Rupia: Hazina ya Mjerumani

Rupia: Hazina ya Mjerumani

Hizo habari zipo na kweli kuna maeneo nimepata kuyaona yanatia mashaka sana, kuna shule moja nilisoma ile shule imejengwa na wakoloni na tangu waondoke kuna handaki moja limejengwa kwa zege imara na juu limefunikwa ( pia kuna mlima mmoja huko kwetu hadi leo unawekewa ulinzi na kuna mzungu mmoja alikuwa anafanya utafiti sana eneo hilo ni mwanajeshi mstaafu wa nchi moja huko ulaya) hizi habari kuna sehemu naweza kuziamini kwa kile ninachokiona.....kama hujawahi kushuhudia huwezi kupata hoja ya Nguvu kwenye huu uzi
Habari zaidi
 
Niliwahi shuhudia jamaa mmoja aliyesanukia kaburi lenye mali za wajerumani mkoa fulani hapa Tanzania akifa na kukauka kama mti wa mpingo..ama kwa hakika ilinisikitisha sana! Inasemekana jamaa wameacha kafara za kufa mtu katika mali hizo kiasi kwamba kama huna nguvu huwezi chukua! Hii ndio tofauti kati ya uchawi mweupe na mweusi!
Habari zaidi
 
Nina marafiki wajerumani na baadhi walikuwa nazo wakizitunza kama souvenirs tu. Hizi hadithi za mtaani kuhusu hivyo vipimo sijui haionekani kwenye kioo niwasimulia huwa wanacheka sana. Sidhani kama zina ukweli wowote. Mjomba wangu alifilisika na kufa masikini kwa tafuta sarafu zenye hivyo vigezo!
Habari zaidi
 
Acha uongo wako, Mimi nimesoma Iyunga kuanzia mwaka 1991 hadi namaliza form four Hilo shimo pale Luthuli lilikuwepo na nilikuwa nakaa Shaban Robert bwenini. Kuna wakati walikuwa wanachimba then wanatoa Maji then wanapotea kwa miezi kadhaa wanarudi hadi namaliza sikuwahi kuona wala kusikia mzigo umetoka. High equipment machine zao yalikuwa masululu na makoleo na wachimbaji walikuwa weusi tii hakuna mzungu na ilisemekana Ni mchongo wa mwalimu anaitwa Gumbo...
Uyu gumbo ambaye alienda kufundisha DiT

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mwaka 2008 wakati wa likizo ndefu ya miezi ka mitatu, walikuja hao mnaowaita wazungu(german) wakachimba bwenini, luthuli na kuchukua izo rupee...
Ndo Ile likizo ilitokana na Nini,Mabweni mabovu au. Au ndo ilikuwa Mbinu ya kuchukua Mali zao pale. Mkulu inamuhusu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sorry mkuu, nilipata hizo hisia sababu ya hivyo vigezo vya mavazi na mida ya kuingia nikaweka hapo dhana ni kwa masharti. Thank you again🙏
Aisee na mimi nimeingilia Kati Mavazi ni weli yapo siyo kila rangi ya Nguo ni ya kuingia nayo Kule (German Treasures Sites)
 
Vintage Mshana Jr

Huwa nakukubali sana mkuu, ulivyopangilia hizi hoja ni kama thesis ya PhD.

You're a great thinker indeed
Ahhh Hii ame Copy na KuPest Maelezo ya Dr. Thabeet kwenye Web site ya Kampuni ,siyo Hoja za Jamaa aliye post. yenye kuwa na Malipo kwa uhakika.
 
  • Thanks
Reactions: T11
Step ya kwanza: nenda kahakikishe kweli kuna pango lenye zege? kisha mlikague jinsi lilivyo, mlango ulipo, mandhari ikoje.

Step ya pili: Ukishajiridhisha rudini na team yako, anzeni kuchambua madhara ya sehemu hiyo kutokana na mazingira yake..... hii itawasaidia kujua namna mtakavoingia kwa kujilinda.

Step ya tatu: Mkishajua namna na kujipanga, hapa mnapanga kwenda kuchunguza ndani.... step hii mjiandae kisaikolojia zaidi mkiwa na vitu vya kujikinga na madhara, pia muwe tayari kurudi na chochote, hivyo jiandaeni na vibebeo kabisa(kumbuka step hii ni ukaguzi wandani)

Step ya nne: Mmeshajua ndani kuna nn(yawezekana hakuna kitu, vimeshabebwa) lakni kama vipo muwe mnajua kilichopo ni nini, hivyo mmejipanga kubeba, taa za chemli zinazowaka bila mafuta, pasi za dhahabu ambazo haziwekwi mkaa, vikombe vya dhahabu.... sarafu, manwe kukuta buti(sema hapa zitakuwa zimeshaharibika na kuwa km bigijii)au bunduki na masanduku ya unga wa baruti, hizi acganeni zazo kwa kuwa ni rahisi kukamatwa nazo..... lkn km una mtu unaeza muuzia, chukua.

Kwa step hizo, mko tayar kuwa matajiri.... pangeni safari fasta.

