Ukifatilia kwa karibu, utagundua ukabila ni kisingizio tu. Pale kuna ubavu wa watu wazito,wasiotaka kuonekana, wanaojikinga kwenye ukuta wa watu furani, wao wasionekane, ila ndo wanakoleza moto kwa masrahi yao. Kuanzia watu binafsi, makampuni na mataifa.
Mfano hai: siku za nyuma ulisikia Umoja wa Ulaya ukitaka kuipa serikali ya Rwanda,msaada wa Euro milioni 22. Msaada huu, ulikuwa tu kwa ajili ya jeshi lililopo Mozambique. Badhi ya nchi zikagoma usitolewe, badhi zikasisitiza utolewe. Ikasemekana: Uingeleza ilikuwa na dili lake la wakimbizi haramu, ilitakiwa inyenyekee. Ufaransa, wana mradi wa Gesi huko, na jeshi la Rwanda ndo linalousimamia. Raisi wa ufaransa huyo huyo, ndo anaesimama mbele za umati wa watu na kudai Rwanda iondoe majeshi yake. Apple, kampuni ya mmarekani. Sasa hivi yeye na raisi ni pete na kidole. MAdini ya Congo, ndo hayo hayo yanayomuingizia. Je,afunge kiwanda? Raisi huyo unadhani ana undugu na mwafrika? Kila aliyepo kule, yupo kimasrahi tu.