Wakuu hivi ni mimi sina taarifa au vipi? mbona kila sehemu ukienda watu wanadai rushwa bila kificho? Immigration, TANESCO hata TRA. Nini kimetokea ghafla?
1. Immigration - ili upate passport lazima ujipange sawasawa, zile siku zilizoainishwa ni geresha?
2. Kuwekewa umeme - unaambiwa hamna nguzo, hadi uwape chochote, nguzo zinapatikana siku hiyo hiyo.
3. Tunduma na Kasumulu Border posts - kila ukigusa Ni mwendo wa rushwa kuanzia (polis, TRA),
4. Hospitali - Mwananyamala pamoja na makamera kukaa kila corridor hiyo nyomi Lazima ulazimishwe kutoa Chochote. Sawa akanunue pharmacy nje ya geti