ANGALIZO: kuna mitego mingi sana, ukiachilia ya kichawi, kuna.mitego ya gesi chafu(wataalamu wanazijua kwa majina) hizi ni pale umekuta kikombe maridadi cha dhahabu( hasa mwanzoni mwanzoni mnapoingia) halafu ww unakibeba kwa pupa kumbe limetegeshwa na unapokitoa unategua kitu kinachoatoa hiyo gesi.... hivyo MNAKUFA MNAJIONA kabla ya kusonga mbele, inaweza kuwa sehem yamepangwa mawe, mkaondoa moja tu, lkn hilo ndo limebeba uzito wa mengine yaliyopangwa kiustadi yatakayopelekea kuporomosha mengine yatakayoziba njia mliyoingilia(MNAKUFA MNAJIONA)

Kwa hiyo mnapaswa kuwa makini sana kugusa vitu msvyovijua kwa kuwa mpo kwenye hatua ya uchunguzi, pia hakikisheni mna kamera yenye flash, taa zenye mwanga mweupe, na diary ili kunote kila mnachokiona.
Umesahau kuwataadharisha kuhusu dhamiri yao ni nini?
Kuona au Kuchukua?
na kama ni kuona Je,wakibadilika na kutaka Kuchukua ni nini kitatokea?
pia Je ni wangapi huwa wanaruhusiwa Kuingia Saiti na wanatakiwa kuwaje kuanzia Mavazi nk?
Nini wafanye kabla na nini wasifanye?
Ahsante yangu ni Hayo tu.
 
Mwaka 2009 nilipata kibarua ya mda pale ngorongoro, nikazoeana na mwenyeji mmoja wa pale ingawa yeye si mzaliwa wa hapo... Siku moja akanipa wazo tupande mlima moja mrefu ulio pembezoni mwa creta, akanipa data kidogo kuwa wakati wa vita vya pili wajerumani walitumia mlima huo km chimbo lao. Chini ya huo mlima kuna mashamba na majengo yao ambayo yapo hadi leo.... Tulipanda huo mlima tukiwa tumebeba lunch box zetu, tulipofika karibu na kilele tulipita kati ya miamba fulani tukaona maganda ya risasi na vichupa vidogo vya soda vikiwa vimepoteza sura. Tulifika mahali juu kidogo tukakuta kidimbwi ikiwa imezungukwa na miti mikubwa. Mojawapo ilikuwa na kitu kikiwa kimefungwa na mnyororo ambao umezama ndani ya mti yaani mti umekua nao ukameza mnyororo. Tulicheki tukaona ni kisanduku kina kofuli ilopata kutu na kuzeeka sana... Tuliamua tujaribu kuitoa ghafla ukaja upepo tukajikuta tuko chini ya mlima nyuma ya shule fulani ya msingi, hatukuwa na ujanja tukarudi kambini. Baada km wiki mbili tukaazimia kurudi na vifaa ili tushushe lile sanduku... Tulipofika hapo ile tumegusa ule mti mi nikajikuta niko barabara fulani inayoenda kijiji fulani inaitwa endulen, sikujua mwenzangu yuko wapi, nilijaribu kumpigia cm yake ikawa haipatikani. Nikarudi kambini jioni lakini jamaa bado hayupo hadi siku ya pili ndo akapatikana kwenye cm. Akanijibu amejikuta yuko wilaya jirani ya karatu ilimbidi apande basi ili arudi kazini... Tulikoma kwakweli. Miaka chache tena baadae 2014 kuna mzee fulani mwenyeji wa manyara akaniambia nimsaidie kutafuta soko la mali zake fulani ambazo alichimbua ktk pori kilomita kadhaa mashariki mwa hoteli ya ndutu kule Serengeti. Akaeleza kuwa aliona kitu km msingi wa nyumba kimesakafiwa ktk bonde waliamua kivunja ili waone kuna nini. Walifanikiwa kutoa sanduku lakini ghafla akatoka shimoni joka kubwa aina ya chatu akapanda juu ya hilo sanduku. Wakaamua wachukue kondoo moja km kafara kwa joka hilo, baadae likarudi shimoni na wao wakachukua sanduku hilo. Wakafika mahali ikabidi walivunje wakakuta bunduki 2, mawe yanayon'gaa km kilo 3, mikufu 2, binocular 2, nguo za khaki, pesa za rupia sarafu 52 imeandikwa tabora pound, na vitu vidogo vidogo. Bunduki waliamua wazichimbie ardhin, na vingine wakaweka ndani mfuko afu wakachimbia ndani ya boma la tajiri wao wa ngombe... Mwaka ukapita afu yeye akarudi kwao manyara. Baadae yule mwenye boma akawa amemtuma kijanake kumweleza huyu mzee aje aondoe vitu hivo kwake kwasababu vinaleta vitisho vya radi kila siku. Niliposikia hayo nikapatana nae aende mtu wangu moja ili walete, soko si tatizo. Baada ya wiki niliandaa safari yao walipokaribia ile nyumba ghafla mzee akawa km hajielewi anaongea mwenyewe hataki mtu karibu yake. Jamaa akanipigia cm, nikamwambia urudi nae, eti wakati wa kurudi ile wenge imepotea yuko sawa. Na yeye anashangaa mbona tunarudi walikotoka awali? Ikabidi tutemane na hiyo mambo coz kila utakalogusa lina mauzauza....... Simshauri mtu afuatilie hizi mali coz unaweza ukajikuta we ni mganga wa kienyeji au ni mchawina
Aisee japo umeshauri watu kutokutafuta ila mimi nakuja tofauti kwako,,,,kama kutunukiwa uishatunukiwa mpaka kufika kwenye vitu husika sema sasa haukuwa na Mwanga wa kumalizia kazi Mkuu ... kwenye sehemu ya kwanza ulifika kwenye saiti husika na Kosa ni Kugusa na je Mlienda siku gani ya Juma?
pili kisanduku kilikuwa ni cha Shaba kama si Nyekundu Basi Njano... hapo iltakiwa kutamka maneno Machache na kingetoka na kushuka Mpaka ardhini na Baada ya kukaa ardhini ungekichukuwa na wala kisingekuwa na Madhara Kwako.
Tatu kwa mzee wa Kimasai alifanikiwa kupata lakini ukisha chinja Mnya na damu ikamwagika basi yale madudu huwa yanakunywa kidogo na inakuwa kama ina walevya kwa kipindi cha Masaa 72 na pia unatakiwa kuondoka eneo husika na Mzee wa Kimasai Hope alifanikiwa ila kwa kuwa hakuwa na namna ya Kutenganisha ile mali na yale Madudu basi Masaa 72 yalipoisha akaendelea kuwa na vy o kwa kufukia chini na Zilipoisha siku 90(miezi 3)akiwa na zile mali na yeye akawa Saiti na ndiyo maana alipofatwa kwa ajili ya kwenda kurudisha kwa wakusanyaj ili apate Hela akawa kama anawehuka na ukiacha kuongelea Mali basi anakuwa sawa.....hapo ni kwasababu aliwapa Damu sasa na yeye aliyatoa kule Basi yalimtaka aendelee kuyaabudu na Mpaka leo kuna Vitu atakuwa anaendelea Kufanya kama hakupata wakutenganisha Items husika na zile roho Chafu.
MAELEZO YAKO YALIKUWA SAHIHI na ndiyo Maana nimepata hamasa ya Kuchangia kwenye Makosa yakiyofanyika kwenu.
Nyongeza FunFu Mark ndiyo yenye Tabia ya Kumrusha Mtu Mbali na Box uliyoona Hope full 100% ndani yake zilikuwepo.
 
