Rupia: Hazina ya Mjerumani

Rupia: Hazina ya Mjerumani

Mkuu,
Suala la Rupee/ Rupia ni fedha iliyotumika wakati wa Ukoloni wa Mjerumani. Kuhusu thamani ya fedha hiyo haina thamani yoyote kama inavyodhaniwa. Pamoja na hilo la utafutaji hazina na hilo la utafutaji Rupia ni mbinu za Wajanja ( Matapeli) kujipatia fedha kwa watu wanaowalenga. Wengi wamelizwa kwa mtindo huu wa utajiri wa haraka na mteremko.
Umeongea ukweli mtupu. This rupee/rupia hype is nothing but a scam.
Thanks
 
Kujua ukweli wa haya masuala ya wajerumani na kuficha hazina zao hapa nchini serikali inge fanya hivi; Kwa kuwa reli iliyojengwa na mjerumani ni moja ya maeneo twaja, basi itangaze tenda ya ujenzi wa hiyo reli upya. Kigezo kiwe atakaye tenda kuijenga kwa gharama ndogo au kuijenga bure ndiye atapewa hiyo kazi. Wajerumani wakijitokeza na kushinda basi tuamini haya masimulizi tuliyo ya soma hapa. Vinginevyo tuendelee tu kusoma kama hadithi za alifulela ulela.
 
Mkuu kutokana na uzoefu wangu ktk sekta mbalimbali nianze na hv,kama utakuwa mfuatiliaji mzuri wa mambo ya FREEMANSORY au ILLUMINATI na alama zao kishetani utagundua kuwa alama zao nyingi hupenda kuziweka kwenye fedha iwe ya coin au noti mfano mzuri ni USD ambayo ina bundi,fuvu,nyota,piramidi,satanic eye,nk alama zote hizo zinalengo moja kuu nalo ni mazindiko! Na kama ujuavyo mazindiko yote ni moja ya ibada za kishetani ambazo hujumuisha majini,mapepo,mizimu,roho chafu pamoja na kafara hasa kafara ya damu ya binadamu!
Na ukifuatilia kwa umakini utagundua hao ma-FREEMANSONS & ILLUMINATI wana origin ya sehem moja nayo ni UJERUMANI ktk jimbo moja linaitwa BAVARIA!
Sasa swala la kujiuliza ni hili ikiwa dunia ya sasa ya sayansi na technology mambo ya mashetani na makafara yapo ktk ela kubwa kama USD na tena kwa kiasi kikubwa SEMBUSE ENZI ZILE ZA GERMANY EMPIRE?.sasa ndio nakuja kwenye Rupia,nikweli ile coin ya rupia inamaajabu flan ambayo yakichanganywa na mazindiko na kafara zingine huwa inaleta kile mtu anakuwa anatake either pesa,cheo au utajiri hii inatokana kuwa ela ya rupia ilipata zindiko la damu ya binadamu wkt wa utengenezaji inasadikiwa madin yaliyotumika kuitengeneza yalikuwa yakichanganywa na damu za binadam thats y wajeruman wkt wanaondoka walizificha hzi ela sehem mbalimbali za tanzania hasa ktk maboma,makanisa(moravian),mito,visima na mashimo marefu sehem nyingi hupatikana mkoa wa mbeya,iringa na swanga! Na wajeruman waliweka alama kibao hasa katika magome ya miti mikubwa na mawe na huwa wanakuja kuchukua hizo rupia + madini mengine waliyoyaifadhi baadhi ya sehem zilikofichwa madini haya kwa mkoa wa mby ni hizi hapa,
1.Wilaya ya chunya-makongorosi-kijiji cha ujerumani(hapo panamgodi wa dhahabu wa zaman wa mjerumani ni DEEP GOLD MINE)kunamashimo makubwa ma4 nimakubwa sana!, 2.Sehem zote zilizojengwa hospitali za mission za moravian hasa na mjerumani flan ambaye kwa sasa ni marehemu ila watoto wake wanaendeleza game anaitwa LENHNER(LENA) hospitali ya mbalizi,IFISI SONGWE NA MATEMA BEACH!
Kuna ukweli asilimia nyingi sana kwenye hichi ulichoandika.
Nimeambiwa,kuna wajerumani ambao wameanza kutafuta sanduku lenye rupia kwenye baadhi ya mito kwenye milima ya Uluguru.
Inasadikiwa hutumia ramani flani kuweza kutambua eneo hilo lililowekwa hilo sanduku lililosheheni rupia na vitu vya thamani.
Dunia ina mambo
 
