Kenya 2022 Ruto atashinda kesi, double agent kamuangusha Raila Odinga

Kenya 2022 Ruto atashinda kesi, double agent kamuangusha Raila Odinga

Kenya 2022 General Election
Hawezi kuanzisha fujo maana anajua atamalizia,Maisha yake jela kwani lazima atapelekwa The Hague (ICC). Nchi za,magharibi ambazo zimekita mizizi yake ya investment kenya haziwezi kukubali wasiendelee kunufaika kwa sababu ya tu mmoja.
RAILA hawezi kufungwa!! Kama aliapishwa hakupewa kesa ya uhaini, walichinjana 2007 mbona hakufungwa?

RAILA akifungwa au kuuawa ndio utakua mwisho wa Kenya kutawalika, itakua vita isiyoisha ya kikabila. Kama ingekua rahisi hivyo Wakikuyu wangeshamuua tokea enzi za Moi huko.
 
Sakaja kumbe ni wa Raila?
Igathe pia hakua wa Raila ni mgombea wa Jubilee!! ODM haikua na mgombea maana wanyonyi alijitoa.

Ili context ieleweke Senator ni ODM, Woman rep ni ODM, na Urais kashinda Odinga hapo Nairobi. So logic ni kwamba kama ODM ingeweka mgombea Ugavana kupitia Tim huyo mfoji vyeti angekua anauza miwa sugoi!!

By the way Azimio Ina wabunge wengi Nairobi zaidi ya 70%, na MCAs majority ni Azimio. So we can conclude kuwa Nairobi ni ya ODINGA
 
Naam uo ndiyo ukweli! Raila alichofanya ni kutafuta kila sehem wapi atapatia kaupenyo! Na sijaona wapi anaweza kushinda kwakweli.
Voter suppression ya Kakamega na Mombasa is a serious case, haiwezekani 40% wapige kura ya Urais kisa tu muhuni mmoja afute kura za Ugavana a day before.

Ili upate context national tally average ni 64%. Mind you hizo ni ngome za Raila maana kuanzia Governor mpaka MCA ni ODM majority.
 
hela nyingi aliiba kipindi cha KANu akiwa mkuu wa vijana wa chama walipewa kazi ya kusambaza mapesa mtaani kama rushwa hadi uchumi wa kenya ukaanguka in 1992
Ufisadi wote wanao unless hujui Rail alichukua mabilllions ya pesa kwenye handshake .......muacheni Rutto akapige kazi huyo Rail ashukuru tu Mungu maana hata uchaguzi ukirudiwa ashinde mwaka mmoja wanamuua kenya ipate Rais w kwanza mwanamke ambaye atakuwa anaendeshwa kwa remote control na uhuru kenyatta
Mkuu kama angetaka pesa za handshake si angeomba post serikalini kwani angenyimwa hata "uwaziri Mkuu" ?? Ili afuje pesa vizuri kwa miradi hewa!!

Kingine Raila amezaliwa kwenye Hela, Mzee jaramogi alikua na pesa nyingi na pia Odinga ni established politician wa miaka mingi so ana funds za kueleweka kutoka ndani na nje ya Kenya so sio limbukeni wa pesa kama hao wauza kuku wa Sugoi!!

Kingine Raila hawezi kuuawa he's not that weak, kama ni kifo wangeshamuua zamani sana alipowasumbua tokea Moi mpaka Kibaki!! Why wasimuue 2017 alipojiapisha waje kumuua akiwa Rais? Unadhani nchi itabaki na amani?
 
Unajua

Unajua gavana WA nairobi ni nani? Acha kukariri
Kura za Urais hapo Nairobi Odinga HAJAWAHI kuzidiwa na yeyote awe Kibaki au Kenyatta au Ruto!! Hiyo ni fact.

2. Senator, women rep ni ODM na majority ya wabunge na MCAs ni AZIMIO so ukitaka upate uhalisia usiangalie post moja tu. Nje ya sakaja ni wapi kwingine Ruto kamzidi Raila??

3. Igathe ni chaguo la Kenyatta ila Odinga alikua na mgombea wake Tim Wanyonyi ambaye bila shaka angembwaga Sakkajja asubuhi na mapema coz ni mchapakazi, msomi, yet mlemavu!!
 
RAILA hawezi kufungwa!! Kama aliapishwa hakupewa kesa ya uhaini, walichinjana 2007 mbona hakufungwa?

