Dr Akili
JF-Expert Member
- Aug 21, 2011
- 5,119
- 4,569
- Thread starter
- #41
Hicho unachokiita mabaki ya nyukilia bila shaka unamaanisha radioactive waste. Hizi hazikwepeki kwa ulimwengu wa sasa wa tekinolojia. Zinazalishwa maeneo mbali mbali hususani kwenye hospitali zetu ambavyo vina vitengo vya nuclear medine. Zinazalishwa kwenye vitengo na taasisi mbalimbali za utafiti hususani za kilimo na kadhalika. Hivyo hata hapa Tanzania tunazalisha sana tu hizi radioactive wastes.Hivi mabaki ya nyukilia si yana athari zake na namna ya kuhifadhi na utupwaji wake. Ambayo hutupwa huku afrika Kwa kulipwa na mataifa Makubwa , Kwa baadhi yetu kupewa chenji kidogo
Radioactive wastes hizi zinazibitiwa kitekinolojia kwa miongozo na usimamizi wa International Atomic Agency ambalo hapa kwetu linawakilishwa na Tanzania Atomic Agency yenye makao makuu huko Arusha.
Pia ikumbukwe kuwa uzalishaji wa radioactive wastes katika mitambo hii ya nuclear power plants si mkubwa. Eneo la ardhi linalokaliwa na mitambo ya nuclear power plant yenye uwezo wa kuzalisha umeme wa GW 1.0 ni square mile moja tu (2.6 square km). Kuweza kuzalisha umeme wa GW 1.0 kwa kutumia upepo, eneo la ardhi litakalotumika ni mara 360 sawa na 936 square km, kwa umeme wa jua ni mara 75 sawa na 195 square km. Eneo la bwawa la umeme la Nyerere lina ukubwa wa 1,200 square km. Haya ni maeneo makubwa sana ya ardhi sawa na wilaya tatu au zaidi. Hivyo madhara yake kwa mazingira ni kubwa sana kuliko yale ya umeme wa nyukia. Kumbuka mabilioni ya miti iliyokatwa na matrillion ya uoto/ majani (fauna) ulioangamizwa ili kupata hilo bwawa la Nyerere.
View: https://youtu.be/3QXSkXHDZgU?si=Rz4n_KwkoUlnFOYg