Lavit
JF-Expert Member
- May 16, 2011
- 14,834
- 32,522
Kwa hili Rwanda nawapongeza sana, zile kelele za alfajiri zinakera sana.
Hii ni Taharifa ya BBC...
Waislamu wanaoadhimisha mwezi mtukufu wa Ramadhani nchini Rwanda hawasikii adhana wakati wa swala ya asubuhi, na huenda wasisikie tena, kutokana na marufuku iliyowekwa na mamlaka nchi humo.
Mwezi uliopita mamlaka ilipiga marufuku matumizi ya vipaza sauti kwenye misikiti asubuhi na mapema, ikisema kuwa ilikiuka sheria za uchafuzi wa kelele ambazo zinakataza kelele zaidi ya decibel 55 wakati wa mchana na decibel 45 usiku katika maeneo ya makazi.
Mamlaka ya Rwanda inasema kuwa wakaazi walilalamika kuhusu mwito wa mapema wa maombi - ambao hufanyika majira ya alfajiri na huchukua kama dakika mbili au tatu.
===
Waislamu wanaoadhimisha mwezi mtukufu wa Ramadhani nchini Rwanda hawasikii adhana wakati wa swala ya asubuhi, na huenda wasisikie tena, kutokana na marufuku iliyowekwa na mamlaka nchi humo

"Uamuzi huo ulikiuka haki zetu za kutekeleza imani yetu," anasema Zaina Mukamabano mwenye umri wa miaka 55 ambaye anaishi katika mji mkuu, Kigali.
Anasema ni mara ya kwanza katika maisha yake kuwa hakuna wito wa maombi, au "adhan", asubuhi wakati wa Ramadhani.
Zoezi la kupachika vipaza sauti kwenye minara kwenye misikiti lilianza huko Asia katika miaka ya 1930 na kuenea kote ulimwenguni. Wito tano hutolewa kwa siku, kuwaita waumini kwa sala zao tano za kila siku.

"Hatuna furaha ... wakati wa Ramadhani ni adhana ambayo inatuambia kuwa ni wakati wa kuanza kufunga, na sio Waislamu wote nchini Rwanda wana saa za kengele," anasema mkazi mwingine, Nuhu Bihibindi.
Bi Mukamabano anasema serikali ingeweza kuiambia misikiti kupunguza tu sauti, "kama wanavyowaambia mabaa kupunguza sauti ya muziki wao".
“Adhana ni utamaduni wetu, ni imani yetu, kuipiga marufuku ni kuwakera Waislamu, kutokuwa nayo wakati wa Ramadhani kunatia uchungu zaidi,” anasema.
Mkazi mwingine wa Kigali, Issa Karim Mugabo, anasema yeye na wengine sasa wanafikiria kupeleka serikali mahakamani.
Lakini Sheikh Souleiman Mbarushimana, mshauri wa mufti wa Rwanda, na mwanazuoni wa Kiislamu, anasema viongozi wa Kiislamu tayari wamelijadili suala hilo na serikali na kukubaliana juu ya uamuzi huo.
"Waislamu wanasema haki yao ya imani ilikiukwa ... lakini mamlaka imetuambia (Adhana)] imepigwa marufuku kwa manufaa ya wote," Bw Mbarushimana anasema.
"Tulisema kwamba lazima tukubaliane na kuendelea, kwa sababu imani yetu pia inatutaka kuheshimu uamuzi wa mamlaka."
Sent from my Redmi Note 9S using JamiiForums mobile app