Kenya 2022 Ruto atashinda kesi, double agent kamuangusha Raila Odinga

Kenya 2022 Ruto atashinda kesi, double agent kamuangusha Raila Odinga

Kenya 2022 General Election
Hivi ile form 34A walionesha kwamba Mvenezuela aliingilia server ya IEBC ilijibiwaje?
Hakuna uingiliaji ila picha ya fomu ilipigwa juu ya kava ya registre yenye jina la huyo Mvenezuela
IMG_20220902_145326.jpg
IMG_20220902_155526.jpg
 
Ruto kacheza hii game smart sana, leo ushahidi wa huyo njoroge uliotumiwa na ma lawayers wa Raila umegeuka kichekesho
Raila kaangushwa na vingi, hakuwa hata na ma agents karibu asilimia 50 ya pllling stations, kina Joho, Junet Mohamed walikula hel ya agents wakaweka nguvu mombasa tu na kuna mazungumzo ya simu walirekodiwa wakimkebehi Raila
Subiri jumatatu baada ya hukumu timbwili litakalozuka huko azimio
kwa conclusion ya leo ya jaji mkuu Koome naona kama jumatatu atakataa madai ya servers kudukuliwa sababu forms physically zilihesabiwa ila atashauri tume ya uchaguzi ifanyiwe marekebisho
Ufanyiwe marekebisho kwa makosa yapi?? Hayo makosa si ndio yatasababisha kurudiwa kwa uchaguzi??
 
Mkuu Ruto ni fisadi ni suala la muda tu tutakuja wote kukumbushana humu. Haiwezekani "muuza kuku" apate uongozi awe billionaire!! Hapana it's not right!! Majaji wawe wazalendo wafute matokeo in fact mahakama hiyo hiyo ilimkuta Rigathi na hatia ya kufuja mabilioni ya Nairobi county so they are not fit for office!!

NB: Raila kaanza siasa Kenyatta akiwa Bado ananyonya Maziwa!! In fact it's Raila who partly ended uhuru in 2002, how comes awe project ya junior kama Uhuru?
Kesi gani Rigathi alikutwa nayo, ile ya 200 million KES ambayo ilitangazwa leo kwenye majukwaa na kesho yake kina Odinga wakaibandika kwenye mabango ya kampeni wakimchora Gachagua kama katuni ameshika fuko la pesa?

Odinga ana watu wengi sana nyuma na kila sekta ya serikali ila hali ni tete. Kama tume watu wanne wanajitoa kwa kushindwa kujumlisha, sembuse mahakama kutaja kesi. Sisemi ni ya kutungwa, ila siondoi kuamini uwezekano kwamba ni feki.
 
Mbona mwaka huu dosari ndio nyingi. Kumtangaza matokeo haraka bila kufikia muafaka wa makamishna. Chebukati alikuwa na upande wake kuanzia zamani. Ndio maana wakacheza rafu Mombasa na kakamega maana wangejitokeza wengi.
Kutangaza matokeo siku kabla ya deadline kuna shida gani kama wameona matokeo tiyari yamekamilika. Hata ungekuwa wewe ndio Chebukati, ungesubiri watu waliokimbilia Serena Hotel kuitisha press conference kujitoa uhusika wa matokeo na kulala hapo siku mbili bila kubadilisha hata nguo ili mjadili matokeo siku ya mwisho?

Tofauti zingebaki maana wanne wale walishakimbia hata wangeongeza wiki kutangaza matokeo bado sintofahamu ingekuwepo
 
Bila kuangalia uhasi na uchanya wa hoja mbali mbali hapo supreme court na matokeo yatakuaje...
Kesi inapigwa kama ile series ya family court. Inavutia sana.

Kila lenye kheri wa kenya.
 
Hawawezi upeo wao kwa sasa ni mkubwa mnoo, ila lazima Raila atalazimisha machafuko sababu hata hii kesi inayoendelea alitaka wafuasi wake wafanye sit down nje ya mahakama baadaaye akaghairi, maskini wa kibera walimuambia wamechoka kutumika na mtu anayedai kuibiwa kila uchaguzi tena safari hii akisaidiwa na incumbent
Kenya bado hamjapigana mpaka Leo, Sisi tunasubiri mchapane
 
hahahahaha kwa taarifa yako wakikuyu weeeengi wamempa ruto hawataki mjaluo labda watu wa kisumu ndiyo watakunja, cha kwanza Ruto kaahidi kufanyia kazi ni kushusha bei ya unga, in few days akifanikisha hakuna atakumbuka ujinga wa Raila
Sasa Nyie ni wa kabila sana si tunasubiri mpigane ili tuwauzie mahindi

Nashauri Wakikuyu anzisheni vita ili sisi tufanye biashara

Kenya nchi ya kishamba sana, Yaani karne ya 21 unawaza ukabila

Hivi mngekuwa hapa Tanzania tuna makabila zaidi ya 120 lakini huwezi muuliza mtu kabila tumeoana na kuchanganyika sana
 
Hustler anaapishwa tarehe 13....huyo Mganga hana watu wa mikakati na washauri wazuri linapokuja suala la kushinda uchaguzi...