Nakuja na hii kitu na ntawatafuta wanaojua hizo sehemu tukasake mali hizo
105cfbe0e5661a0e7e7396fb6b620a37.jpg
Haina Nguvu pale huwa zinakufa
 
Jamani hiii nikweli waliacha mali Tanzania..kuna maeneo mengi ukitembea milimani utakuta vyuma flani vya mviringo vimejazwa udongo wa cement kali.juu kuna maandishi yanaonesha vipimo flani vya umbali kutoka usawa wa alama hiyo ilipo.ninae changia maada hii ninauhakika. Ila cjawahi kuona wamefika na kuchukua mali ila hali hii ipo kabisa.. Nivigum kuamini kwasababu tumechelewa kupata elim lkn habari hii ni yakweli kabisa
Kabisa Mkuu
 
Upo uvumi pia, kuwa aliyewahi kuwa Mkuu wa nchi (Tanzania) amejenga HEKALU katika moja ya mkoa (Mwambao) chini kuna utajiri wa DHAHABU..

Vipi na tetesi hizi..! Naomba anaefahamu kuhusu hili atujuze..

Nazo zikiachwa, uvumi utarithishwa kizazi na kizazi
Ni kweli.
 
nitakuja kuwaondoa hao nyuki ili tukombe rupia ili tuishi kama malaika maana usawa huu chama tawala kinajua kinachofanya
Samahani Mkuu japo nipost ya Muda Mrefu nataka kujua kwenye hili eneo unaloliongelea bado kuna hiyo hali?
na nyuki hao ni wale wekundu?
 
Niliwahi shuhudia jamaa mmoja aliyesanukia kaburi lenye mali za wajerumani mkoa fulani hapa Tanzania akifa na kukauka kama mti wa mpingo..ama kwa hakika ilinisikitisha sana! Inasemekana jamaa wameacha kafara za kufa mtu katika mali hizo kiasi kwamba kama huna nguvu huwezi chukua! Hii ndio tofauti kati ya uchawi mweupe na mweusi!
Yes hii Nikweli io hivyo Mkuu kama huna elimu ya kitu Husika ni hatari Kufanya na Kaburi aliloenda unalikumbuka?
Je bado unainterst na hii kitu?
naweza Hojiana na wewe Inbox?
 
"Mzee mwenye upara" ndiye huyo. Kaizari Friedrich Grosherzog aliyetwala tangu 1858 mpaka 1907. Upande wa nyuma unafanana na Fufumaki zingine. Hata nijuxeni wapi nikachote hayo mabilioni. Kuna 10% kwa atakayetoa mwongozo wa soko!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Siyo Funfumark
 
Back
Top Bottom