Rwanda wanajenga kinu cha Nyuklia; sisi bado tuna maono ya kujenga madarasa miaka 60 ya uhuru

Rwanda wanajenga kinu cha Nyuklia; sisi bado tuna maono ya kujenga madarasa miaka 60 ya uhuru

US itaisambaratisha kama ilivyofanya Iran, Korea Kaskazini nk. Nuclear Power ya South Africa inatosha kusambaza nishati kwa bara lote la Afrika kwamba hatuhitaji Rwanda et al (sundries).
Nuclear power ya South Africa ndogo nayo haiwatoshelezi! Inazalisha 5% tu ya mahitaji yao.
 
You sound logical mkuu, why? hata ile gesi pale Lindi, tumeshindwa kama taifa kujenga kiwanda hadi leo badala yake inasafirishwa kwa meli kwenda Ulaya ili ichakatwe huko ndiyo irudishwe kwa mlaji Tz kutumia majumbani na mahospitalini. Veta waligundua siku nyingi matumizi ya gesi kwenye magari lakini ubunifu wote huo unaachwa ufie mbali, tutapataje kupona kama taifa? Mgunduzi wa kwanza wa bunduki duniani aligundua gobore kwanza ndipo ikaboreshwa kuwa bunduki ya kisasa, sisi hapa wagunduzi wa gobore wanaozea jela, wa redio nao wanaozea jela, wa ndege za kuruka kilomita moja nao wanaozea jela. Mhe. Majaliwa kule Kigonsera Secondary akiwa mwanafunzi alibuni redio hadi ikawa inapokea mawimbi hakuendelezwa kipaji chake akaishia kwenye siasa. Rwanda leo wana kiwanda cha ku-assemble simu za viganjani na magari. EAC cake inagombaniwa na Kenya na Rwanda not Tz na Uganda, kama ni soka ktk EAC, basi Kenya na Rwanda ndiyo kama Simba na Yanga sisi huenda ni Geita sijui! Hatuwezi kukataa ukweli kwamba kuna sehemu tuna dosari.
Mifano ni mingi sana mkuu,Brazil ambayo ilikua na mashamba ya miwa na mazao mengine ya kulisha ulaya ndio imebaki nyuma huku nchi za ulaya zikipiga hatua kubwa,mfano mwingine simple tu ni huu.MKULIMA WA TZ HUA ANATUMIA GHARAMA KUBWA MPAKA ANALUFIKISHA ZAO SOKONI LAKINI CHA AJABU YULE MFANYA BIASHARA NDIE ANAETENGENEZA FAIDA KUBWA KULIKO HUYO MKULIMA.
 
Mfano CHADEMA badala ya kuja na sera mbadala za maendeleo wao wanachangishana hela za kuwapa familia za makomandoo.
Mkuu CDM waliambiwa ndiyo wanaurudisha maendeleo nyuma, ikaamuliwa au likapitishwa azimio kwamba kuanzia Kiongozi wa nyumba 10 hadi Rais watoke CCM kwenye uchaguzi mkuu, hili likafanyika kama lilivyoamuliwa na Kamanda mkuu wa wakati huo.

Haya leo viongozi wote ni CCM sasa haya maendeleo yanakwama wapi tena? maana wafanya fujo wote wapo benchi.
 
Ni lazima viongozi wote wabadilishe namna ya kufikiri, haiwezekanu miaka 60 ya uhuru serikali imekazana kujenga madarasa tu na vyama vya siasa vimejikita kwenye kusaka ruzuku.

Mfano CHADEMA badala ya kuja na sera mbadala za maendeleo wao wanachangishana hela za kuwapa familia za makomandoo.

Wenzetu Rwanda wanajenga kinu cha Nyukria kwa ajili ya kuzalisha umeme sisi tunakazana na majenereta.