RAILA akifungwa au kuuawa ndio utakua mwisho wa Kenya kutawalika, itakua vita isiyoisha ya kikabila. Kama ingekua rahisi hivyo Wakikuyu wangeshamuua tokea enzi za Moi huko.
Raila na babake Jara.mogi waliishakaa jela ( kizuizini) muda mrefu tu enzi za Moi na Kenya ilitawalika. Waliachiwa on goodwill kwa kutambua mchango wa mzee wake (Jaramogi) katika kupigania uhuru wa Kenya na hususan kupigania kutolewa jela kwa, mzee Jomo Kenyatta na wakoloni.

Nilichozungumzia mimi ni kupelekwa the Hague na hao hao wazungu sio kushtakiwa na Ruto ndani ya Kenya.
 
Ndio Nasema mbona 2007 hakupelekwa the Hague? Kwani kipi alichofanya Ruto bila kupewa Baraka na Raila?

Moi alijua nguvu ya Odinga ndio maana alimpa uongozi KANU na kama angebaki pamoja na wenzie kina Musyoka then KANU isingekufaga!!

Kusema Raila ni project ya uhuru ni dharau hiyo, hivi kweli Kenyatta utalinganisha na Raila kwa lipi? Wakikuyu tu wamemkataa Uhuru vipi umewahi ona Raila kasalitiwa na ngome yake hata siku moja?

kipindi Odinga anapanga njama za kumpindua Moi huyo Kenyatta alikua anakunywa pombe tu kwenye night clubs ndio Leo aje kumfanya Odinga proxy? Haiwezekani
 
Naona ni kama Kenya imegawanyika nusu kwa nusu Raisi atakaeshinda ana kazi ya kiwaunganisha Ndugu zetu Wakenya.
Hatujagawanyika kaka, mimi nimempigia Raila mara mbili na kati ya miaka kumi hio nimefaidi mengi kutoka kwa serekali ya Uhuru... Naamini itakua ni hivyo hivyo na serekali ya Ruto i.e Wale ambao hawakumpigia pia watafaidi na maisha yataendelea.... Wale ambao watabaki kushindana na kuchukiana ni wale ambao hawana la kufanya maishani, hata kama mtu wao angeshinda bado wangetafuta sababu ya kuendeleza chuki zao...
 
Hotep Bro.
 
Watu wana maneno tayari hukumu imeshatolewa.Kama ni rahisi hivyo sioni haja ya hiyo mahakama ya juu.
 
Ndio Nasema mbona 2007 hakupelekwa the Hague? Kwani kipi alichofanya Ruto bila kupewa Baraka na Raila?

Moi alijua nguvu ya Odinga ndio maana alimpa uongozi KANU na kama angebaki pamoja na wenzie kina Musyoka then KANU isingekufaga!!

Kusema Raila ni project ya uhuru ni dharau hiyo, hivi kweli Kenyatta utalinganisha na Raila kwa lipi? Wakikuyu tu wamemkataa Uhuru vipi umewahi ona Raila kasalitiwa na ngome yake hata siku moja?

kipindi Odinga anapanga njama za kumpindua Moi huyo Kenyatta alikua anakunywa pombe tu kwenye night clubs ndio Leo aje kumfanya Odinga proxy? Haiwezekani
Unakumbuka BBI? Kama ingefanikiwa na pia kama Raila angeshinda Kenyatta asingeondoka mikono mitupu bado angeendelea kuwa na nguvu fulani nyuma ya Odinga. Kusema kuwa wakati Raila anapanga kumpindua Moi Kenyatta alikuwa anakunywa bia night club ni kakashifu kwani sio lazima kila mtu wakati wote awe anafanya jambo linalofanywa na mwenzake. Wakati wa Moi Uhuru hakuwa interested na mambo ya siasa alikuwa anashughulika na biashara za familia. Moi katika kulipa fadhila kwa Mzee Jomo Kenyatta kwani bila yeye asingepata nafasi ya kuwa rais wa Kenya, aliamua kuirudisha KANU kwa Kenyatta na kumteua Uhuru kugombea urais kupitia chama hicho kinyume cha makubaliano waliyoafikiana na Raila wakati anawarudisha KANU kuwa mchakato wa kumpata mgombe urais kwa tiketi ya KANU utakuwa wa kidemokrasia; kitendo hicho ndicho kilichowaondoa Raila, Mwai Kibaki na wengine toka KANU mwaka 2003 na wakaungana kupambana na KANu na ili kugawa kura za Wakikuyu huku makabila mengine yakimuunga mkono mgombea wao, walimteua Kibaki ambaye niu mkikuyu ili apambane na Uhuru mkikuyu pia; plan hiyo ilifanikiwa na Kibaki akaukwaa urais.

