Rwanda wamewafikisha Mahakamani walioruhusu pombe haramu, je Tz tunasubiri nini?

Stuxnet

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2011
Posts
18,875
Reaction score
29,427
Ofisi ya Upelelezi wa Rwanda (RIB) imewakamata Prof. Emile Bienvenu, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini Rwanda (Rwanda FDA), pamoja na watu wengine 17 katika uchunguzi unaohusu uzalishaji na usambazaji wa vileo vinavyodaiwa kutokidhi viwango.

Kati ya watu 18 waliokamatwa, 10 ni wafanyakazi wa Rwanda FDA, huku wengine wakitoka Rwanda Standards Board (RSB) na serikali za mitaa.

Kwa mujibu wa RIB, Prof. Bienvenu anachunguzwa kwa madai ya kutoa leseni ya uendeshaji wa biashara ya chakula na vinywaji bila kufuata kikamilifu uamuzi wa kamati ya kitaalamu ya Rwanda FDA.

Soma pia

Your browser is not able to display this video.


Mytake: Wakati aina 14 ya vinywaji hivyo vinatoka Tanzania, lakini huku kwetu hakuna aliyefikishwa kwenye vyombo vya sheria. Tunasubiri nini?
 
 
Tanganyika kwa mvinyo feki ni kiboko. Juzi kati hapo nipo katikati ya JIJI nimekuta kuna jamaa ananunua machupa ya K-VANT yalio tumika bila uoga.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…