Ukiangalia nchi/timu zote zilizochukua kombe la dunia, utagundua kuwa kulikuwa na ile inaitwa golden generation. Kwa mfano brazil ile ya kina pele % kubwa ni walewale ndio walichukua kombe mara zile tatu. Kina Didi, Vava, Pele, Garincha Zagalo n.k.
1978 Argentina wanachukua kombe wakiwa na kizazi cha dhahabu, kina Valdano, Burcharga na 1986 wanarudia wakiwa wameongeza mastaa kibao akiwepo Diego Maradona, na Caniggia.
1990 Ikawa kama hii ya 2018 timu kibao zilienda zikiwa ma mastaa kibao. Uingereza ya Shilton, Paul Parker, Peter Birdslay, Terry Butcher, Chriss Wadle, Garry Liniker na wengine.
Ujerumani ya Ruddy Voller, Klinsmann, Andreas Brehme, Lother Matheus nk.
Argentina ya Maradona, Ganigia, Valdano, Burchagga nk
94. Brazili ya wakali kina bebeto, Cufu,Romario,, Leonardo, Aldair marius Santos, Captain Dunga, Mazinho, Mauro Silva, Rai nk.
98. France ya Zizou, Lizarazu, Desaily, Libouf, Deschamp, Karembeu,Viera na kina Hendry.
2002. Brazili ya kina Di lima, GAUCHO, Rivaldo nk
2006. Italia ya Pirlo Canavarro, Gatuso, Zambrota na wakali kobao. Fabio Grosso na Vincenzo Ianquitta.
2010. Spaini hii ndio ilikuwa nuksi. Kila mtu analijua hilo. Spain hii ilichukuwa euro 2008, ikachukua world cup 2010, na euro tena 2012. Mastaa kibao Xavi,Iniesta,Puyol,Avid Villa nk.
2014. Germani ya Khadera, Ozil, Gotze, Muller, closer, na nyota kibao.
Sasa 2018. Nchi zenye mastaa na walipewa nafasi ya kushinda ni Brazil, Belgium,France, Argentina na German ambao %kubwa ndio walishinda 2014. Baadhi zimeondolewa. Zilizobaki ni france na Belgium. England ina nyota lakini hawafikii hata wa croatia.
Kwa maoni yangu nusu fainali hii mshindi kati ya france na belgium ndio ataibuka mikono juu. England watapata tabu sana kwa croatia. Na nina uhakika watatolewa maana watakuwa na pressure kuliko Croatia.