Tetesi: Rwanda nyuma ya kufukuzwa Shyrose!

Tetesi: Rwanda nyuma ya kufukuzwa Shyrose!

Kiongozi wa kisiasa aliyekomaa ukubaliana na maanuzi ya vikao
Hapo ndipo ninapomuheshimu Jakaya Kikwete
Kwa yaliyotokea kwake 1995
Ingekuwa viongozi wengine wenye tamaa ya madaraka kama kina mamvi
Leo hii angekuwa amefutika katika siasa za Tanzania
Lakini pamoja na yote alitulia
Akawa mtiifu kwa chama chake
Na baadaye 2005 akaja kuwa mgombea
Hilo ni funzo kubwa sana kwa wanasiasa
Katika siasa kuna kupanda na kushuka
Kuna kubebwa na kuonewa
Kuna kung'aa na kufifia
Cha muhimu ni kuwa mtiifu kwa maamuzi ya vikao vya chama
Maoni mazuri
 
Kikao hujadili na sio mwenyekiti kubwata "huyu sitaki hata kumsikia..." halafu ishu inafungwa. Kikwete alijadiliwa na maamuzi yalikuwa kweli ni ya kikao.
Unao huo ushahidi au porojo tu
 
Mkuu kwani term limit ya EALA ni miaka mingapi na shyrose anayo mingapi?
The EALA representatives hold office for five years and are eligible for re-election once for a further term of five years. Take an example of Mzee Adam Kimbisa, if he is re-elected by the National Assembly.
 
Hivi huyu yeye nani!!?
kwamba hakuna wengine!!
hii mbaya kabisa
kama waliomba zaidi ya 100 kuondolewa yeye tu iwe kelele!!
huo ubunge ni wamaisha!!
Unaichukia Rwanda hasa Serikali ya Kagame
tunajua
lakini usituvuruge kwa kuunganisha chuki zako
na suala hili.
Kama kutetea Maslahi ya Tanzania hawezi kuyatetea pekee
Wengine waliondolewa kwa sababu au vigezo zilizojadiliwa, na sio mwenyekiti single handedly. Najua wewe una mahaba na Rwanda as well.
 
The EALA representatives hold office for five years and are eligible for re-election once for a further term of five years. Take an example of Mzee Adam Kimbisa, if he is re-elected by the National Assembly.
shyrose ana miaka mingapi? Mbona to the best of my recollection aliingia na Kimbisa na Makongoro? i stand to be corrected.
 
shyrose ana miaka mingapi? Mbona to the best of my recollection aliingia na Kimbisa na Makongoro? i stand to be corrected.
Mitano. Re-election hufuata mchakato kama wa mwanzo. Wakati huu hakupenya kwenye mchakato. Aendelee na mambo mengine, vyeo ni temporary (nakubaliana na Rais Magufuli)
 
Unao huo ushahidi au porojo tu
ushahidi wa mwenyewe na wa kimazingira upo. Huwezi kumkata incumbent bila kuonyesha alivyofeli kwenye vigezo. Just like haiwezekani kumkata magu 2020 kama utakavyowakata wanaoanza mwanzo, kwa kuwa huyu ulishampitisha for the first tem, maana yake alishakidhi vigezo vya mwanzo, hivyo kumkata inabidi uthibitishe kuwa vile vigezo alivyokuwa navyo sasa hana tena.
 
Wengine waliondolewa kwa sababu au vigezo zilizojadiliwa, na sio mwenyekiti single handedly. Najua wewe una mahaba na Rwanda as well.
Sina mahaba na Rwanda
wala siichukii Rwanda
lakini lazima kuwe na ukweli nasi chuki binafsi
wew nakusoma sana humu jf
kabla sijajiunga
unachuki kubwa na serikali ya Rwanda
ila unaipenda rwanda maana wewe ni mnyarwanda
 
Shyrose ndio aliyezima jaribio la Rwanda kutumia bunge la EAC kwa maslahi ya utawala wao wa kidikteta, ikiwemo kuongoza wabunge kupinga kupinduliwa kwa spika aliyekataa hoja ya Rwanda kutengeneza historia batili ya genocide ambayo ingekuwa endorsed na bunge hilo. Shyrose pia alikuwa mstari wa mbele kupinga ardhi yetu kuwa ya cha wote ndani ya EAC, kinyume na matakwa ya Rwanda. Hilo ndio kosa lake.

Bahati mbaya mkuu wa sasa ni "rafiki" (mwenzao?) wa utawala wa kidikteta wa Rwanda, hili liko wazi. Sera yetu juu ya Rwanda kisiasa tuliyokuwa nayo toka tuwasuluhishe 1994 imepinduliwa chini juu! Hii ndio sababu haijawahi kutokea mtu anakatwa jina na mwenyekiti kimabavu bila kikao kuelezwa chochote kile!

Kashfa hizi zinazorudiwa rudiwa kuhusu ulevi na kupigana etc, zilishathibitika kuwa ni fitna za vyombo vya habari vya serikali ya Rwanda humu humu JF kitambo sana. (threads ziko chini). Jamani, bunge la EAC linaendeshwa kwa sheria, mbunge akikosea anafukuzwa kama ilivyo bunge lingine. Ukweli ni kuwa baada ya vyombo vya serikali ya Rwanda kueneza propaganda juu ya Shyrose, HAKUNA SHITAKA HATA MOJA ambalo shyrose alipewa kutokana na huo uzushi wa Rwanda! Na mtu akifanya fujo kwenye ndege pia hukamatwa immediately akitua huko anakokwenda. Vyombo pekee vya habari vilivyoandika habari hizi ni vya serikali ya Rwanda!
In fact SERIKALI YETU WENYEWE pia ilisimama kifua mbele kwa kumtetea shyrose! (thread hapa: Serikali: Shy-Rose hakupigana Kenya), leo hii mkuu wa serikali anamkata Shyrose kwa tuhuma zipi tena?

