Ruzuku ya vyama vya siasa haitokani na Wabunge wa Viti Maalum


Hata nyiee mnajua fika kabisaa kwamba Kwa yule mwamba jpm hata asingepiga kampeni kugaragazwa kwenu kulikua pale paleee. Uchaguzi ulikua wa kweli na hakiii.
 
Hilo suala la Cdm kuchukua ruzuku linawapa stress za kujitakia kama kipindi kilichopita walisema hatuchukui na kwa sasa baada ya maridhiano ambayo nature yake ni nipe nikupe wakaamua kuchukua ww mtu baki unateseka ni kama wamechukua hela ya kulelea familia yako .Ni akili za wapi hizo hao CCM au Act wenyewe hawachukui ?Acheni gubu zenu msije pata pressure za kujitakia
 
‘Mkono mtupu aulambwi’ hiyo ndio CDM hakina Mdee walinunuliwa na ubunge wa vitu maalum; wakimbizi wamerudi kusikia mishahara inaanza kutoka tena.

Shibe mwanamalevya, njaa mwanamalegeza
 
Wabunge wa viti maalumu hupatikana kwa fomula hiyo hiyo.
Hapa upo unafanya nn hujaelewa jambo dogo, nikwamba huwezi kua diwani au MBunGE viti maalum kabla ya kukusanywa jumla ya kura za rais na wabunge nchi Zima ,elewa kwamba kabla ya hili tukio hakuna wabunge viti maalum , baada ya kurahizi kujulikana ndipo hupendekezwa majina ya watu wanaokidhi vigezo kuteuliwa kuwa wabunge viti maalum

Hivyo hawahusiki na mambo ya ruzuku na Kila kura Moja ruzuku yake ni 5000
 
Ruzuku inatokana na idadi ya kura za urais
 
Hii ni taarifa rasmi ya ofisi ya msajili wa vyama vya siasa ambaye ndiye mgawaji wa hiyo ruzuku.

https://www.orpp.go.tz/pages/subvention

NB:Baada ya "maridhiano" CDM inayatambua matokeo ya uchaguzi 2020 ni halali na uchaguzi ulikuwa wa huru na haki ndiyo maana imekubali ruzuku tofauti na msimamo wa awali.

Ama kweli mbwa ukimjua jina hakusumbui.
 
Kwahiyo uchaguzi ulikuwa halali na kura mlizipata ndio ilikuwa stahiki yenu na hiyo ruzuku ndio kiwango chenu

R,I.P CDM
 
N leo Mahakamani nini kimetokea tena ? Tufafanulie tuelewe vema
 
Maridhiano ya CCM na CDM hayana ridhaa ya wananchi.

Mnakubali kupeana RUZUKU wakati hapakuwa na uchaguzi!!

Wabunge wanasamehewa na kuendelea na matumizi ya V8?

Tupambanie KATIBA mpya Ili tuvinyooshe hivi vyama vya siasa vyenye kukandamiza wananchi wakiangalia Maslahi Yao.
 
Pesa kitu kibaya sana, inaweza kuwagombanisha baba na watoto.
 
Unajitekenya afu unacheka mwenyewe

Sasa ndo mnakubali kuwa uchaguzi ulikuwa halali

Kumwamini mpinzani LAZIMA uwe chizi
Inaonekana hata huelewi maana ya maridhiano.

Maridhiano ina maana pande zote zinazoridhiana zinakubaliana kuna mgogoro. Na hakuna namna ya wazi ya kumaliza mgogoro isipokuwa kwa kujadiliana na kisha kukubaliana kwa fomula mpya tofauti na iliyosababisha mgogoro.

Ni kweli uchaguzi wa 2020 ulikuwa batili. Rais alipora kura za wapinzani, wabunge walipora kura za wapinzani, madiwani walipora kura za wapinzani. Rais Samia, japo hakupigiwa kura lakini alipatikana kupitia kura alizokuwa amepora Rais.

