Tetesi: Rwanda nyuma ya kufukuzwa Shyrose!

Tetesi: Rwanda nyuma ya kufukuzwa Shyrose!

Y
Shyrose ndio aliyezima jaribio la Rwanda kutumia bunge la EAC kwa maslahi ya utawala wao wa kidikteta, ikiwemo kuongoza wabunge kupinga kupinduliwa kwa spika aliyekataa hoja ya Rwanda kutengeneza historia batili ya genocide ambayo ingekuwa endorsed na bunge hilo. Shyrose pia alikuwa mstari wa mbele kupinga ardhi yetu kuwa ya cha wote ndani ya EAC, kinyume na matakwa ya Rwanda. Hilo ndio kosa lake.

Bahati mbaya mkuu wa sasa ni "rafiki" (mwenzao?) wa utawala wa kidikteta wa Rwanda, hili liko wazi. Sera yetu juu ya Rwanda kisiasa tuliyokuwa nayo toka tuwasuluhishe 1994 imepinduliwa chini juu! Hii ndio sababu haijawahi kutokea mtu anakatwa jina na mwenyekiti kimabavu bila kikao kuelezwa chochote kile!

Kashfa hizi zinazorudiwa rudiwa kuhusu ulevi na kupigana etc, zilishathibitika kuwa ni fitna za vyombo vya habari vya serikali ya Rwanda humu humu JF kitambo sana. (threads ziko chini). Jamani, bunge la EAC linaendeshwa kwa sheria, mbunge akikosea anafukuzwa kama ilivyo bunge lingine. Ukweli ni kuwa baada ya vyombo vya serikali ya Rwanda kueneza propaganda juu ya Shyrose, HAKUNA SHITAKA HATA MOJA ambalo shyrose alipewa kutokana na huo uzushi wa Rwanda! Na mtu akifanya fujo kwenye ndege pia hukamatwa immediately akitua huko anakokwenda. Vyombo pekee vya habari vilivyoandika habari hizi ni vya serikali ya Rwanda!
In fact SERIKALI YETU WENYEWE pia ilisimama kifua mbele kwa kumtetea shyrose! (thread hapa: Serikali: Shy-Rose hakupigana Kenya), leo hii mkuu wa serikali anamkata Shyrose kwa tuhuma zipi tena?

Shyrose so far ndio mbunge mwenye mchango mkubwa EAC kuliko wengine, lets be objective hapa, ni mchango gani wabunge wengine wote wa TZ wametoa bungeni EAC kumzidi shyrose? Kwa nini hoja isiwe kiwango cha kazi yake na badala yake tunajikita kwenye mfumo dume kuhoji masuala ya ndoa yake? Huu ni unafiki just because she is a woman!

Hatari tuliyonayo sasa ni kuendeshwa na Rwanda. Hii ndio system yao duniani kote, unapoingia utawala rafiki na wao, wale maadui zao wote wa zamani huwa "wanasomeshwa" namba kama anavyofanyiwa Shyrose. Msishangae kashfa mbalimbali zikaanza kuibuka dhidi ya Membe, Kikwete, Kamanda kibolwa na wengineo wote.

Na tusishangae sasa tukaanza endorsement ya historia ya genocide according to Kagame, ingawa nchi yetu ilikuwapo na ilishuhudia what happened, tayari amri za ma DC kuwatoa wafugaji haramu maporini kule Kagera, zinatenguliwa na "ngazi za juu" kwa upuuzi eti "hatuna pa kuwaweka wanyama"! Sasa tusishangae serikali yetu ikiridhia kuwa ardhi yetu ni iwe ni free for all kwa EAC wote n.k
Kwa tunaoelewa geopolitics, shyrose will always be a heroine!

Past theads:
1. Shy-Rose Bhanji Ajitetea
2. Sakata la Shyrose Bhanji na agenda ya Wanyarwanda kumng'oa Spika wa Bunge la Afrika Mashariki
3. Aibu: Shyrose Bhanji azua tafrani ziara ya EALA
Thread za mihemuko hizi, umeitaja Rwanda zaidi ya Mara 6, sasa Rwanda inaingiaje uteuzi wa ccm kweli, na hoja zako hazieleweki moja umesema ni kwa sababu ya Rwanda, pili ukasema kakosa kwasababu ni mwanamke!? which is which sasa. ubinafsi tu ndo umekujaa, eti usishangae ardhi yetu ikawa ya wote! hoja yako hasa ni nini? ila sentensi yako ya mwisho inakutambulisha wewe ni nani"Shyrose will always be a heroine!!!!!)
 
Nikuambie kuwa sisomi threads zako tu
michango yako sana
kuna hawa watu murutongore ,mchambawima1 nawengineo
mlikuwa mkibishana sana kuhusu Interahamwe
elewa hivyo
wewe unachuki na serikali ya Rwanda sana
huna jema kutoka kwa Pk
hahahaha sawa mkuu, kuwa mchambawima1 na muturongore, possibly koba na mukamasimba huwa wana hoja zinazokushawishi zaidi ya zangu. Ni vizuri.
 
