa ambao wajerumani waliufanya hivyo ni vigumu kuweza kufikia hazina hzo bila idhini yao.

Nakumbuka kipindi cha nyuma kuna jamaa mmoja alitoa ushuhuda huko sehemu za tabora kuwa wajerumani walifika na kwenda kuchukua baadhi ya Mali walizoziacha na walifanikiwa na haikuonekana kama ilikuwa ni kazi kubwa kwa upande wao. lakini wananchi wa maeneo hayo wamejaribu kuzifikia hizo hazina kwa miaka bila mafanikio.

Hii inanipeleka niwaze kuhusiana na nchi ya Misri. Kupitia filamu mbalimbali tumekuwa tukiaminishwa nchi ya misri hususani kwenye zile pyramid zake kuna hazina kubwa ikiwemo dhahabu ambayo huwezi kukisia utajiri wake.

Swali ni je, habari kuhusu hizi Mali za wajerumani zilizofichwa ni za kweli? Zimefichwa maeneo gani? Kwanini wazawa hatuwezi kuzifikia hizi Mali? Je, hii nadharia ya ushirikina kwenye maeneo haya ni ya kweli? Ni kweli pia kuwa wajerumani huwa wanafika kuchukua hizi Mali zao walizoficha.

Lets contribute na tujifunze
 
Hivyo vitu yani madini nikweli yaliachwa mi hapa binafsi kijijin kwetu kwa utashi Wangu kijijin kwetu kuna sehemu kulikuwa na becone fulani alafu nondo ikawa imechomoka juu tukawa hatuelewi walikuja jamaa fulani ambao kati yao mmoja alikuwa wa maeneo ya kwetu alikuwa someone informed na mwingine alikuwa ni mzungu wengine hatukuwajua that was 1985 na wqlikuja mchana sa8 tukichunga hapo wakafanya yakwao pale kichotokea baada ya kupomoa hixo zege la nguvu walitoa chupa fulani zilikuwa na tobo chini ambalo ukingiza kidole kinazama chupa zilikuwa na red mercury yule jamaa wa kwetu a lichenga Magorofa mpaka Leo yupo sasa jiulize red mercury 1gram ni million ngapi na Walitoa chupa 5 za lita 2...
 
Mbona Sasa Tunakufa Maskin Nawaka Upo Embu Fanya Makeke Twende Huko

Mshana Jr Atatupa Elim Zaid

Cc: Mshana Jr
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…