roboka kafwekamo
JF-Expert Member
- Mar 12, 2017
- 821
- 451
Nilisema ile hija ilikuwa ya mapema mno kwa mr presdent sasa kagsndsmizia yote ya kagame twafwa.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yatakuwa ni mambo ya Zero GrazingMie nadhani Shy-rose kuna kitu kasahau kule EALA, si kwa kulia-lia huko.
Shyrose ndio aliyezima jaribio la Rwanda kutumia bunge la EAC kwa maslahi ya utawala wao wa kidikteta, ikiwemo kuongoza wabunge kupinga kupinduliwa kwa spika aliyekataa hoja ya Rwanda kutengeneza historia batili ya genocide ambayo ingekuwa endorsed na bunge hilo. Shyrose pia alikuwa mstari wa mbele kupinga ardhi yetu kuwa ya cha wote ndani ya EAC, kinyume na matakwa ya Rwanda. Hilo ndio kosa lake.
Bahati mbaya mkuu wa sasa ni "rafiki" (mwenzao?) wa utawala wa kidikteta wa Rwanda, hili liko wazi. Sera yetu juu ya Rwanda kisiasa tuliyokuwa nayo toka tuwasuluhishe 1994 imepinduliwa chini juu! Hii ndio sababu haijawahi kutokea mtu anakatwa jina na mwenyekiti kimabavu bila kikao kuelezwa chochote kile!
Kashfa hizi zinazorudiwa rudiwa kuhusu ulevi na kupigana etc, zilishathibitika kuwa ni fitna za vyombo vya habari vya serikali ya Rwanda humu humu JF kitambo sana. (threads ziko chini). Jamani, bunge la EAC linaendeshwa kwa sheria, mbunge akikosea anafukuzwa kama ilivyo bunge lingine. Ukweli ni kuwa baada ya vyombo vya serikali ya Rwanda kueneza propaganda juu ya Shyrose, HAKUNA SHITAKA HATA MOJA ambalo shyrose alipewa kutokana na huo uzushi wa Rwanda! Na mtu akifanya fujo kwenye ndege pia hukamatwa immediately akitua huko anakokwenda. Vyombo pekee vya habari vilivyoandika habari hizi ni vya serikali ya Rwanda!
In fact SERIKALI YETU WENYEWE pia ilisimama kifua mbele kwa kumtetea shyrose! (thread hapa: Serikali: Shy-Rose hakupigana Kenya), leo hii mkuu wa serikali anamkata Shyrose kwa tuhuma zipi tena?
Shyrose so far ndio mbunge mwenye mchango mkubwa EAC kuliko wengine, lets be objective hapa, ni mchango gani wabunge wengine wote wa TZ wametoa bungeni EAC kumzidi shyrose? Kwa nini hoja isiwe kiwango cha kazi yake na badala yake tunajikita kwenye mfumo dume kuhoji masuala ya ndoa yake? Huu ni unafiki just because she is a woman!
Hatari tuliyonayo sasa ni kuendeshwa na Rwanda. Hii ndio system yao duniani kote, unapoingia utawala rafiki na wao, wale maadui zao wote wa zamani huwa "wanasomeshwa" namba kama anavyofanyiwa Shyrose. Msishangae kashfa mbalimbali zikaanza kuibuka dhidi ya Membe, Kikwete, Kamanda kibolwa na wengineo wote.
Na tusishangae sasa tukaanza endorsement ya historia ya genocide according to Kagame, ingawa nchi yetu ilikuwapo na ilishuhudia what happened, tayari amri za ma DC kuwatoa wafugaji haramu maporini kule Kagera, zinatenguliwa na "ngazi za juu" kwa upuuzi eti "hatuna pa kuwaweka wanyama"! Sasa tusishangae serikali yetu ikiridhia kuwa ardhi yetu ni iwe ni free for all kwa EAC wote n.k
Kwa tunaoelewa geopolitics, shyrose will always be a heroine!
Kwenye red sijaelewa mimi.
