Ruto ana funzo kwetu dhidi ya walamba asali


Funzo nilionalo kwa Ruto ni kwenye kuwaunganisha watu dhidi ya establishment. Hii ni jitihada yenye ku transcend party politics.

Umoja kama huo ndiyo utakaotupa katiba mpya, tume huru, uchaguzi wa haki na hatimaye kuheshimiwa kwa kura za watu.
 

Sielewi unachomaanisha, haujibu swali kwa nini Mbowe hakwenda kukutana na Ruto? Mbowe ni team Raila na Uhuru, na huu uchaguzi wameangukia pua, ila sasa hivi mnataka kuanza kujipendekeza kwa Ruto kwa sababu kashinda na Dunia nzima inamuongelea kabla ya hapo hamkujali chochote kuhusu Ruto, ninyi ni wanafiki kama Raila na ndio maana hamfiki popote kisiasa kwani mmezoea Unafiki, Majungu na Fitina na mtaishia hivyo hivyo tu kubadilika kama malaya bila ya msimamo, you are not real!
 

Uchaguzi wa Kenya haujaamriwa. Hadi wa sasa hayupo aliyedhahiri kuchukua nchi.

Nini usichoelewa katika nilichoandika?

Kwani Ruto ni malaika? Au Raila ni shetani? Hatuwezi kujifunza na kuchukua yaliyo ya kufaa toka kwa watu wote?

Ruto ni mfano mzuri kwenye kuwakataa walamba asali nyie.

Raila ni mfano mzuri kwenye kupigania katiba muafaka dhidi ya walamba asali nyie.

Hatupoi hatuwataki walamba asali na tozo zenu nyie.

Habari ndiyo hiyo.
 

Walamba asali ni chadema Mbowe na Tundu Lisa atleast labda kama haujauelewa huo msemo, hakuna mtu aliyenuifaika na Utawala wa Samia kama Viongozi wa chadema Mbowe, Tundu lisu au Zito Kabwe na ndio maana hata wameacha na Upinzani wenyewe!
 
Walamba asali ni chadema Mbowe na Tundu Lisa atleast labda kama haujauelewa huo msemo, hakuna mtu aliyenuifaika na Utawala wa Samia kama Viongozi wa chadema Mbowe, Tundu lisu au Zito Kabwe!
Chadema Mbowe na Lissu ndiyo wanaorithishana utawala wa nchi na kuturundikia utitiri wa tozo hadi benki?

Sayari ulikotokea hawajambo ndugu?
 
Chadema Mbowe na Lissu ndiyo wanaorithishana utawala wa nchi na kuturundikia utitiri wa tozo hadi benki?

Sayari ulikotokea hawajambo ndugu?

Ndiyo, ni sehemu ya mfumo wa Utawala uliopo, ni wanufaika wakuu wa Utawala wa sasa hivi, na ndiyo maana wameacha Upinzani!
 
Nani kakuambia Ruto alikuwa alambi asali
 
Ndiyo, ni sehemu ya mfumo wa Utawala uliopo, ni wanufaika wakuu wa Utawala wa sasa hivi, na ndiyo maana wameacha Upinzani!
Acha wanufaike waliteseka Sana utawala uliopita
 
Hujui usemalo. Ruto sio tu mlamba asali bali mchonga mzinga kabisa.
Huyu hadi muda huu ni Naibu rais uaani makamu wa rais, hioni anaogelea asali kabisa?
 
Sijui Mbowe ametishwa?
Hata mimi simuelewi kabisa.
Namshauri Lissu ajitenge mapema
 
Nani kakuambia Ruto alikuwa alambi asali
Nani kasema Ruto hakuwa akilamba asali? Mpango uliokuwapo wa kumwengua kundini kumepelekea anguko lao.

Kwa hakika amepambana nao na walipo sasa wanapumulia mashine.
 
Kenya wametuacha mbali sana
 
Hujui usemalo. Ruto sio tu mlamba asali bali mchonga mzinga kabisa.
Huyu hadi muda huu ni Naibu rais uaani makamu wa rais, hioni anaogelea asali kabisa?

Walamba asali ni wenye mamlaka yao. Wamehodhi madaraka ya nchi. Ni nia yao waendelee kutawala wao tu vizazi kwa vizazi.

Ruto alikwisha pigwa chini kama outsider. Kapambana na state machinery yote dhidi yake.

Kwamba hili linawezekana wenye tozo zao salamu ziwafikie.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…