Guys, hao Wajerumani wa Kempiski kama wapo kweli watakuwa tu na lengo la kuwatapeli Watanganyika kwasababu sio kila Rupia ina thamani sawa na ingine hapana. Kuna Rupia moja inaitwa Fufumaki alama zake ni kuwa ule upande wa kichwa cha mtu ni " Mzee mwenye Upara " hii moja tu ina uwezo wa kuwafanya watu zaidi ya 200 kuwa " Mabilionea " sasa haiwezekani mtu ainunue ati kwa Mil 200 hata Mil 500 si sawaa !
Stan Mzalendo - Ruvuma ni moja ya mikoa ambayo ina hazina nyingi sana za Kijerumani na hasa kwenye Mahospitali makubwa na Makanisa kuna underground kubwa sana na milango imara sana ambayo haifunguliwi funguliwi hovyo
Binafsi nimesoma high school mkoa huo ila kwa bahati mbaya sanaa nyakati zile sikuwahi kuzisikia hizi habari ila baada ya kusikia na namna nlivyozisoma baadhi ya sehemu mkoa ule ? Tanzania ni nchi Tajiri sana Duniani!
mkuu kuhusu shule ya iyunga sina data napo sana ila kwa uzoefu wangu sehem ninazozijua hivyo vitu sijui rupia,masanduku yenye dhahabu,na vito mbalimbali ni sehem zenye makanisa/hospitali za moravian,shule,maboma +nyumba ambazo zilijengwa na wajerumani wenyewe enzi za ukoloni pamoja na migodi yao ya zamani mfano iliyoko chunya (makongolosi na saza),
mwaka 2008 wakati wa likizo ndefu ya miezi ka mitatu, walikuja hao mnaowaita wazungu(german) wakachimba bwenini, luthuli na kuchukua izo rupee...
Uliwaona kwa macho yako hao Germans wakichimba kusaka hizo rupia au ulisimuliwa neoo?
mpaka lishimo lilibaki, walichimba na high equiped machines.. maana ata kelele azikuwepo.. wakapakia kwenye land cruser yao moto bati,
pole sana ,uliingia kichwakichwa kwa matapeli ,mimi pia nipo ktk halakati hizo,hizo biashara zipo tatizo wengi waongo. kuna soko la mayai ya bundi kama yapo ni pm tufanye biashara
Last week nilikua kwenye stationary nawatolea wateja photocopy akaja jamaa ana karatasi lililoandikwa list ya hela mbalimbali anazomiliki mzee flani katika list hyo zipo rupia kama 5 za mwaka 1904 1905 na nyingine na pia kuna hela za nyerere kadhaa.....nikamtolea copy akaondoka alikua anahitaji copy mbili baada ya kama lisaa akarudi mtoto na karatasi ile ile anahitaji copy mbili tena nkaitoa nkamgea akaondoka baada ya masaa 5 akaja tena jamaa mwngine akaitoa copy mbili akasepa kesho yake tena wakaja pale mwishoe nikauliza mbona hii mnaitoa copy sana jibu alilonipa hata sikumuelewa...sasa baada ya kusoma hii post ndio nmeshtuka nilikua nataka kutengenezewa mchezo wa utapeli walitaka nidadisi waniingize kwenye loop wanipige hela...how come waje watu kama wa4 tofauti kukitoa kipande kile stationary ile ile.....
Ubwege wangu wa kutofuatilia mambo ndio umeniokoa....
Hii article siyo kwamba nimeipenda, imenishangaza sana, ila sasa kwa sababu hamna button ya ku-express mshangao, ikabidi nitumie hiyo ya like. Modulators naomba watuwekee pia button ya kuonyesha msahangao
Kwa wajuzi wa mambo mtujuze kunani ruvuma...
1. Peramiho hiki ni kijiji kilichosheheni underground ways na investments za kutosha....
2.Kuna mzungu flani ana villa yake pale njia ya kwenda mbinga nmeisahau jina ni eneo kubwa tu na wamejenga kitambo porini kule...
3. Hospital ya litembo njia ya kwenda mbamba bay ni hospital kubwa tu na ipo maporini sijui kipindi kile walipoijenga walitarget nini maana ni muda sana....
4. Kuna kanisa kubwa sana baada ya kupita nyoni njia hiyo hiyo ya ziwani...
5. Lituhi napo nasikia....
6. Ukitoka namtumbo kuelekea tunduru kuna mapori makubwa tu ila hayo maeneo yameshapimwa na kuwa planned kitambo sana yani maeneo ya shule makazi ibada maziko mashamba viwanda michezo na kila kitu vimepimwa na alama na mabango yamewekwa....
Hayo ni baadhi tu ya maeneo niliyoyashuhudia kwa macho yangu..
JE kwa wajuzi wa mambo na watu wa historia mnaweza kutupa mwanga kiasi....
Rupia sio lupia