Ruzuku ya vyama vya siasa haitokani na Wabunge wa Viti Maalum

Ruzuku ya vyama vya siasa haitokani na Wabunge wa Viti Maalum

SAWA.
Na hili la kutotambua na kushiriki katika mambo yatokanayo na uchaguzi haramu je? Au hayo yalikuwa ni matamshi ya kufurahisha watu tu?
Haya maswali yako naona yanajibika, tatizo naona kujibu naweza haribu mantiki ya mleta mada, hivyo kwangu ni vyema akajibu mwenyewe.
 
Unajitekenya afu unacheka mwenyewe

Sasa ndo mnakubali kuwa uchaguzi ulikuwa halali

Kumwamini mpinzani LAZIMA uwe chizi
wewe ndio chizi huko kwenye lichama lenu la majiz ya kura ila mamayenu amewanyoosha mpaka hamjui mfanye nini na 2025 mtakuwa vichaa kabisa maana bukusaba hamtaiona tena.
 
Kwa kutetea huku swala la ruzuku, mnaukubali uchaguzi wa 2020 au hamuukubali? 😂😂😂 kuwa na tonge mdomoni tena la moto lazima likuwie
Ugumu kuongea unabaki unamung’unya tu na kutoa moshi mdomoni kama dragon
 
Chama kimepoteza mvuto baada ya wachache kulamba asali..hata wewe Erythrocyte ni vile hujafikiwa na asali!!
Wako kimkakati Zaidi wanaongea hoja dhaifu ili kupoteza uungwaji mkono Wa chama kwa wananchi
chama kupoteze mvuto kwa kuwa lumumba bukusaba amekoment jf, by the way mamayenu anaenda kukabodhiwa kadi ya chadema au nguruwe wa lumumba hio habar hamna, pia nawakumbasha kuwa katibu mkuu wenu anamikutano ila mmemtelekeza.
 
Kwa kutetea huku swala la ruzuku, mnaukubali uchaguzi wa 2020 au hamuukubali? 😂😂😂 kuwa na tonge mdomoni tena la moto lazima likuwie
Ugumu kuongea unabaki unamung’unya tu na kutoa moshi mdomoni kama dragon
fake news ta Act imewatafuna wajinga wa buku saba na bado 2025 mtakuwa vichaa kabisa maana yule shetani wa kuwabeba hayupo mtagongwa mpaka maji muite mmaaa.
 
Hili ni jambo muhimu sana ambalo wana JF mnapaswa kulifahamu, kwamba ruzuku ya vyama vya siasa hutolewa kutokana na Kura za Jumla ambazo Chama kimepata kutoka kwenye Uchaguzi Mkuu husika.

Kwa mfano, Jumla ya Kura ambazo Chama kinapata kwenye Majimbo yote ndio zinazopigiwa mahesabu ya kujua hata idadi ya wabunge wa viti maalum watakaotokana na chama hicho na kiasi cha ruzuku ambayo chama hicho kitapewa.

Kwahiyo kumbe ule uzushi kwamba Wabunge wa viti maalum ndiyo wanaviletea vyama vya siasa ruzuku unazimwa kama Mshumaa kwenye kipupwe kikali.
Kwani hizo kura mlizipata ni lini mmezitambua?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unajitekenya afu unacheka mwenyewe

Sasa ndo mnakubali kuwa uchaguzi ulikuwa halali

Kumwamini mpinzani LAZIMA uwe chizi
Uchaguzi haukuwa halali ila you have to move on. Uchaguzi ulikua umeibwa haya wamekubali tume huru na Katiba mpya, mmepewa mikutano, mmefutiwa kesi, Sasa ulitaka Nini kifanyike ndio watu wa move on?
 
" wanachama wetu na wafuasi waliendelea kufanya kazi za chama bure kabisa bila malipo, na hii inaonesha kuwa Chama chetu ni chama cha watu."
Nimetumia hela zisizohesabika kwa ajili ya Chadema , sijui ni sh ngapi .
 