Shyrose so far ndio mbunge mwenye mchango mkubwa EAC kuliko wengine, lets be objective hapa, ni mchango gani wabunge wengine wote wa TZ wametoa bungeni EAC kumzidi shyrose? Kwa nini hoja isiwe kiwango cha kazi yake na badala yake tunajikita kwenye mfumo dume kuhoji masuala ya ndoa yake? Huu ni unafiki just because she is a woman!

Hatari tuliyonayo sasa ni kuendeshwa na Rwanda. Hii ndio system yao duniani kote, unapoingia utawala rafiki na wao, wale maadui zao wote wa zamani huwa "wanasomeshwa" namba kama anavyofanyiwa Shyrose. Msishangae kashfa mbalimbali zikaanza kuibuka dhidi ya Membe, Kikwete, Kamanda kibolwa na wengineo wote.

Na tusishangae sasa tukaanza endorsement ya historia ya genocide according to Kagame, ingawa nchi yetu ilikuwapo na ilishuhudia what happened, tayari amri za ma DC kuwatoa wafugaji haramu maporini kule Kagera, zinatenguliwa na "ngazi za juu" kwa upuuzi eti "hatuna pa kuwaweka wanyama"! Sasa tusishangae serikali yetu ikiridhia kuwa ardhi yetu ni iwe ni free for all kwa EAC wote n.k
Kwa tunaoelewa geopolitics, shyrose will always be a heroine!

Past theads:
1. Shy-Rose Bhanji Ajitetea
2. Sakata la Shyrose Bhanji na agenda ya Wanyarwanda kumng'oa Spika wa Bunge la Afrika Mashariki
3. Aibu: Shyrose Bhanji azua tafrani ziara ya EALA
Hivi hamjui kuwa rais wetu ana asili ya rwanda na huenda baadhi ndugu zake wa damu bado wako huko. Kumbuka kagame ndiye aleyempa semina elekezi baada ya kuapishwa ndio maana maamuzi yake ni ya kikagamekagame
 
Si mmalizane wenyewe na huyo Dikteta wenu. Hata mkija kulialia hapa JF, sisi tunawasaidieje?
 
ushahidi wa mwenyewe na wa kimazingira upo. Huwezi kumkata incumbent bila kuonyesha alivyofeli kwenye vigezo. Just like haiwezekani kumkata magu 2020 kama utakavyowakata wanaoanza mwanzo, kwa kuwa huyu ulishampitisha for the first tem, maana yake alishakidhi vigezo vya mwanzo, hivyo kumkata inabidi uthibitishe kuwa vile vigezo alivyokuwa navyo sasa hana tena.

Haha ndio maana mnaliali
mlikuwa na 100%
 
Mitano. Re-election hufuata mchakato kama wa mwanzo. Wakati huu hakupenya kwenye mchakato. Aendelee na mambo mengine, vyeo ni temporary (nakubaliana na Rais Magufuli)
1. Nashukuru kwanza tumekubaliana kuwa kuwa ishu sio term limits.
2. Tukija kwenye mchakato mbona alishapita kwenye hatua za mwanzo za kupigiwa kura na kufikia top 4? Amekatwa at the last stage ambayo kikao kinakaa na kujadili waliopitishwa. According to waliopo ndani ni kuwa mkuu aliamua kuskip jina lake altogether akidai "hataki hata kumsikia, hataki mjadala kwenye jina hili...." How is this fair? Hii haina tofauti na majina ya mfukoni ya kikwete kweney kumkata lowassa. Na ndio sababu huwezi kukwepa uhusiano wa mkuu na Rwanda katika hili.
 
Hivi hamjui kuwa rais wetu ana asili ya rwanda na huenda baadhi ndugu zake wa damu bado wako huko. Kumbuka kagame ndiye aleyempa semina elekezi baada ya kuapishwa ndio maana maamuzi yake ni ya kikagamekagame
Mamuzi ya kikagamekagame kila mtu anayaona.
 
1. Nashukuru kwanza tumekubaliana kuwa kuwa ishu sio term limits.
2. Tukija kwenye mchakato mbona alishapita kwenye hatua za mwanzo za kupigiwa kura na kufikia top 4? Amekatwa at the last stage ambayo kikao kinakaa na kujadili waliopitishwa. According to waliopo ndani ni kuwa mkuu aliamua kuskip jina lake altogether akidai "hataki hata kumsikia, hataki mjadala kwenye jina hili...." How is this fair? Hii haina tofauti na majina ya mfukoni ya kikwete kweney kumkata lowassa. Na ndio sababu huwezi kukwepa uhusiano wa mkuu na Rwanda katika hili.
Top 4 alifikaje wakati wamepitishwa 12? Jiongeze, acha kuamini viblog uchwara
 
Sina mahaba na Rwanda
wala siichukii Rwanda
lakini lazima kuwe na ukweli nasi chuki binafsi
wew nakusoma sana humu jf
kabla sijajiunga
unachuki kubwa na serikali ya Rwanda
ila unaipenda rwanda maana wewe ni mnyarwanda
....hiyo line huwa mnaipenda kweli ya kuwa mlisoma threads zangu kabla hamjajiunga. Sijui ni watu wangapi huwa mnawasoma na kuwakariri kabla hamjajiunga. So for 7 years unamsoma jmali ila ukajiunga 2015! Okay.
 
Back
Top Bottom