Raila hajui kushinda uchaguzi ni mikakati...alidhani deep state itaagiza atangazwe hata asiposhinda...imekula kwake...aende Bondo apumzike sasa
Ni kweli, lakini pia hakuwa na backup kumsoma Kunyata kama anamsaidia kwa dhati au ana ajenda nyuma ya pazia. Hadi Kikwete anamaliza game kumsaidia Ruto kwa ombi la Kunyata, Raila alikuwa bado anamwamini sana Kunyata.

Raila alisahau kuwa urafiki wake na Magufuli ambaye alikuwa adui wa Kunyata, umekufa. Kumbe bado Kunyata ana jambo moyoni akiumizwa na urafiki wa Raika na Magufuli.

Siasa mchezo mchafu.
 
Amos wako mwnasheria mkuu wa zamani wa kenya, afisa mkubwa jeshi mwenye nyota tatu jenerali, mkuu wa jeshi la polisi na wengine wa baraza la usalama la kenya pamoja na katibu mkuu wa chama cha raila, Raphael Tuju walimtembelea chebukati saa tisa usiku siku anatangaza matokeo kufosi ayabadili akakataa

alipewa na ahadi ya 500 millions ya kenya akakataa, hapo chebukati na wenzake wawili walisimamia kucha tu ila jamaa kama nchi wamepiga hatua sana hapa miaka 2 imepita kuna forms mahera hataki kuziweka mtandaoni kama sheria inavyosema watu walinganishe mahesabu
kenya forms 46,000 zilipanda in 2 days

IGP wa kenya kabla ya hii kesi kuanza alishanusa aibu akaomba likizo ya kimatibabu nafasi yake inakaimiwa na msaidizi wake aliyetuliza fujo za wafuasi wa Raila pale boma na matokeo yakatangazwa
Mke Wa Amos Wako ni Justice Mwilu

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Ni mchezo ambao raila aliucheza. Kama angetaka kuwa Rais angegombea urais kwa chama chake Cha LDP. Lakini hakutaka hivyo, akamnadi Kibaki kwa msemo wa Kibaki tosha. Nadhani Raila angestaafu pamoja na Kibaki ingekuwa nzuri zaidi.
Sio mchezo ilikuwa ni tamaa kama zilivyo mfanya tena kujiunga na Uhuru 2018 licha ya kumtuhumu kwa kumuibia kura na ufisadi, akidhani kuwa Uhuru atamuachia nchi, kapigwa tena chenga nyingine
 
Ruto kacheza hii game smart sana, leo ushahidi wa huyo njoroge uliotumiwa na ma lawayers wa Raila umegeuka kichekesho
Raila kaangushwa na vingi, hakuwa hata na ma agents karibu asilimia 50 ya pllling stations, kina Joho, Junet Mohamed walikula hel ya agents wakaweka nguvu mombasa tu na kuna mazungumzo ya simu walirekodiwa wakimkebehi Raila
Subiri jumatatu baada ya hukumu timbwili litakalozuka huko azimio
kwa conclusion ya leo ya jaji mkuu Koome naona kama jumatatu atakataa madai ya servers kudukuliwa sababu forms physically zilihesabiwa ila atashauri tume ya uchaguzi ifanyiwe marekebisho
Hiv tunaposema Saver zilidukuliwa, zilidukuliwa kwa malengo gani? Mi naona Raila alijaribu tu kutupa karata yake Court huku akiweka mitege mingi ili aone wapi anaweza kupatikana mtu kufanya lolote ila kimsingi sijaona mahala popote penye mashiko!

Inshort ata IEBC waliwah kusema wale Wavenezuela na watu wao, walikuja pale nchini kwa kazi maalumu na ndiyo maana baadhi ya nyaraka zina mpaka majina yao.