Past theads:
1. Shy-Rose Bhanji Ajitetea
2. Sakata la Shyrose Bhanji na agenda ya Wanyarwanda kumng'oa Spika wa Bunge la Afrika Mashariki
3. Aibu: Shyrose Bhanji azua tafrani ziara ya EALA
alichaguliwa kwa kura nyingi mwanzo na hata sasa alichaguliwa kwa kura nyingi vile vile. Nyie mnaomshambulia bila sababu ndio mnaji expose.....sasa na mimi nasema kakatwa sababu anajiita Rais wa Mbweni wakati Rais ni mmoja tu;
...kwani alipochaguliwa mwanzo si kwa mbeleko?
.akafanye ishu nyingine,hiyo ndo siasa!
tukiacha ya Shyrose there is a bunch of points from thereHakuna haja ya kudhanidhani, Shyrose amemaliza muda wake na apumzike. Siasa ni zamu kwa zamu. Na kila zama ina watu wake
...narudia,alichaguliwa mwanzo kwa mbeleko;na wapo waliolialia,alichaguliwa kwa kura nyingi mwanzo na hata sasa alichaguliwa kwa kura nyingi vile vile. Nyie mnaomshambulia bila sababu ndio mnaji expose.
Mkuu wangu nipo!Mkuu upo? Umerudi tu na kuanza na Lowasa? Kwani Mizengo K. Pinda hawezi kumpa jibu?
Nadhani hii inaleta shida sababu yeye alikua bado anagombea nafasi..its like mkulu akatwe kichwa 2020!..utavyolia mkuu!!Watu waliojitokeza kuomba ubunge ni zaidi ya 400 halafu mtu mmoja anadhani ni haki yake pekee kuwa mbunge.
Uongozi ni kupokezana vijiti. Muda wa uongozi wake ndani ya bunge la EAC umefika kikomo kwa tiketi ya CCM. Kulia lia hakusaidii chochote. Just shake the dust and move on!
Unadai hakuna mtu aliyekatwa jina kwenye vikao vya CCM bila kutolewa maelezo. Are you kidding me? Kamuulize Edward Lowassa atakupa jibu sahihi.
Mkuu;Nadhani hii inaleta shida sababu yeye alikua bado anagombea nafasi..its like mkulu akatwe kichwa 2020!..utavyolia mkuu!!
Hoja sio yeye kukatwa hoja ni kukatwa bila kuzingatia utaratibu. Kwa namna ambavyo imefanyika mchakato mzima hauna maana kwani mwenyekiti anaweza kuamua nani akatwe na sio kikao.Mkuu;
Ningeelewa angalau kidogo kama angekuwa bado ni Mbunge wakati jina lake linakatwa. Kisheria na kikanuni kwa sasa siyo Mbunge tena kwa sababu kipindi chake kimefikia kikomo ndio maana kuna mchakato mwingine wa kuteuwa wagombea ubunge.
Kama hii ndio hoja yake basi kulikuwa hakuna umuhimu wowote wa kufanya mchakato mpya kutafuta wagombea ubunge wa EAC.
Mkulu ni nani? Kama una maana ya Rais Magufuli basi elewa kuwa nitamshangaa hata yeye kama akikatwa na kuanza kulalamika kwa sababu huo ni utaratibu ambao CCM wamejiwekea katika kutafuta wagombea.
Utaratibu upi huo?Hoja sio yeye kukatwa hoja ni kukatwa bila kuzingatia utaratibu. Kwa namna ambavyo imefanyika mchakato mzima hauna maana kwani mwenyekiti anaweza kuamua nani akatwe na sio kikao.
Sawa fikra za upande mmoja, je huyou wa upande wa pili anasema nini? Nini sababu rasmi za kumkata jina mtu aliyepitishwa kwa kura? Hizi kauli za "fikra za upande mmoja" ndio zile zile ya Mwakyembe juu ya sakata la clouds hazibadilishi kitu!Utaratibu upi huo?
Unaujua utaratibu wa CCM katika kutafuta wagombea wa Ubunge kwenye EAC?
Ulikuwepo kwenye kikao au unajenga hoja kwa kutumia fikra za upande mmoja na mitandao ya udaku?
1. sio professional ni profession.kwani ubunge unasomewa...arudi kwenye professional yake........hana agenda mpya ...ni zamu ya wengine...akumbuke hata yye alipopata nafasi ya kuingia yalisemwa mengi....na kuna mtu alitoka yye akapata nafasi basi ni zamu yake kutoka mwingine apate nafasi.....ule ni ubunge sio umalkia