Well & good. Tunaomba huko mbeleni badala ya kununua magari zaidi, ni vyema wakajenga ofisi kila mkoa. Nina uhakika hayo magari hayapungui 70m@, lakini 70m tunaweza kununua eneo la heka moja+ kila mkoa kwa bajeti isiyozidi 10m. Na kujenga ofisi ya 60m, ambayo mbali ya jengo, kutakuwa na eneo kubwa la wazi nyuma ambalo litaezekwa kwa bati na kutumika kama sehemu ya mikutano ya ndani. Ukishakuwa na ofisi za kudumu, ni rahisi chama kuendelea kuwa na sehemu sahihi za kukutana, hata nyakati za hujuma. Hiyo itapelekea kutokuhitaji vibali kwa ajili vya mikutano ya ndani. Na kwa hapa Dar Nina uhakika ikitengwa 500m, kuna uwezekano wa kujenga jengo la ghorofa mbili au tatu litakalokuwa ofisi za kisasa za chama.