Uchaguzi haukuwa halali ila you have to move on. Uchaguzi ulikua umeibwa haya wamekubali tume huru na Katiba mpya, mmepewa mikutano, mmefutiwa kesi, Sasa ulitaka Nini kifanyike ndio watu wa move on?
Asante sana mkuu
 
SAWA.
Na hili la kutotambua na kushiriki katika mambo yatokanayo na uchaguzi haramu je? Au hayo yalikuwa ni matamshi ya kufurahisha watu tu?
Mkuu huwa nakuelewa sana , Lakini ni lazima utambue kwamba Chadema ni Taasisi ambayo ina utaratibu wake na hasa inavyo vikao vya maamuzi , chama kinapoingia kwenye maridhiano kuna vitu ni lazima kikubali kupoteza , kama vile ccm walivyokubali kupoteza baadhi ya mambo yao .

Kwahiyo kumbe huwezi kupata vyote unavyotaka kwa 100% , na huwezi kuingia kwenye maridhiano na misimamo ile ile , ni lazima mambo mengine ukubali kuyapoteza , bali ninachokijua ni kwamba COVID 19 wataondoka bungeni .

Na haya ambayo chama kinayaridhia huletwa kwenye vikao vya Kamati kuu na team ya Maridhiano , humo hujadiliwa na kura hupigwa miongoni mwa Wajumbe wa kanati kuu , wamo wanaopinga kwa hoja na wamo wanaokubali kwa hoja , mwisho wa siku wengi wanapewa na unakuwa msimamo wa Chama na wote tunasonga nao mbele , Jambo kubwa tuliloliangalia ni kwa ccm kukubali Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi ( Japo hapa tumesaidiwa na Wazungu ) , waliweka shinikizo ambalo limefanya ccm ilegee.

Yako mambo ambayo hata mimi nimeyapinga sana , lakini kwenye maridhiano huwezi kupata yote unayoyataka , na ili kuonekana mnaridhiana basi pande zote ni lazima zikubali kupoteza baadhi ya mambo yake .
 
Hii kazi unayofanya sasa inazidi kuwa ngumu sana, hasa kwa mtu kama wewe unayeamini chama kwa dhati kabisa.
Ushauri ninaoweza kukupa ili usiharibu hadhi yako kwa sasa, tena kwa haraka sana, ungejipa muda kidogo ili mambo yafumbuke zaidi huku ndani ya chama.
Haitachukua muda mwingi sasa, hapa tulipofikia sasa kwa hali halisi ya chama kujitokeza mbele kila mtu ajue kipo upande gani.
Hakuna nisichokijua na kwa kweli hata ya huko mbele nayajua kwa kiasi kikubwa japo hakuna lolote la kunitoa kwenye reli , yote ni mazuri sana kwa mstakabali wa chama na nchi , sina haja ya kujificha kisa maridhiano .
 
fake news ta Act imewatafuna wajinga wa buku saba na bado 2025 mtakuwa vichaa kabisa maana yule shetani wa kuwabeba hayupo mtagongwa mpaka maji muite mmaaa.
Nipo nimekaa pale hiyo 2025 mkifika na wafuasi wa kutosha niiteni bata bukini
 
Hili ni jambo muhimu sana ambalo wana JF mnapaswa kulifahamu, kwamba ruzuku ya vyama vya siasa hutolewa kutokana na Kura za Jumla ambazo Chama kimepata kutoka kwenye Uchaguzi Mkuu husika.

Kwa mfano, Jumla ya Kura ambazo Chama kinapata kwenye Majimbo yote ndio zinazopigiwa mahesabu ya kujua hata idadi ya wabunge wa viti maalum watakaotokana na chama hicho na kiasi cha ruzuku ambayo chama hicho kitapewa.

Kwahiyo kumbe ule uzushi kwamba Wabunge wa viti maalum ndiyo wanaviletea vyama vya siasa ruzuku unazimwa kama Mshumaa kwenye kipupwe kikali.
Naunga mkono ruzuku ichukuliwe. Huwezi kumsusia nguruwe shamba la mihogo. Utakula hasara mwenyewe.
 
Back
Top Bottom