Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
RUWASA YAENDELEA KUFANYA VIZURI MUSOMA VIJIJINI: MRADI WA MAJI WA CHUMWI-MABUIMERAFURU UNAENDA VIZURI
Maji ya Ziwa Victoria yaendelea kusambazwa Musoma Vijijini.
Jimbo la Musoma Vijijini lenye Kata 21 zenye jumla ya Vijiji 68 limezungukwa na Ziwa Victoria.
Utekelezaji wa Mradi wa maji ya bomba wa Chumwi- Mabuimerafuru unaendelea vizuri chini ya usimamizi mzuri wa RUWASA.
Ujenzi unaoendelea kwa wakati huu ni:
*ujenzi wa TENKI lenye ujazo wa LITA 300,000 Kijijini Mabuimerafuru.
*ujenzi wa vioski vya maji kwenye Vijiji vya Chumwi na Mabuimerafuru.
Mradi huu una thamani ya Tsh bilioni 1.7 na umepangwa kukamilishwa kabla ya tarehe 30.7.2023
Baadae, sehemu ya pili ya Mradi huu (LOT II) ni ya ujenzi wa miundombinu ya kusambaza maji kwenye Vijiji vya Lyasembe na Murangi.
TAARIFA YA MIRADI MINGINE :
*Mradi wa Tsh bilioni 4.75 wa kusambaza maji ya bomba kwenye Kata za Tegeruka (Vijiji 3) na Mugango (Vijiji 3) unakaribia kuanza.
Mkandarasi ameishapatikana, na taratibu za mkataba zinakamilishwa.
Maji ya Kata hizi 2 yatatoka kwenye Bomba la Maji la Mugango-Kiabakari-Butiama ambalo limepangwa kukamilika kabla ya tarehe 30 Juni 2023.
*Usanifu wa miundombinu ya usambazaji wa maji ya bomba kwenye Kata za Busambara na Kiriba unakaribia kukamilika.
Kata hizi 2 zitasambaziwa maji kutoka kwenye TENKI la MLIMA KONG lenye ujazo wa LITA 500,000. Maji ya Tenki hili yatatolewa kwenye Bomba la Maji la Mugango-Kiabakari-Butiama.
Fedha za usambazaji wa maji ya bomba kwenye Kata za Busambara na Kiriba zipo, na utekelezaji utaanza hivi karibuni, Julai 2023
Musoma Vijijini tunaendelea kuishukuru sana Serikali yetu chini ya uongozi mzuri wa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutusambazia maji ya bomba vijijini mwetu - Ahsante Sana!
Usisahau kutembelea TOVUTI ya Jimbo letu ambay ni : www.musovijijini.or.tz
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijijini
www.musomavijijini.or.tz
Tarehe:
Jumamosi, 1.4.2023