Mbona kama tunaongea lugha moja ila tunatofautiana kwenye uelewa wa hisabati na sayansi. Twende taratibu utaelewa:
NB: 1 GW ni sawa na 1,000 MW.
Wewe unasema hizo nuclear power plant (aka kinu) ndogo zinagharimu $ 1.0 billion sawa na TZS 2.5 trillion na zina uwezo wa kuzalisha 300 MW.
Mimi nimesema nuclear power plant ya size ya kawaida inauwezo wa kuzalisha 1,000 MW yaani mara tatu ya hizo ndogo za kwako. Hivyo na gharama yake itakuwa si zaidi ya mara tatu ya hizo ndogo ie $ 3.0 sawa na TZS 7.0 trillion
Bwawa la umeme la Nyerere lina uwezo wa kutoa 2,115 MW sawa na 2.1 GW na limetugharimu $ 2.9 billion sawa na TZS 7.0 trillion. Maana yake ni kuwa umeme wa kiasi cha JNHPP ungaliweza kuzalishwa na vinu viwili vya size ya kawaida kwa bei, kwa calculation zako, ya $ 6.0 billion sawa na TZS 15.0 trillion.
Bado bei hii si mbaya kwani hizo nuclear power plant hazina changamoto ya kuishiwa hiyo uranium iliyomo kwenye hivyo vinu. Half life ya uranium ni 4.5 billion years. Kinachotokea ndani ya hivyo vinu ni kugongana kwa neutrons na atoms za uranium. Mgongano huo unaitwa fission na hutoa joto la kuzalisha mvuke (steam) ambao ndiyo huzungusha turbine generator ya kutoa umeme. Hakuna kinachopotea au kuungua ndani ya humo kwenye nuclear power plants. Changamoto ya umeme wa maji ni kamq ambavyo tunashuhudia kwa mabwawa kuishiwa maji wakati wa kiangazi au ukame.
Usimikaji wa hivyo vinu vya nuclear power plant ni rahisi kuliko ule wa kutengeneza mabwawa kama hilo la JNHPP. Gharama kubwa huwa ni uranium ya high grade (aka weapon grade) ambayo bei yake maradufu ya bei ya dhahabu. Bei ya kilo moja ya hii uranium - isotope 238 ni $ 100,000 kwa kilo moja. Ninachosema ni kuwa sisi Tanzania tunayo kwa wingi hii uranium, hivyo usimikaji wa nuclear power plant hapa kwetu utakuwa rahisi sana, ni chini ya nusu ya ile uliyo kokotoa hapo juu. Assuming of course kwamba hakutakuwa na ufisadi au mikataba mbovu katika muradi huo. Uranium hii ilishaanza kuwa extracted na kampuni ya Urusi (state owned) tangia mwaka 2013 baada ya kununua kutoka kampuni binafsi ya Fredrick Kibodya et al waliokuwa wanamiliki uranium deposits zilizomo mto Mkuju huko Namtumbo. Kampuni hiyo ya Kibodya et al ilijulikana kwa jina la Mantra Tanzania Limited. Kampuni ya serikali ya Russia iliyonunua deposits hizo inaitwa Rosatom, ni 100% owned by the state of Russia na inauzoefu wa zaidi ya miaka 70 kwenye shughuli ya ku extract uranium and plutonium.
Usimikaji wa hivi vinu vya nuclear power plant 2huchukua muda mfupi, ndani ya miezi sita, siyo kama ule wa ujenzi wa mabwawa ya umeme. Ndiyo maana unaweza kununua hata ka kinu kadogo ka matumizi yako binafsi kenye kilo moja tu ya uranium- 238 ambako katakuzalishi muda wote 24,000,000 units (kWh) za umeme. Kilo moja ya mineral oil (gasoline) au gesi inatoa 12 units baada ya kuungua, kilo moja ya makaa ya mawe inatoa 8 units tu za umeme baada ya kuungua. Nuclear power generators do not burn fuel just like hydo power generators.
Nadhani sasa tunazungumza lugha moja ya kisayansi na siyo ile ya wana si hasa.
Mantra Tanzania Limited – a subsidiary of Uranium One Holdings and which owns the Mkuju River Project at Namtumbo in Ruvuma Region – is deploying the latest technology as it plans to start mining...
www.thecitizen.co.tz