Lakini Rais huyu wa sasa ni mwenye busara na mstaarabu ambaye amekubali kuwa 2020 kulikuwa na tatizo, sasa mtalitatuaje, ni lazima kuwa na maridhiano. Na maridhiano maana yake ni kuondoka kwenye misimamo ya awali.

Kwa upande wa upinzani, ni kukubali kuwa baada ya yule aliyedhulumu uchaguzi kutokuwepo, aliyepo ni Rais kwa mujibu wa katiba, ana mamlaka yote kikatiba. Na kwa upande wa Rais, naye kukubali kuwa wapinzani japo waliporwa na kunyang'anywa ushindi wao maeneo mengi.

Sasa mnatokaje hapo, kwa upinzani ni aheri kuchukua hiyo ruzuku ndogo ili isaidie kuandaa mazingira ya kuja kuurudisha ushindi ulioporwa.
 
Haya maswali yako naona yanajibika, tatizo naona kujibu naweza haribu mantiki ya mleta mada, hivyo kwangu ni vyema akajibu mwenyewe.
Najua kwa tabia zetu waTanzania, ni swali linalojibika kirahisi kwa vile hatuoni aibu tunapokiuka tuliyoahidi, hata katika mambo ya msingi kabisa.
Imekuwa ni tabia ya kipuuzi sana. Huwezi kumwamini mtu yeyote kwa akisemacho, hata awe ni padre kabisa kama Dr Mhogo, au Shekh wa Mkoa.
 
Kama kawaida yako, unapoamua kujibu kwa maelezo marefu unaeleweka bila ya shaka yoyote.

Ninakubaliana nawe kabisa kuhusu majadiliano na matarajio ya matokeo ya majadiliano.
Sina sabau ya kusema hapa kwamba huko ndani ya chama kuna watu wote wamepungukiwa wasione hatari wanayoingizwa, la hasha. Ninachoona hapa ni heshima kubwa sana inayopitiliza aliyopewa Mwenyekiti; na kwa bahati mbaya sana safari hii amekiingiza chama kwenye chaka ambalo hataweza kukitoa tena.

Baada ya yote haya, CHADEMA itabaki na nini cha kukisimamia kama chama? Au tukubali sasa kwamba CCM na CHADEMA hawana tena tofauti yoyote kati yao, na kwa maana hiyo CHADEMA imezwe na CCM, maana sioni uwezekano wa CCM kufa ili CHADEMA iendelee.

Chama chochote kina mambo yake makuu ya msingi, ambayo yanakitofautisha na kamwe hakiwezi kukiuka misingi hiyo bila kutetereka.

Hakuna anayepinga majadiliano hapa, na wala siasa siyo mambo ya kuwekeana uadui, lakini huwezi kutoka kwenye misingi unayosimamia eti kwa vile upo kwenye majadiliano.
Hayo majadiliano Samia hayaoni? Mbona anafanya mambo ambayo ni kama anavuruga juhudi za majadiliano kwa maksudi kabisa, kama kumteua Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi!

CHADEMA mmekubali kirahisi sana kuingizwa chakani, na hatma ya chama chenu ipo mashakani. Aliyoshindwa kuyafanya Magufuli, Samia kayamaliza kirahisi kabisa.
 
Hakuna nisichokijua na kwa kweli hata ya huko mbele nayajua kwa kiasi kikubwa japo hakuna lolote la kunitoa kwenye reli , yote ni mazuri sana kwa mstakabali wa chama na nchi , sina haja ya kujificha kisa maridhiano .
Nikurudishe kwenye mada yako nyingine ya hivi karibuni. Kwa CHADEMA hakuna Hichilema.
 
Swadakta
 
Muda utaongea
 
Muda utaongea
Nikwambie ukweli wangu wote mkuu, hakuna ninachokitamani kama kuiona CHADEMA ikiibuka na heshima zake zote baada ya hadaa zote hizi inazofanyiwa sasa hivi.

Kwa hiyo, ngoja tuone itakuwaje.
Lakini kuna hofu kubwa sana kwamba CHADEMA shanaswa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…