Step ya kwanza: nenda kahakikishe kweli kuna pango lenye zege? kisha mlikague jinsi lilivyo, mlango ulipo, mandhari ikoje.
Step ya pili: Ukishajiridhisha rudini na team yako, anzeni kuchambua madhara ya sehemu hiyo kutokana na mazingira yake..... hii itawasaidia kujua namna mtakavoingia kwa kujilinda.
Step ya tatu: Mkishajua namna na kujipanga, hapa mnapanga kwenda kuchunguza ndani.... step hii mjiandae kisaikolojia zaidi mkiwa na vitu vya kujikinga na madhara, pia muwe tayari kurudi na chochote, hivyo jiandaeni na vibebeo kabisa(kumbuka step hii ni ukaguzi wandani)
Step ya nne: Mmeshajua ndani kuna nn(yawezekana hakuna kitu, vimeshabebwa) lakni kama vipo muwe mnajua kilichopo ni nini, hivyo mmejipanga kubeba, taa za chemli zinazowaka bila mafuta, pasi za dhahabu ambazo haziwekwi mkaa, vikombe vya dhahabu.... sarafu, manwe kukuta buti(sema hapa zitakuwa zimeshaharibika na kuwa km bigijii)au bunduki na masanduku ya unga wa baruti, hizi acganeni zazo kwa kuwa ni rahisi kukamatwa nazo..... lkn km una mtu unaeza muuzia, chukua.
Kwa step hizo, mko tayar kuwa matajiri.... pangeni safari fasta.
ANGALIZO: kuna mitego mingi sana, ukiachilia ya kichawi, kuna.mitego ya gesi chafu(wataalamu wanazijua kwa majina) hizi ni pale umekuta kikombe maridadi cha dhahabu( hasa mwanzoni mwanzoni mnapoingia) halafu ww unakibeba kwa pupa kumbe limetegeshwa na unapokitoa unategua kitu kinachoatoa hiyo gesi.... hivyo MNAKUFA MNAJIONA kabla ya kusonga mbele, inaweza kuwa sehem yamepangwa mawe, mkaondoa moja tu, lkn hilo ndo limebeba uzito wa mengine yaliyopangwa kiustadi yatakayopelekea kuporomosha mengine yatakayoziba njia mliyoingilia(MNAKUFA MNAJIONA)
Kwa hiyo mnapaswa kuwa makini sana kugusa vitu msvyovijua kwa kuwa mpo kwenye hatua ya uchunguzi, pia hakikisheni mna kamera yenye flash, taa zenye mwanga mweupe, na diary ili kunote kila mnachokiona.