Lakini mwenyekiti ndio kiongozi wa kikao
Sasa kama wajumbe mwisho walikunaliana na mwenyekiti
Labda kama useme wajumbe walishinikizwa na mwenyekiti kukubaliana naye
Kama hivyo ndivyo basi kuna mapungufu mahala
nakubali kuwa officially ni maamuzi ya kikao. Lakini maamuzi yanayoitwa official hayawezi kuleta maswali. Mfano: hautauliza swali endapo Magufuli atachujwa awamu ya kwanza kabisa 2020 wakati yeye tayari ni rais?
 
Ni vema kuandika ukijuacho sio bora kuandika Tanzania hasa CCM kuna utaratibu wa kupata wagombea Shy rose kafanya kazi yake sasa basi.
Rwanda ni nchi huru katika EAC TUNASHIRIKIANA VEMA MAENDELEO YAO ANGALIA DATA HAYANA MFANO USAFI,USALAMA,ELIMU LAPTOP KWA KILA MTOTO,MATIBABU BURE,HAKUNA NYUMBA ZA NYASI,NG'OMBE KILA FAMILIIA we baki maneno tu
 
May God bless you!
same to you, sijui hawa chadema ilikuwaje wakamchukua mtu ambaye taarifa rasmi za CCM zilidai kuwa alichujwa kwa sababu hakuwa na maadili...ngoja niwaulize wenyewe....thank you though.🙂
 
Ni vema kuandika ukijuacho sio bora kuandika Tanzania hasa CCM kuna utaratibu wa kupata wagombea Shy rose kafanya kazi yake sasa basi.
Rwanda ni nchi huru katika EAC TUNASHIRIKIANA VEMA MAENDELEO YAO ANGALIA DATA HAYANA MFANO USAFI,USALAMA,ELIMU LAPTOP KWA KILA MTOTO,MATIBABU BURE,HAKUNA NYUMBA ZA NYASI,NG'OMBE KILA FAMILIIA we baki maneno tu
...halafu ni wahamiaji haramu Tanzania ambako hakuna maendeleo! Na hakuna mhamiaji haramu wa Tanzania anayeganga njaa Rwanda. Okay bwana acha nibaki na maneno yangu.
 
Y
Thread za mihemuko hizi, umeitaja Rwanda zaidi ya Mara 6, sasa Rwanda inaingiaje uteuzi wa ccm kweli, na hoja zako hazieleweki moja umesema ni kwa sababu ya Rwanda, pili ukasema kakosa kwasababu ni mwanamke!? which is which sasa. ubinafsi tu ndo umekujaa, eti usishangae ardhi yetu ikawa ya wote! hoja yako hasa ni nini? ila sentensi yako ya mwisho inakutambulisha wewe ni nani"Shyrose will always be a heroine!!!!!)
Kama umeisoma thread bila mhemuko halafu hujaielewa basi hilo sio tatizo langu.
 
Mbona kama wengine my wagumu kuelewa? tatizo ni aina ya njia iliyotumika kumwondosha.mkulu kutoruhusu maswali!
 
hahahaha sawa mkuu, kuwa mchambawima1 na muturongore, possibly koba na mukamasimba huwa wana hoja zinazokusha wishi zaidi ya zangu. Ni vizuri.
Hapana najua hujanielewa
namaanisha kuwa Nakufuatilia kitambo sana
tena sina maana nakuchukia au la
tena huwa napenda sana michango yako ya hoja
lakini nimekuambia wewe unachuki na serikali ya Rwanda huo ndio ukweli
 
dada (?🙄) mbona unaniamulia? Nimeshasema nimekuelewa. Unapenda michango yangu ya hoja halafu unaconclude kwamba naichukia Rwanda. Asante.
 
Hapana najua hujanielewa
namaanisha kuwa Nakufuatilia kitambo sana
tena sina maana nakuchukia au la
tena huwa napenda sana michango yako ya hoja
lakini nimekuambia wewe unachuki na serikali ya Rwanda huo ndio ukweli
Umenena vema.
 
Mbona kama wengine my wagumu kuelewa? tatizo ni aina ya njia iliyotumika kumwondosha.mkulu kutoruhusu maswali!
Tatizo ni kuwa linapokuja suala la demokrasia ndani ya vyama, hakuna tofauti kati ya CCM na vyama vya upinzani. Wenyeviti wao nao hubaka demokrasia kwa kuwa na majina yao mifukoni, kukata watu wasiowapenda bila kufuata utaratibu n.k, kwa vigezo wanavyovijua wao mfano "kuepusha kukigawa chama" etc.
Kwa hiyo hapa inakuwa ngumu kumpinga magu katika hili kwa kuwa hata kwenye chaguzi zao wenyeviti wao hufanya hivyo hivyo.
Ingekuwa ni figisu zao za CCM nisingeandika hii thread, ila kinachosikitisha hapa ni kuwa huyu ni shujaa aliyetetea nchi yetu kutoburuzwa na Rwanda EAC, anafanyiwa hivi kwa sababu ya "urafiki" wa nchi nyingine.
 
....sasa na mimi nasema kakatwa sababu anajiita Rais wa Mbweni wakati Rais ni mmoja tu;
...kwani alipochaguliwa mwanzo si kwa mbeleko?
.akafanye ishu nyingine,hiyo ndo siasa!
 
Back
Top Bottom