Rushwa ya trafiki sasa ni bila kificho, yakijiri mpo?

Hizo pesa za matrafiki zina laana, hamna trafiki mwenye kumiliki jengo la ghorofa kariakoo au apartment dar es salam, wote wanaishia kujenga vibanda na kumiliki vigari vya aina ya baby walker.
 
Kitu umatakiwa kuelewa mikoa mikubwa traffic Wana day la 150k ambayo wanatakiwa wapekeke ofisini baada ya hapo kinachofuata ni chao.

Ukuona traffic kakusimamisha ukampa ten akajomaa kukuandikia unue hajafikisha 150k ya ofisi na hapo ndio hata kosa la kukuonya unaandikiwa.
Asipofikisha hesabu hapangiwi barabara
 
Sasa mkuu 150k si ni magari matano tu? barabarani yanapita zaidi ya magari 1000 kwa siku
 
Kuna mmoja Simiyu alinikamata na tochi ya overspeed , i was doing 65 in a 50km/h zone, huku na huku akawa anakomaa 10000, au aniandikie , mi nikawa nataka nimtoe 5000, baada ya kulia lia sana ikabidi anipe ukweli , kasema bro hiyo teni ningekuwa nachukua peke yangu ningekuwa tajiri , maana nikikamata gari kumi tu ni laki,tatizo hadi mkuu wa idara anaitolea macho na anahesabu kila gari tunayokamata. Ilibidi nimpe tu ten. Ila kwa point waliyokuwa wamekaa na tochi yao naamini walitengeneza zaidi ya milioni siku ile
 
Hela ndogo sana hiyo
 

Jambo usilolijuwa..... Unafanya analysis kwa sababu imekutokea wewe[emoji2369]
 
Ndio hivyo; siku hizi unaona Hadi maboss wao wanakaa barabarani maana waligundus kuwa hawapati mgao sawa sawa hivyo nao wanasonga front
 
Umeandika namba ya gari waliotoa Rushwa huku wapokeaji umeacha harafu unataka kuipinga rushwa sio kweli...
 
Hiyo rushwa ilibarikiwa na mungu wa wapumbavu aliyefungua Mahakama ya mafisadi na uhujumu uchumi kisha akatumia kuwatesa mabosi ambao hawajamchangia pesa 2015 alipogombea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…