Ruto anaunga mkono busara za Magufuli

Ruto anaunga mkono busara za Magufuli

Mwanafalsafa

Platinum Member
Joined
Jun 24, 2007
Posts
673
Reaction score
865
Kutoka tovuti ya Nation:

Huku kwetu bahati mbaya busara hii ya kutenga muda wa siasa na muda wa kazi imeonekana haina maana. Kampeni zisizokwisha zinaungwa mkono sasa.

1674883617195.png
 
Tangu Uhuru Kenyatta aondoke katika uongozi, Chadema hawakanyagi Kenya kama walivyokuwa wanakanyaga zamani. Nadhani Uhuru aliwapa space na ufadhili kidogo.

Na hii ilitokana na sera ya JPM kuwa upande wa Raila Amolo Odinga
 
Una maana ingekuwa leo Lissu ingebidi aelekee Muhimbili tu wala si Nairobi tena?
 
Kutoka tovuti ya Nation:

Huku kwetu bahati mbaya busara hii ya kutenga muda wa siasa na muda wa kazi imeonekana haina maana. Kampeni zisizokwisha zinaungwa mkono sasa.

View attachment 2497913
Msiwadanganye watu. Ruto hajapiga marufuku mikutano ya vyama vya siasa bali anawashawishi watu wasihudhurie mikutano ya siasa kwa sababu, kwa maoni yake, haina maana kwa sasa.

Kama mwanasiasa, ni sahihi kufanya hivyo. Kazi ya vyama vyama vya siasa na wanasiasa ni kushawishi, mamlaka yao yaishie hapo. Wapo watakaokubaliana na ushawishi, wapo watakaokataa. Wote wapo sahihi.

Lakini kazi ya Serikali ni kusimamia na kutenda kila kitu kwa mujibu wa sheria. Siyo mwanasiasa atumie Serikali kuvunja sheria kwaajili ya kutimiza matamanio yake ya kisiasa. Na hapo ndipo marehemu Rais Magufuli, alipofanya kosa kubwa.
 
Ni vile tu katiba yao.
Huku siku sa100 aseme hvyo uone nini kinafuata
 
Msiwadanganye watu. Ruto hajapiga marufuku mikutano ya vyama vya siasa bali anawashawishi watu wasihudhurie mikutano ya siasa kwa sababu, kwa maoni yake, haina maana kwa sasa.

Kama mwanasiasa, ni sahihi kufanya hivyo. Kazi ya vyama vyama vya siasa na wanasiasa ni kushawishi, mamlaka yao yaishie hapo. Wapo watakaokubaliana na ushawishi, wapo watakaokataa. Wote wapo sahihi.

Lakini kazi ya Serikali ni kusimamia na kutenda kila kitu kwa mujibu wa sheria. Siyo mwanasiasa atumie Serikali kuvunja sheria kwaajili ya kutimiza matamanio yake ya kisiasa. Na hapo ndipo marehemu Rais Magufuli, alipofanya kosa kubwa.
Kuna kitu bado najiuliza!
2016 ni kweli Rais Magufuli aliweka zuio la kufanya mikutano ya siasa kiholela! Kwa maana kila mbunge afanye kwenye eneo lake la utawala sio nje ya eneo lake, ila sasa ilikuwaje mtu kama Mh Mbowe asifanye ata mikutano mi10 tu pae Hai kwenye jimbo lake ila mwisho wa siku ndani ya miaka 5 alifanya mikutano miwili tu ila akawa anataka kuja Dar kufanya mikutano ya kisiasa?

Kwanini Dar na sio Hai? Mbona Msigwa alifanya sana mikutano katika jimbo lake?
 
Katiba inasemaje?

Mbowe alitaka kufanya mikutano Dar kama mbunge wa Hai au kama kiongozi wa kitaifa wa CHADEMA?

Vyama vya siasa vimepewa haki ya kufanya mikutano wakati wote, nchi nzima kutegemea mahitaji ya chama. Kama chama cha siasa hakiwezi kufanya mikutano wakati wote isipokuwa tu mwezi mmoja ndani ya miaka mitano, ni lini kitawapata wananchama na wapenzi? Ni lini kitafanya tathmini ya kuungwa mkono au kukataliwa kwa sera zake?

Katiba inatoa haki ya vyama vya siasa kufanya mikutano, hatuongelei mikutano ya wabunge. Na hakuna mbunge kupitia vyama vya upinzani aliyewahi kuonesha nia ya kutaka kwenda kufanya mkutano wa hadhara kwenye jimbo la uchaguzi lisilo lake. Zuio lile lilikuwa haramu kabisa kisheria na kikatiba.
 
Kutoka tovuti ya Nation:

Huku kwetu bahati mbaya busara hii ya kutenga muda wa siasa na muda wa kazi imeonekana haina maana. Kampeni zisizokwisha zinaungwa mkono sasa.

