Ujamaa ni mhimu
JF-Expert Member
- Sep 30, 2022
- 1,203
- 1,011
Hili ni jambo muhimu sana ambalo wana JF mnapaswa kulifahamu, kwamba ruzuku ya vyama vya siasa hutolewa kutokana na Kura za Jumla ambazo Chama kimepata kutoka kwenye Uchaguzi Mkuu husika.
Kwa mfano, Jumla ya Kura ambazo Chama kinapata kwenye Majimbo yote ndio zinazopigiwa mahesabu ya kujua hata idadi ya wabunge wa viti maalum watakaotokana na chama hicho na kiasi cha ruzuku ambayo chama hicho kitapewa.
Kwahiyo kumbe ule uzushi kwamba Wabunge wa viti maalum ndiyo wanaviletea vyama vya siasa ruzuku unazimwa kama Mshumaa kwenye kipupwe kikali
Hata nyiee mnajua fika kabisaa kwamba Kwa yule mwamba jpm hata asingepiga kampeni kugaragazwa kwenu kulikua pale paleee. Uchaguzi ulikua wa kweli na hakiii.