Tetesi: Rwanda nyuma ya kufukuzwa Shyrose!

Tetesi: Rwanda nyuma ya kufukuzwa Shyrose!

Kwani anamkataba wa kudumu kuwa mgombea/mbunge?

Aende akajiajiri aache kulia lia
 
Huo ni uzushi tu
hatutaweza kukubaliana katika hili kwa kuwa vikao hivi huwa havina taarifa za wazi ambazo ni rasmi. Tufanye hivi ili tufunge mjadala. Naomba kuuliza swali personal kidogo.
Unaamini au huamini taarifa kuwa majina ya wagombea top 5 wa CCM yaliletwa mfukoni? Najua hakuna relation lakini ukijibu hili utakuwa pia umemaliza na swali la kama Shyrose amekatwa kwa kutumia process halali.
 
....hiyo line huwa mnaipenda kweli ya kuwa mlisoma threads zangu kabla hamjajiunga. Sijui ni watu wangapi huwa mnawasoma na kuwakariri kabla hamjajiunga. So for 7 years unamsoma jmali ila ukajiunga 2015! Okay.
Nikuambie kuwa sisomi threads zako tu
michango yako sana
kuna hawa watu murutongore ,mchambawima1 nawengineo
mlikuwa mkibishana sana kuhusu Interahamwe
elewa hivyo
wewe unachuki na serikali ya Rwanda sana
huna jema kutoka kwa Pk
 
Natamani wanaosoma namba waongezeke mara 100 zaidi ya sasa, ili 2020 wapiga debe upande wa pili tuwe wengi
 
hatutaweza kukubaliana katika hili kwa kuwa vikao hivi huwa havina taarifa za wazi ambazo ni rasmi. Tufanye hivi ili tufunge mjadala. Naomba kuuliza swali personal kidogo.
Unaamini au huamini taarifa kuwa majina ya wagombea top 5 wa CCM yaliletwa mfukoni? Najua hakuna relation lakini ukijibu hili utakuwa pia umemaliza na swali la kama Shyrose amekatwa kwa kutumia process halali.
Huo pia ni uzushi. Amini taarifa rasmi tu, utaumiza kichwa chako kwa habari za kizushi.
 
Hakuna haja ya kudhanidhani, Shyrose amemaliza muda wake na apumzike. Siasa ni zamu kwa zamu. Na kila zama ina watu wake
Petro mselewa nimesoma ulichokiandika sasa tujiulize kwani lazima yeye tu ndio awe mbunge? Pili hivi kila anayekatwa kwenye chama lazima a it we kujieleza kwanini asikatwe? Chadema, ACT, na CUF wamefanya hiyo michakato swali ni je walioomba wote kwenye teuzi za kivyama ndio waliopata na kama hawakupata wote je wakati chama kinawakata kwenye mchakato huo wale waliokosa wameitwa kuhojiwa ? Je maelezo ya sababu zako za Rwanda na ndoa yana ithibati yoyote au unahisi tu ndugu yangu MOO PALMO? Wewe ni mwanasheria mbobevu tena mwenye uwezo hasaa sasa kale "kaprinciple no evidence no right to speak " naomba kaaply kwako mdogo wangu.
 
Hilo ndio swali. lakini huyu alikuwa haanzi mwanzo alikuwa anatetea kiti chake kama makongoro na kimbisa. Hivi inawezekana Magufuli kukatwa jina ndani ya CCM 2020? Term limit ya EALA ni miaka 10.
Team limit ni 5 years renewable sasa kashamaliza miaka yake
 
Petro mselewa nimesoma ulichokiandika sasa tujiulize kwani lazima yeye tu ndio awe mbunge? Pili hivi kila anayekatwa kwenye chama lazima a it we kujieleza kwanini asikatwe? Chadema, ACT, na CUF wamefanya hiyo michakato swali ni je walioomba wote kwenye teuzi za kivyama ndio waliopata na kama hawakupata wote je wakati chama kinawakata kwenye mchakato huo wale waliokosa wameitwa kuhojiwa ? Je maelezo ya sababu zako za Rwanda na ndoa yana ithibati yoyote au unahisi tu ndugu yangu MOO PALMO? Wewe ni mwanasheria mbobevu tena mwenye uwezo hasaa sasa kale "kaprinciple no evidence no right to speak " naomba kaaply kwako mdogo wangu.
Classmate wangu Kiba mzaire, kwanza nakusalimu. Pili, nashukuru kwa kukubaliana kuwa Shyrose akubali kilichotokea na afanye mambo mengine. Wa kuwa Mbunge wa Afrika Mashariki si yeye tu. Na afahamu pia kuwa kila chama cha siasa kina 'udikteta' katika kuamua kwa kulinda maslahi yake. Hakuna pasipo na ubabe hasa katika kuamua. Ajifunze kukubali matokeo na kujipanga upya. Hapo anaharibu zaidi. Jumong hapa!
 
