Walijaribu kuchokoza nyuki wakapokea Kibano kikali kule Mkoa wa pwani kusini wakakimbilia mozambique hawajarudi tena . Pale mpakani mwa Tanzania na Mozambique walijaribu mara moja walichokoza kwa kuvuka mpaka kwa kushitukizia na kuwasumbua kijiji cha mpakani wakarudi upesi Mozambique , mpaka leo hawajatamani kurudia tena kuwasumbua . Tofauti na Shabab kila kukicha wanaleta madhara kenya ambalo ni jambo la kusikitisha , mkenya akidhurika ni maumivu kwa afrika mashariki yote,vizuri mataifa ya africa yanatakiwa kuiga wazungu na kushirikiana kuondoa ugonjwa wa ugaidi.Hakuna mtu anayetamani vita, kwanza hatutaki kabisa, ila haimaanishi tukichokozwa ndio tukunje mikia, la sivyo wanajeshi watakua wa mapambo tu wa kuonyesha makucha siku za maadhimisho. Wanavijiji wenu walichinjwa kama mbuzi, leo utakuta waliosalia wanaishi kwa uwoga sana na misongo ya mawazo ila siku za maonyesho wanaona kwa TV wanajeshi wenu wanapita na magwaride yao.
Magaidi yakiizidi Msumbiji nguvu na kuteka taifa lote mjue hamtakua salama kwa uwoga wenu huo, mjue wale ni Wabantu walioaminishwa pumba za kidini, hivyo wana uwezo mkubwa sana kuhusisha vijana wenu na kusumbua kwenu ndani kwa ndani. Wanapaswa kukatwa mizizi mapema, tena waparamiwe na mataifa yote kwa pamoja, akigeuza huku kipodo, kule kipodo...yaani hakuna sehemu salama kwake.
Marekani ni super power Lakini anapenda kushirikiana