Ruto: Vile Wakenya wameikataa "Finance Bill", tutakopa Tsh. Trilioni 20.6 (Ksh.1 T) ili nchi iweze kujiendesha

Ruto: Vile Wakenya wameikataa "Finance Bill", tutakopa Tsh. Trilioni 20.6 (Ksh.1 T) ili nchi iweze kujiendesha

Hivi kuna nchi hapa duniani inaifikia China katika kuendesha miradi mikubwa mikubwa ndani na nje ya nchi yao ya mabilioni ya pesa.

Juzi tu hapa wamezindua Shenzhen-zhongshan bridge bonge la daraja.

Mbona wachina hawalalamiki haya yanayo lalamikiwa sehemu kubwa ya Afrika na pamoja uliyo lalamikia wewe ?
China haifugi wezi wala machawa.
 
Maendeleo hayasubiriwi hufuatwa of course uhitaji upo.
Uhitaji upi huo? Mwakani sio mbali,utapata majibu ya hasara usije kimbia.

Yaani reli ya Kenya ambayo imejengwa kwenye uhitaji mkubwa inaleta hasara ndio ije kuwa hiyo ya Tzn ambayo Haina chochote Cha maana Cha kubeba ilete faida? Kwa economic feasibility gani mliyofanya au hisia zenu?
 
Wachina nchi yao ni ya Kijamaa kama ilivyo Cuba na Urusi kwa hiyo nchi zao ni vigumu kuandamana kwa vile kule hakuna Demokrasia ya Mfumo wa Vyama vingi.
Urusi sio nchi ya kijamaa, Cuba sasa wanafanya reforms kama za China na Vietnam.

Hata huo ujamaa wa China una mabadiliko mengi kila pale watakapo ona uhitaji wa maendeleo ya taifa lao, wana utafsiri vile wao wanavyo taka.

Unafikiri wachina hawaandamani wenda huwafuatilii kabisa kwa ufupi huwafahamu.

Demokrasia ya vyama vingi hata Tanzania haipo, kwa nini hayupo kama hao wachina ?
 
Rais wa Kenya ,William Ruto amesema kutokana na Wananchi wa Kenya kuukataa mswaada wa sheria ya Bajeti Maarufu kama Finance Bill uliozua Maandamano makubwa, Serikali yake italazimika kukopa Zaidi ya Shilingi Trilioni 20.6 ( Ksh.1Trilioni) za kulipia Madeni na kugharamia mambo mengine ya serikali.

Ruto amesema hatua hiyo ni sawa na kurudi nyuma miaka 2 😁😁👇👇

View: https://twitter.com/bbcswahili/status/1807844155281797191?t=_0LXMMUVV_ybPZs65UYj9A&s=19

My Take
Kenya imefika huko kutokana na Mamiradi mengi makubwa chini ya Rais Hayati Mwai Kibaki na Reli ya SGR ya Uhuru Kenyatta.

Mwenzako akinyolewa zako tia maji.👇👇

View: https://www.instagram.com/p/C86wRT4tMqV/?igsh=eDB1ZWs2YmNvZDJ4

Mnaposhangilia Sgr mkae mkijua ni mikopo na italazimika kuja kulipwa. Hakuna sababu ya kukurupukia miradi mikubwa ya kupigia picha za kisiasa "cosmetic projects" kama hakuna huo ulazima.

Pia soma Marais Museveni wa Uganda & Mwinyi wa Zanzibar Wamekataa Itikadi za Kijamaa, Bajeti zao kugharamiwa na Mikopo kwa 60%

Kenya inajulikana ni nchi ya kifisadi,bajeti inayowekwa katika miradi na uhalisia wa thamani ya mradi ni tofauti.
Kenya wamejenga SGR yao kwa pesa nyingi kuliko yetu ilhali kiuhalisia hawakutakiwa kutumia pesa nyingi hivyo.
Anguko la Kenya ni viongozi wake wenyewe kwa kuzidisha sifuri.
 
Reli inaleta maendeleo gani? Kule kwenu Mbozi Kuna Tazara imewaletea maendeleo? 🤣🤣
Usafirishaji wa bidhaa kutoka Mbozi kwenda sehemu nyingine kama Zambia na nje ya Tanzania kupitia bandari ya Dar es Salaam.Vile vile imetengeneza ajira kwa wakazi wa Mbozi na maeneo yote ilikopitia na kupunguza umaskini.Pia sehemu zote ambako Tazara imepita kiwango cha ujinga ni kidogo.Na reli ya TAZARA imezalisha miji mingi tofauti na sehemu ambako TAZARA haijapita.Vile vile TAZARA imeweka mawasiliano mazuri baina ya Tanzania na Zambia.
 
Kenya inajulikana ni nchi ya kifisadi,bajeti inayowekwa katika miradi na uhalisia wa thamani ya mradi ni tofauti.
Kenya wamejenga SGR yao kwa pesa nyingi kuliko yetu ilhali kiuhalisia hawakutakiwa kutumia pesa nyingi hivyo.
Anguko la Kenya ni viongozi wake wenyewe kwa kuzidisha sifuri.
Kenya Kuna Ufisadi vs Tanzania miradi ya kukurupuka.

Sitarajii Tzn kufikia hatua ya Kushindwa kulipa deni ila hakuna faida itakuja kuletwa na hiyo Sgr zaidi ya hasara Kila mwaka.mfano mzuri ni Tazara na meter gauge ya TRC.
 
Ndio kwani wapi hazikutumika kama ilivyokusudiwa? Shida ni kuanzisha miradi ya Kisiasa ambayo Haina Tija kiuchumi eg Sgr yenu Ina Tija gani kiuchumi?
Kenya miradi mingi imeendeshwa kiupigaji kaka.
Kenya ufisadi ndio umewamaliza,kuna daraja moja county nimeisahau pale Kenya ukitakiwa limejengwa kwa hiyo gharama unaweza ukatukana mpaka kesho.
Kenya wanaiba mpaka kujisahau.
Kama SGR kwa reli gani hasa itumie gharama ile na reli ina kilometa fupi mkuu!?
 
Kenya Kuna Ufisadi vs Tanzania miradi ya kukurupuka.

Sitarajii Tzn kufikia hatua ya Kushindwa kulipa deni ila hakuna faida itakuja kuletwa na hiyo Sgr zaidi ya hasara Kila mwaka.mfano mzuri ni Tazara na meter gauge ya TRC.
Metre gauge ya TRC ni wasimamizi ndio hawaiendeshi ipasavyo,ila TRC huwa haizalishagi hasara kwa kiwango hicho.
SGR kama itasimamiwa vizuri italeta faida mkuu,ila NI KAMA ITASIMAMIWA VIZURI.
Shida Tanzania tunafeli usimamizi.
 
Kipi kiliwahi simamiwa na Serikali hapa Tanzania kikaleta faida kibiashara?
 
Timing ya miradi na Tija ya miradi.Tzn hii ilikuwa inahitaji hayo ma Sgr na mandege ya mabilioni.kwa Matrilioni? Hata wakoloni walijenga reli pale tuu kulikopkuwa na mzigo wa kubeba.
Uhitaji upo,sema hio miradi ilitakiwa iende na mwenye vision yake,,,,maana shida inakuja kwenye usimamizi ila uhitaji upo
 
Back
Top Bottom