Kikao kina maana yake, haya ni maamuzi ya mwenyekiti yaliyovaa koti la kikao.
Lakini mwenyekiti ndio kiongozi wa kikao
Sasa kama wajumbe mwisho walikunaliana na mwenyekiti
Labda kama useme wajumbe walishinikizwa na mwenyekiti kukubaliana naye
Kama hivyo ndivyo basi kuna mapungufu mahala
 
Shyrose ndio aliyezima jaribio la Rwanda kutumia bunge la EAC kwa maslahi ya utawala wao wa kidikteta, ikiwemo kuongoza wabunge kupinga kupinduliwa kwa spika aliyekataa hoja ya Rwanda kutengeneza historia batili ya genocide ambayo ingekuwa endorsed na bunge hilo. Shyrose pia alikuwa mstari wa mbele kupinga ardhi yetu kuwa ya cha wote ndani ya EAC, kinyume na matakwa ya Rwanda. Hilo ndio kosa lake.

Bahati mbaya mkuu wa sasa ni "rafiki" (mwenzao?) wa utawala wa kidikteta wa Rwanda, hili liko wazi. Sera yetu juu ya Rwanda kisiasa tuliyokuwa nayo toka tuwasuluhishe 1994 imepinduliwa chini juu! Hii ndio sababu haijawahi kutokea mtu anakatwa jina na mwenyekiti kimabavu bila kikao kuelezwa chochote kile!

Kashfa hizi zinazorudiwa rudiwa kuhusu ulevi na kupigana etc, zilishathibitika kuwa ni fitna za vyombo vya habari vya serikali ya Rwanda humu humu JF kitambo sana. (threads ziko chini). Jamani, bunge la EAC linaendeshwa kwa sheria, mbunge akikosea anafukuzwa kama ilivyo bunge lingine. Ukweli ni kuwa baada ya vyombo vya serikali ya Rwanda kueneza propaganda juu ya Shyrose, HAKUNA SHITAKA HATA MOJA ambalo shyrose alipewa kutokana na huo uzushi wa Rwanda! Na mtu akifanya fujo kwenye ndege pia hukamatwa immediately akitua huko anakokwenda. Vyombo pekee vya habari vilivyoandika habari hizi ni vya serikali ya Rwanda!
In fact SERIKALI YETU WENYEWE pia ilisimama kifua mbele kwa kumtetea shyrose! (thread hapa: Serikali: Shy-Rose hakupigana Kenya), leo hii mkuu wa serikali anamkata Shyrose kwa tuhuma zipi tena?

Shyrose so far ndio mbunge mwenye mchango mkubwa EAC kuliko wengine, lets be objective hapa, ni mchango gani wabunge wengine wote wa TZ wametoa bungeni EAC kumzidi shyrose? Kwa nini hoja isiwe kiwango cha kazi yake na badala yake tunajikita kwenye mfumo dume kuhoji masuala ya ndoa yake? Huu ni unafiki just because she is a woman!

Hatari tuliyonayo sasa ni kuendeshwa na Rwanda. Hii ndio system yao duniani kote, unapoingia utawala rafiki na wao, wale maadui zao wote wa zamani huwa "wanasomeshwa" namba kama anavyofanyiwa Shyrose. Msishangae kashfa mbalimbali zikaanza kuibuka dhidi ya Membe, Kikwete, Kamanda kibolwa na wengineo wote.

Na tusishangae sasa tukaanza endorsement ya historia ya genocide according to Kagame, ingawa nchi yetu ilikuwapo na ilishuhudia what happened, tayari amri za ma DC kuwatoa wafugaji haramu maporini kule Kagera, zinatenguliwa na "ngazi za juu" kwa upuuzi eti "hatuna pa kuwaweka wanyama"! Sasa tusishangae serikali yetu ikiridhia kuwa ardhi yetu ni iwe ni free for all kwa EAC wote n.k
Kwa tunaoelewa geopolitics, shyrose will always be a heroine!

Past theads:
1. Shy-Rose Bhanji Ajitetea
2. Sakata la Shyrose Bhanji na agenda ya Wanyarwanda kumng'oa Spika wa Bunge la Afrika Mashariki
3. Aibu: Shyrose Bhanji azua tafrani ziara ya EALA
upuuzi tu unaandika. nenda ukalewe huko na shyrazi wako, nonsense.
 
Back
Top Bottom