Ruvuma: Askari Polisi wamchoma Singe Mwenyekiti wa Kijiji baada ya Mwenyekiti huyo kugonga usiku Kituoni akitaka huduma

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,566
Reaction score
4,013
Mwenyekiti wa ulinzi wa kijiji cha Peramiho A mkoani Ruvuma ambaye pia ni mwenyekiti wa kitongoji cha Mtakuja Pastorius Mbuya amejeruhiwa kwa kipigo cha askari polisi waliochukizwa na mwenyekiti huyo kumpigia simu mkuu wao wa kazi na kuwagongea usiku wakati kituo cha polisi kimefungwa.

Mbuya alienda kituoni hapo saa sita usiku akiwa na kijana ambapo polisi walikataa kumshughulikia baada ya kukuta kituo cha polisi kimefungwa hivyo kitendo cha kugonga kiliwachukiza askari hao ndipo wakampiga na kumchoma singe ya bunduki mguuni na mkononi

Mwenyekiti aliyechomwa Singe na Askari Polisi

Dereva wa boda boda Alifa Ausi aliyempeleka Bw.Mbuya kituo cha polisi kushughulikia suala la mwanafunzi anasema alishudia polisi wakimtukana matusi mwenyekiti wa kitongoji kabla ya kumpa kipigo kilichomjeruhi

Mkuu wa wilaya ya Songea Pololet Mgema amesema atalifuatilia suala hilo na kuchukua hatua kwa kuwa linaondoa imani ya jeshi la polisi kwa wananchi

Akizungumza kwa simu kamanda wa polisi wa mkoa wa ruvuma ACP Simon Marwa amesema hawezi kulizungumzia suala hilo kwa kuwa liko kwenye uchunguzi
 
Kwahio sare alio vaa lazma upelelezi ukamirike amini
 
Police Lazima Waheshimiwe Ndugu Zangu Mjifunze Kuchagua
 
Huwa nasikia huko usiku ukiacha mlango wazi unakuta tembo na wanyamapori kibao wako ndani
 
Hao wamalizane wenyewe,watoto wa baba mmoja si vema kuingilia ugomvi wao!
 
Mwenyekiti wa ulinzi wa kijiji cha Peramiho A mkoani Ruvuma ambaye pia ni mwenyekiti wa kitongoji cha Mtakuja Pastorius Mbuya amejeruhiwa kwa kipigo cha askari polisi waliochukizwa na mwenyekiti huyo kumpigia simu mkuu wao wa kazi na kuwagongea usiku wakati kituo cha polisi kimefungwa.

Mbuya alienda kituoni hapo saa sita usiku akiwa na kijana ambapo polisi walikataa kumshughulikia baada ya kukuta kituo cha polisi kimefungwa hivyo kitendo cha kugonga kiliwachukiza askari hao ndipo wakampiga na kumchoma singe ya bunduki mguuni na mkononi

Dereva wa boda boda Alifa Ausi aliyempeleka Bw.Mbuya kituo cha polisi kushughulikia suala la mwanafunzi anasema alishudia polisi wakimtukana matusi mwenyekiti wa kitongoji kabla ya kumpa kipigo kilichomjeruhi

Mkuu wa wilaya ya Songea Pololet Mgema amesema atalifuatilia suala hilo na kuchukua hatua kwa kuwa linaondoa imani ya jeshi la polisi kwa wananchi

Akizungumza kwa simu kamanda wa polisi wa mkoa wa ruvuma ACP Simon Marwa amesema hawezi kulizungumzia suala hilo kwa kuwa liko kwenye uchunguzi
Mbuya, hata mimi ningedhani ni Chadema.
 
Mbuya ni mkurya anafanya nini songea?

ujeuri wa Musoma ana peleka Ruvuma hajui kuwa na mapolisi huko ni Wakurya hivo wamekutana walewale moto ukawaka. + U-ccm kwa CCM. watasuruhishana kwa kabila lao sasa hapo mtu baki atajua?

na huyo kamanda wapolisi ni hao hao! ''Muraa nke nkebhayeee! waitu'' chincha Mbusi ture kichuree ghwansa! hayana aibu haya majamaa, ukute alikuwa na Sime kuinoni Poti aka muwahi Bhort kwa singe chomaa! up! up! up!

duuu! alijua huyu nikifanya kosa tu atanimaliza kimasihara!
 
Mkuu kina mbuya songea n wengi sana tena hasa maeneo ya peramiho iliwahi ishi eneo hilo ni wangoni sasa sijajua muingiliano Wa majina haya
Mbuya ni mkurya anafanya nini songea?

ujeuri wa Musoma ana peleka Ruvuma hajui kuwa na mapolisi huko ni Wakurya hivo wamekutana walewale moto ukawaka. + U-ccm kwa CCM. watasuruhishana kwa kabila lao sasa hapo mtu baki atajua?

na huyo kamanda wapolisi ni hao hao! ''Muraa nke nkebhayeee! waitu'' chincha Mbusi ture kichuree ghwansa! hayana aibu haya majamaa, ukute alikuwa na Sime kuinoni Poti aka muwahi Bhort kwa singe chomaa! up! up! up!

duuu! alijua huyu nikifanya kosa tu atanimaliza kimasihara!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hao ni maswahaba kiimani na matendo hakuna shida watamalizana kifamilia sie wengine wa pembeni tukiingilia tutaonekana wapambe nuksi.
 
Back
Top Bottom