Mi mbona ninazo kama sita hivi hasa zile zenye matundu katikati nimeziweka tu hata b.o.t hawana kweli mi maskini kama mengi
 
Wakati nasoma Sekondary niliingiaga kwenye haya mambo ni baada ya mzee mmoja kutuambia tukimpelekea jiko la mjerumani anatupatia milioni 2, Lakini hatukufanikiwa. Ila kama mawiki matatu yamepita nilikutana na mzee akanionyesha Rupia anazo mbili ila zina makuti kwa nyuma, nilipoongea naye akanambia nimtafutie mteja. Cha ajabu kila mteja anambia miaka sio zenyewe ni 1905 na 1913. Wataeja wote wananambia inabidi mwaka 1904 kwa Rupia za makuti. Inaonekana kweli kuna uhuni na wateja hakuna wanachofanya ni kukwepesha miaka ili zionekane sizo zenye uhitaji. Lakini kama kweli ni dili, zikifanikiwa kuuzwa hizi ambazo nimezishuhudia ntajua biashara ni ya ukweli.
 
Last week nilikua kwenye stationary nawatolea wateja photocopy akaja jamaa ana karatasi lililoandikwa list ya hela mbalimbali anazomiliki mzee flani katika list hyo zipo rupia kama 5 za mwaka 1904 1905 na nyingine na pia kuna hela za nyerere kadhaa.....nikamtolea copy akaondoka alikua anahitaji copy mbili baada ya kama lisaa akarudi mtoto na karatasi ile ile anahitaji copy mbili tena nkaitoa nkamgea akaondoka baada ya masaa 5 akaja tena jamaa mwngine akaitoa copy mbili akasepa kesho yake tena wakaja pale mwishoe nikauliza mbona hii mnaitoa copy sana jibu alilonipa hata sikumuelewa...sasa baada ya kusoma hii post ndio nmeshtuka nilikua nataka kutengenezewa mchezo wa utapeli walitaka nidadisi waniingize kwenye loop wanipige hela...how come waje watu kama wa4 tofauti kukitoa kipande kile stationary ile ile.....
Ubwege wangu wa kutofuatilia mambo ndio umeniokoa....
 
Last week nilikua kwenye stationary nawatolea wateja photocopy akaja jamaa ana karatasi lililoandikwa list ya hela mbalimbali anazomiliki mzee flani katika list hyo zipo rupia kama 5 za mwaka 1904 1905 na nyingine na pia kuna hela za nyerere kadhaa.....nikamtolea copy akaondoka alikua anahitaji copy mbili baada ya kama lisaa akarudi mtoto na karatasi ile ile anahitaji copy mbili tena nkaitoa nkamgea akaondoka baada ya masaa 5 akaja tena jamaa mwngine akaitoa copy mbili akasepa kesho yake tena wakaja pale mwishoe nikauliza mbona hii mnaitoa copy sana jibu alilonipa hata sikumuelewa...sasa baada ya kusoma hii post ndio nmeshtuka nilikua nataka kutengenezewa mchezo wa utapeli walitaka nidadisi waniingize kwenye loop wanipige hela...how come waje watu kama wa4 tofauti kukitoa kipande kile stationary ile ile.....
Ubwege wangu wa kutofuatilia mambo ndio umeniokoa....

hahahaaaa,hata mie ningekuwa ----- tu na kuwaza moyoni hayanihusu.
 
Kwa wajuzi wa mambo mtujuze kunani ruvuma...
1. Peramiho hiki ni kijiji kilichosheheni underground ways na investments za kutosha....
2.Kuna mzungu flani ana villa yake pale njia ya kwenda mbinga nmeisahau jina ni eneo kubwa tu na wamejenga kitambo porini kule...
3. Hospital ya litembo njia ya kwenda mbamba bay ni hospital kubwa tu na ipo maporini sijui kipindi kile walipoijenga walitarget nini maana ni muda sana....
4. Kuna kanisa kubwa sana baada ya kupita nyoni njia hiyo hiyo ya ziwani...
5. Lituhi napo nasikia....
6. Ukitoka namtumbo kuelekea tunduru kuna mapori makubwa tu ila hayo maeneo yameshapimwa na kuwa planned kitambo sana yani maeneo ya shule makazi ibada maziko mashamba viwanda michezo na kila kitu vimepimwa na alama na mabango yamewekwa....
Hayo ni baadhi tu ya maeneo niliyoyashuhudia kwa macho yangu..

JE kwa wajuzi wa mambo na watu wa historia mnaweza kutupa mwanga kiasi....
 
Back
Top Bottom