Wewe unatakiwa utulize akili yako kwani inaonekana umetawaliwa na ushabiki (fanatism) badala ya rational.
Huyo jamaa mada yake inasema ; "kwanini nchi za KIAFRIKA haziendelei, ikiwemo Tz, licha ya kupewa misaada??",--- sasa kwani kenya sio nchi ya kiafrika kiasi kwamba usiingize katika kundi la nchi zisizokuwa na maendeleo licha ya kupewa misaada??!, au Kenya haipewi misaada??
Umeshupalia juu ya Albino, sasa nikuulize; je hilo sakata la Albino lilianza lini??, na kabla halijaanza ni uchumi upi kati ya Tz na Kenya ulikuwa mkubwa??, je, hivi sasa Sakata hilo la Albino bado lipo??, je hivi sasa baada ya sakata hilo ni uchumi upi mkubwa kati ya Tz na Kenya??.
Ninachotaka kukufundisha ni hiki kwamba maendeleo ya kiuchumi katika Tz hayahusiani na sakata la kinyama la mauaji ya Albino kwani jambo hilo lilikuwa ni jambo la kihalifu lisilohusiana kabisa na maendeleo ya uchumi na jambo hilo lilianza na limeshatokomezwa miaka kadhaa iliyopita, ninashangaa umeendelea kulishikilia bila mantiki yoyote isipokuwa ushabiki tu.
(1)---Mimi nimekupa somo lenye mantiki kwamba; Maendeleo ya kiuchumi ya nchi ni lazima yanufaishe umma (wananchi), kama nchi itakuwa na uchumi mkubwa lakini uchumi huo kwa namna yoyote ukashindwa kutumiwa kusaidia kustawisha umma basi uchumi huo ni useless, uchumi unajengwa na umma, serikali inaendesha uchumi kwa ajili ya kuletea umma maendeleo nk,.
(2)----Tunajua na kutambua kuwa Kenya ni nchi yenye uchumi mkubwa EA, lakini inasikitisha na kuhuzunisha tunapona ndugu zetu Wakenya wanakufa kwa njaa kila mwaka licha ya uchumi wa nchi yao kuwa mkubwa!!!, je serikali unashindwa kutenga bajeti kila mwaka kukabiliana na janga la njaa??!! au hao wanaokufa sio watu??!, au ni watu wa tabaka la chini??, au ndio tribalism in action ??!, semeni tujue!!, ---kumbuka hakuna hitaji la muhimu kuliko yote katika maisha ya binadamu kama chakula, sasa tunashangaa iweje Uchumi mkubwa usiweze kuzibiti njaa??!!, huku Tz tunahadithiwa, baada ya vita vya kagera (Tz vs Uganda) uchumi wa Tz uliporomoka vibaya sana, bidhaa muhimu zote kupatikana ilikuwa ni shida kubwa lakini Nyerere alihakikisha hakuna Mtz atakaye kufa njaa zama hizo na ndipo mahindi ya njano (Yanga) kutoka marekani yakaingia na kwa kiasi kikubwa yalisaidia sana kukabiliana na tatizo la njaa lililokuwa linatunyemelea, Nyerere alichukua hatua hizo kama kiongozi mwenye dhamira na dhamana ya kulinda uhai wa watu wake, sasa kulikoni ndugu zetu wakenya??!!---3.5 million people kila mwaka (routinely) hukumbwa na njaa na matokeo yake ni utapiamlo nk, licha ya Uchumi wenu mkubwa huku wakati huo huo mkijisifia kurusha satellite, kujenga flyovers, SGR kwa gharama kubwa nk!!,
(3)---Kama Tz imeweza kukabiliana na mauaji ya kinyama ya Albino na kuyatokomeza kabisa, mauaji dhidi ya ubinadamu, basi nimatumaini yetu Kenya nayo kila mwaka itakuwa ikiweka initiatives za kukabiliana na baa la njaa (njaa ni janga dhidi ya ubinadmu), for good ili jambo hilo liwe ni historia kwa vizazi vijavyo sio vya Kenya tu baki vya wana E Africans kwa ujumla na hapo ndipo locals and internationals media HEADLINES za aina hii zitakoma👇🏻
View attachment 2295828