View attachment 2497913
Tafuta tafsiri ya nene "busara". Magufuli hakuwa na busara hata kidogo, alikuwa mwehu
 
Kuna kitu bado najiuliza!
2016 ni kweli Rais Magufuli aliweka zuio la kufanya mikutano ya siasa kiholela! Kwa maana kila mbunge afanye kwenye eneo lake la utawala sio nje ya eneo lake, ila sasa ilikuwaje mtu kama Mh Mbowe asifanye ata mikutano mi10 tu pae Hai kwenye jimbo lake ila mwisho wa siku ndani ya miaka 5 alifanya mikutano miwili tu ila akawa anataka kuja Dar kufanya mikutano ya kisiasa?

Kwanini Dar na sio Hai? Mbona Msigwa alifanya sana mikutano katika jimbo lake?
Hivi watu wa namna hii bado wapo?
 
Msiwadanganye watu. Ruto hajapiga marufuku mikutano ya vyama vya siasa bali anawashawishi watu wasihudhurie mikutano ya siasa kwa sababu, kwa maoni yake, haina maana kwa sasa.
Ni kweli hajapiga marufuku lakini mtazamo wake ndo unaoendana na Magufuli. Mtazamo wa kwamba kuna wakati wa siasa na wakati wa kazi. Na kwamba wakati siasa ukiisha siasa inatakiwa zikome ili waliochaguliwa wafanye kazi.
 
Mikutano isizuiwe ila siasa isiwe kama vile tupo kwenye uchaguzi kila siku. Kwasasa tudai katiba na hii sio siasa!

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Hata mfanyeje mama kasharuhusu mikutano sasa. Wewe unadhani marehemu alikuwa na akili?
 
Hiyo kashfa ya Golden berg ni wachache tu ambao hawakuwa wazalendo, sikujua hatima yake ilikuwaje! Sio sawa na Tz, ni upigaji wa kijinga.
 
Ndiyo bado tupo tunaojiuliza Mh Mbowe kama mbunge kwanini alishindwa kufanya mikutano katika jimbo lake, ambako kuna wananchi wake waliomchagua ila akawa anang'ang'ana na Dar? Je! Hakukuwa na haja ya kuwasikiliza wananchi wake? Wapiga kura wake hawakuwa na changamoto zozote?
Hivi watu wa namna hii bado wapo?
 
Katiba inasemaje?

Mbowe alitaka kufanya mikutano Dar kama mbunge wa Hai au kama kiongozi wa kitaifa wa CHADEMA?

Vyama vya siasa vimepewa haki ya kufanya mikutano wakati wote, nchi nzima kutegemea mahitaji ya chama. Kama chama cha siasa hakiwezi kufanya mikutano wakati wote isipokuwa tu mwezi mmoja ndani ya miaka mitano, ni lini kitawapata wananchama na wapenzi? Ni lini kitafanya tathmini ya kuungwa mkono au kukataliwa kwa sera zake?

Katiba inatoa haki ya vyama vya siasa kufanya mikutano, hatuongelei mikutano ya wabunge. Na hakuna mbunge kupitia vyama vya upinzani aliyewahi kuonesha nia ya kutaka kwenda kufanya mkutano wa hadhara kwenye jimbo la uchaguzi lisilo lake. Zuio lile lilikuwa haramu kabisa kisheria na kikatiba.
Sababu ulizoweka hapa hazijitoshelezi kueleza kwanini katika jimbo lake hakutaka kufanya mikutano na wananchi wake waliomchagua! Labda uniambie wapigakura wake hawakuitaji mikutano cos walishajutosheleza na hawakuwa na changamoto zozote
 
Msiwadanganye watu. Ruto hajapiga marufuku mikutano ya vyama vya siasa bali anawashawishi watu wasihudhurie mikutano ya siasa kwa sababu, kwa maoni yake, haina maana kwa sasa.

Kama mwanasiasa, ni sahihi kufanya hivyo. Kazi ya vyama vyama vya siasa na wanasiasa ni kushawishi, mamlaka yao yaishie hapo. Wapo watakaokubaliana na ushawishi, wapo watakaokataa. Wote wapo sahihi.

Lakini kazi ya Serikali ni kusimamia na kutenda kila kitu kwa mujibu wa sheria. Siyo mwanasiasa atumie Serikali kuvunja sheria kwaajili ya kutimiza matamanio yake ya kisiasa. Na hapo ndipo marehemu Rais Magufuli, alipofanya kosa kubwa.
Nimeweka bold sentensi ya mwisho. Uki messup tu na mifumo ya sheria na utawala bora, you are in for it. Magufuli alijisahau akajifanya mungu, Cha Mtema Kuni alikiona tarehe 17/ 03/ 21
 
Back
Top Bottom