Baada ya Kibaki kuwa rais hakutekeleza makubaliano waliyoafikiana ya kurekebisha katiba na kumfanya Raila waziri mkuu hivyo wakafarakana pia. Kibaki baada ya kufarakana na kina Raila akaungana na Uhuru kwa makubaliano kuwa Uhuru amuunge mkono Kibaki mwaka 2007 na kisha Kibaki naye amuunge mkono Uhuru mwka 2012. Bada ya Kibaki kushinda mwaka 2007 kwa kipindi cha pili Raia alianzisha vurugu na abaada ya usuluhishi naRaaila kufanywa waziri mkuu vurugu zilipoa. Kwa kuwa Marekani chini ya Obama walikuwa wanamtaka sana Raila awe Rais mwaka 2012 na ili kumzuia Uhuru asigombee mwaka huo ndipo ikatengenezwa kesi The Hague ambako Uhuru akabambikiwa kuwa alichoichea vurugu lakini lengo likiwa ni kumzuia asigombee mwaka 2012 kama ataakuwa amefungwa tayari. Ili kuweka balance, ilibidi upande wa Raila nako apatikane mtu wa kushtakiwa pamoja na Raila na kwa kuwa mhusika wa vurugu alikuwa Raila ambaye walitaka ndiyo awe rais basi upande wa Raila wakamtoa kafara Ruto ili ashtakiwe The Hague, hapo ndipo uhasama wa Ruto na Raila ulipoanzia. Kwa uhuru yeye hakutolewa kafara na Kibaki ndio maana uhusiano wao haukuvurugika. Kesi hiyo ndiyo iliyowaunganisha Ruto na Uhuru na wakaweka mikakati ya pamoja ya kuikabili na kutengeneza muungano wa kisiasa kwa kutambua nguvu kubwa ya makabila yao na uchaguzi wa mwaka 2012 Ruto akamsaidia Uhuru kushinda na kwa makubaliano kuwa mwaka 2022 Uhuru pia amsaidie Ruto kushinda na makubaliano hayo yalikuwa ni ya kikabilazaidi kuliko watu wawili tu.

Wakikuyu hawajamgeuka Uhuru, ila wamemtosa baada ya kuoana Uhuru amekengeuka kwa kukiuka makubaliano ya kiapo aliyoyafanya na Ruto na wao wakaamua kusimamia kiapo chao ndio maana wamempigia kura Ruto na chama cha Uhuru cha Jubilee hakikushinda ubunge wala useneta huko kikuyu. Wakikuyu sio watu wa kuburuzwa wala sio wanafiki kama watanzania ni watu wanaojielewa.

Raila hawezi kuanzisha vurugu Kenya kwani anajua fika kitakachompata. Wazungu wa magharibi hawawezi kukubali mabilioni ya pesa wanayoingiza toka Kenya kama faida ya uwekezaji wao ihatarishwe na tamaa ya Raila ya kutaka urais watamshughulikia mara moja. Wewehushangai kwa nini kablaya uchaguzi Raila alienda Uingereza na Marekani.
 
Ruto has ended Kenyatta's, Moi's and Odinga's political Careers
 
Naam ile nchi jirani iliyojipambanua kwamba ina majaji wenye akili timamu na judiciary yenye nguvu jumatatu inaweka historia nyingine kwa kuendesha kesi nzito ndani ya siku chache na kutoa maamuzi

Kesi hiyo ambayo kuna baadhi ya nchi majaji kama wangepewa waisikileze basi kila dakika wangekuwa kwenye simu kupata malekezo kutoka juu imekuwa na mvuto hadi katika nchi yenye matatizo ya kuibia watu bando la internet

Naam Baba Raila byebye kwishney , mtaalamu wako wa IT bwana Njoroge kakusaliti vibaya sana ka mislead ma lawyers haswa miss soweto wakajichoresha mahakamani,Ruto hatari sana

View attachment 2343408View attachment 2343409View attachment 2343410
William Ruto the assistant president of Venezuela kenya
 
Yametimia hongereni kenya kwa system nzuri ya judiciary wengine huku ni comedy
 
Back
Top Bottom