Mi sion cha kurekebisha kwenye tume zaidi tuseme hakuna uchaguzi utafanyika isijutokeze kasoro ata moja! Kasoro ilanawesa kubwa hiyo ndo inaleta mkanganyiko ila kasoro za IEBC ni ndogo kwakweli na hazina impact yoyote.
 
Hawawezi upeo wao kwa sasa ni mkubwa mnoo, ila lazima Raila atalazimisha machafuko sababu hata hii kesi inayoendelea alitaka wafuasi wake wafanye sit down nje ya mahakama baadaaye akaghairi, maskini wa kibera walimuambia wamechoka kutumika na mtu anayedai kuibiwa kila uchaguzi tena safari hii akisaidiwa na incumbent
Hawezi kuanzisha fujo maana anajua atamalizia,Maisha yake jela kwani lazima atapelekwa The Hague (ICC). Nchi za,magharibi ambazo zimekita mizizi yake ya investment kenya haziwezi kukubali wasiendelee kunufaika kwa sababu ya tu mmoja.
 
Hiv tunaposema Saver zilidukuliwa, zilidukuliwa kwa malengo gani? Mi naona Raila alijaribu tu kutupa karata yake Court huku akiweka mitege mingi ili aone wapi anaweza kupatikana mtu kufanya lolote ila kimsingi sijaona mahala popote penye mashiko!

Inshort ata IEBC waliwah kusema wale Wavenezuela na watu wao, walikuja pale nchini kwa kazi maalumu na ndiyo maana baadhi ya nyaraka zina mpaka majina yao.

Mi sion cha kurekebisha kwenye tume zaidi tuseme hakuna uchaguzi utafanyika isijutokeze kasoro ata moja! Kasoro ilanawesa kubwa hiyo ndo inaleta mkanganyiko ila kasoro za IEBC ni ndogo kwakweli na hazina impact yoyote.
Ukifuatilia kwa makini utaona Raila anewekeza madai yake kwenye angles nyingi ili mradi tu angle japo moja inaweza kutick matokeo yakatenguliwa. Anajua fika hakushinda uchaguzi ndio maana hasemi alipata kura ngapi kwa mujibu wa takwimu ambazo anazo ili ziwe basis ya kubishania. Kabla ya natokeo kutangazwa Raila na makamo wake walikutana na wabunge maseneta na magavana wao wateule na kusema waneshinda uchaguzi na wanasubiri Tume imtangaze tu katika mkutano huo hakuleta madai ya mifumo ya IT kuingiliwa wala fomu kughushiwa. Alipoona kuwa ameshindwa na Tume inataka ku.tangaza Ruto kuwa, mshindi akafanya jitihada huku akisaidiwa na serikali na makamishna wanne wa Tume ili itangazwe hakuna mgombea aliyepata asilimia 50 ili uchaguzi urudiwe. Hata baada ya Ruto kutangazwa mshindi walikuja na mahesabu yeye, azimio na .makamishna 4 wa Tume kuwa Chebukati amedanganya hesabu kuwa ushindi wa Ruto haufikii asilimia 50 na walionyesha wazi calculation hizo. Sasa mahakanani waneegenea zaidi kwenye forgery ya kimtandao kuwa mfumo wa IT ulikuwa compromised na sio tena Ruto hakushinda kwa asilimia 50. Kila wakati basis ya kutokubalina na ushindi wa Ruto inabadilika.
 
Naam uo ndiyo ukweli! Raila alichofanya ni kutafuta kila sehem wapi atapatia kaupenyo! Na sijaona wapi anaweza kushinda kwakweli.
 
Kutangaza matokeo siku kabla ya deadline kuna shida gani kama wameona matokeo tiyari yamekamilika. Hata ungekuwa wewe ndio Chebukati, ungesubiri watu waliokimbilia Serena Hotel kuitisha press conference kujitoa uhusika wa matokeo na kulala hapo siku mbili bila kubadilisha hata nguo ili mjadili matokeo siku ya mwisho?

Tofauti zingebaki maana wanne wale walishakimbia hata wangeongeza wiki kutangaza matokeo bado sintofahamu ingekuwepo
Mkuu sheria inataka uwazi na verification ya matokeo. Hawakutangaza matokeo ya majimbo 27 yaliyokua verified akakimbilia kutangaza final results!!!

Sheria hairuhusu Hilo, hata live streaming ya tallying kwenye screen za BOMAS ilizimwa unadhani uwazi uko wapi hapo kisheria?

Kisheria hapo inaruhusu uchaguzi kufutwa thou maana sheria ni sheria tu haiangalii "busara"
 
Back
Top Bottom