Ruto ana funzo kwetu dhidi ya walamba asali

Ruto ana funzo kwetu dhidi ya walamba asali

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Walamba asali wamejisahau. Wamedhani sisi tunayo furaha mno wao na familia zao wakiendelea kujimilikisha nchi na kujineemesha.

Tozo hizi wanazo turundikia sisi, zina ridhaa gani nasi?

Ruto na jamii ya Wakenya iliyochoka mno na madhila kama ya kwetu, ilisimama imara vilivyo kuwakataa walamba asali wa namna hii:

Kujizatiti kupata utawala wa haki na usawa kwa hakika inawezekana.
 
1-2.jpg
 
Na hili ndio kosa chadema wanataka kulifanya, kujikomba kwa mama Samiah kwa uongo wa maridhiano. Shauri zao. Wajitenge mapema na mama Samiah hana jipya kwao, atawazungusha na baadae kuwatosa wabaki wanalia. CCM haijawahi kuipenda CHADEMA hata siku moja. Mtu wa karibu amshauri Mbowe.
 
Kenya kwanza iliasisiwa takribani miaka 2 iliyopita. Vuguvugu la kuwang'oa walamba asali linapaswa kuwa zaidi ya u-vyama.

Funzo kubwa kwetu - umoja ni nguvu.
 
Walamba asali ni Tundu Lisu, Mbowe, Zito Kabwe, Nape, Makamba & Co.
 
Watu hubadilika. Zaidi sana picha tu mkuu? Suala siyo itikadi? Kama ni itikadi huyo mwamba ni huyu hapa in black and white:

Raila uses friendship with Magufuli to win over voters

Siyo kweli, Uhuru Kenyata na Raila wamekampeni pamoja kama team against Ruto na Uhuru Kenyata ndiyo bosi wa Mbowe, Tundu na CCM ya sasa hivi, Uhuru ni adui wa Uongozi wetu uliopita na ni rafiki wa Utawala wa sasa hivi ni patron ndio au malaika mlinzi wao kama ukipenda na ndiyo maana Mungu kamlaani Uhuru kashindwa uchaguzi pamoja na kuwa na kila kitu kuanzia namba za kabila kubwa mpaka Uraisi vyote havikusaidia kitu hata hapa itakuja hiyo laana, watashindwa pia usiniulize how, Mungu anajua kama alivyompa Ruto ushindi atawaangamiza pia Tundu Lisu, Mbowe, Zito na Utawala wao uliopo!
 
Siyo kweli, Uhuru Kenyata na Raila wamekampeni pamoja kama team na Uhuru Kenyata ndiyo bosi wa Mbowe, Tundu na CCM ya sasa hivi!

Raila alikuwa rafiki chanda na pete wa mwendazake. Yupo kwenye records akisema akichukua nchi atakuwa kama mwendazake.

Mwendazake hajawahi kuwa na cha kufanya na Mbowe wala Lissu. Itoshe kusema sera za mwendazake ambazo ni msingi wa sera za baba hazijawahi kuwa msingi wa hao unaoonekana kuwakasirikia mno kutokea kusikojulikana.

Ukombozi wa nchi hii unawahitaji wenye moyo.

Somo la Ruto ni la manufaa kwetu ukiwamo wewe kama nawe umechoshwa na walamba asali wetu na tozo zao.
 
Raila na Uhuru wamekampeni dhidi ya Ruto, kama ni kweli Raila alikuwa team Magufuli, Mbowe alifwata nini kwa Raila Nairobi ? Mbowe na Tundu ni adui wa Magufuli wanamshambulia mpaka leo hii sasa iweje Mbowe aende kumtembelea Raila? Mbona (Mbowe) hakukutana na Ruto popote pale?

Usichanganye mambo, kupenda sera za Magufuli siyo kumpenda Magufuli, ni vitu viwili tofauti, hata Samia akizidiwa huongelea na kusifia sera za Magufuli ingawaje humnanga kila apatapo nafasi!
 
Raila na Uhuru wamekampeni dhidi ya Ruto, kama ni kweli Raila alikuwa team Magufuli, Mbowe alifwata nini kwa Raila Nairobi ? Mbowe na Tundu ni adui wa Magufuli wanamshambulia mpaka leo hii sasa iweje Mbowe aende kumtembelea Raila? Mbona hakukutana na Ruto popote pale?

Usichanganye mambo, kupenda sera za Magufuli siyo kumpenda Magufuli, ni vitu viwili tofauti, hata Samia akizidiwa huongelea sera za Magufuli ingawaje humnanga kila apatapo nafasi!

Hakuna aliye mkamilifu. Hakuna asiye na kasoro. Hakuna asiyekuwa na jema au mapungufu.

Kwamba Raila hana au hakuwa na mema? Kwamba Ruto hana mapungufu?

Hatuwezi kujifunza mema kwa watu tukayaacha mapungufu yao?

Raila katika mema yake ni pamoja na kupatikana kwa katiba madhubuti iliyomfikisha kila mkenya akiwamo Ruto alipo leo.

Kwamba Ruto kuna mapungufu yake mengi yajulikanayo? Hakutusimamishi bado kujifunza kwake dhidi ya walamba asali.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Hili funzo la Kenya naona tumelipata lakini mazingira yetu bado yanatubana tusifanye mambo yetu kwa upana ule waliofanya wakenya.

Wale jamaa siasa zao naona zimepiga hatua kulinganisha na hizi zetu, sisi bado tunatakiwa kujisogeza angalau tufikie pale walipo wakenya.

Kujisogeza huko ili funzo la Ruto liwe applicable kwetu, kwanza naona lazima tuwe na tume huru ya uchaguzi, au ikibidi Katiba Mpya [Rasimu ya Warioba]. Tukishaipata hii tume/Katiba basi hapo ndipo tuanze kuwa na tumaini.

Lakini kuendelea kuwategemea hawa wanasiasa wetu ambao licha ya kuungwa kwao mkono na wapiga kura wengi [refer Lissu 2020] tatizo letu bado maamuzi ya wapiga kura hayaheshimiwi kwenye sanduku la kura, hivyo sioni kama funzo la Ruto litakuwa na impact kwetu.
 
Walamba asali wamejisahau. Wamedhani sisi tunayo furaha mno wao na familia zao wakiendelea kujimilikisha nchi na kujineemesha.

Tozo hizi wanazo turundikia sisi, zina ridhaa gani nasi?

Ruto na jamii ya Wakenya iliyochoka mno na madhila kama ya kwetu, ilisimama imara vilivyo kuwakataa walamba asali wa namna ya kwetu:

View attachment 2329076

Kujizatiti kupata utawala wa haki na usawa kwa hakika inawezekana.
Kwani Chadomo wakiingia hawatalamba asali ila watalamba pilipili?
 
Back
Top Bottom