RIP Julius Kambarage Nyerere
Jambo moja la kushangaza ni hii project ya kujenga madarasa na kununua madawati ambayo haina mwisho. Kila mwaka kuna emergency ya uhitaji wa madarasa na madawati. Kama shule mfano ina capacity ya wanafunzi 3000 na kila mwaka darasa la saba wanaondoka labda 500 , si yanabaki madarasa waliokuwa wanatumia std seven na madawati yao. Kwa maana nyingine kila mwaka wakishaondoka std seven wanaacha nafasi kwa ajili ya std 1. Inaeleweka pia kwamba registration ya watoto ilipanda kwa miaka michache iliyopita kufuatia juhudi za serikali kuondoa ada na mambo kama hayo, kwa hiyo ilitegemewa hi dharura ya madarasa na madawati iwe imeisha kwa sasa baada ya kuongezwa miundombinu hiyo ili kuendana na mahitaji mapya. Sasa kwa nini kila mwaka hii kadhia haiishi
 
Rwanda inaingia mara ngapi kwa Tanzania?
Kieneo na idadi ya watu?
Assume Tanzania ingekuwa Dar es salaam labda na mikoa kama Pwani na Morogoro,unafikiri tungekuwa wapi kimaendeleo?
Hela yote inayokusanywa Dar inaishia kuwahudumia ndugu zako walioko huko madongo poromoka.
Wakati mwingine unapoibua hoja basi tumia logic.
N.B:Logic ni aina ya hesabu ambazo hazina namba waliosoma hesabu Kama kozi wanajua.
Hesabu hizo hukusaidia kufikiri sawasawa.
 
Hahahaa mkuu, hii kitu ni kama hospitalini, wagonjwa wengi wanaruhusiwa lakini dawa, vifaatiba na vitanda bado vinaongezwa tu, population inavyokuwa, ignorance na diseases navyo vinakuja sambamba na ukuaji wa population, hivyo lazima kuwe na muendelezo. Kwa kawaida Mwl anatakiwa afundishe watoto 25 tu kwa standard za UNESCO lakini mafuriko ni makubwa kiasi kwamba wanaomsikiliza Mwl darasani ni wale wanaokaa mbele tu. Nakumbuka kwy awamu ya pili ya JMT wanafunzi wa UD walikuwa wanajaza lecture theatre hadi wengine wanasimama nje dirishani, mabweni nayo yalikuwa hayatoshi hata leo wanaoruhusiwa kwenye mabweni ni finalists na beginners.
 
Hapo sasa unawatukana CCM ambao wanadhamana na hawana mawazo maana chadema haikusanyi kodi, maccm ndio hukusanya kodi na kupanga kujenga madarasa yaani kazi yakufanywa na serikali za mitaa na waisimamie na kuiratibu inashabikiwa hadi na Rais wa nchi
[emoji849][emoji102][emoji849]
 
Ni lazima viongozi wote wabadilishe namna ya kufikiri, haiwezekanu miaka 60 ya uhuru serikali imekazana kujenga madarasa tu na vyama vya siasa vimejikita kwenye kusaka ruzuku.

Mfano CHADEMA badala ya kuja na sera mbadala za maendeleo wao wanachangishana hela za kuwapa familia za makomandoo.

Wenzetu Rwanda wanajenga kinu cha Nyukria kwa ajili ya kuzalisha umeme sisi tunakazana na majenereta.

RIP Julius Kambarage Nyerere
Umeme wa maji na gesi unatutosha sana. Kupanga ni kuchagua. Ila huyo mjinga aliyepewa hiyo wizara asepe tu hatuna imani nae.
 
Kwani huyu nyerere na wenzake waliodai Uhuru wameharibu bars afrika,waliwanza kukaa madarkani na vyama vyao.
Unaongelea madarasa CCM hata vyoo vinahitaji wafadhiri
Uwezo wao no kuiba kura tu.Unaongelea nyukilia wakati CCM wanataka kuajiri division three,four na ziro uliza vijana waliomba ajira polisi.
 
Frankly Speaking Rwanda haiwezi kuizidi Tanzania kitu chochote ni hofu na uelewa mdogo...

Maendeleo ya Viwanda Ulaya yalianzia Uiengereza baade mataifa Jirani yalivoona maendeleo ya Uingereza yawatisha wakaanza nao mwisho wa siku wakawa sawa.

Huko East Asia, China, Korea (Josean wakati huo), pamoja na Japan zilikuwa na Sera ya kutoingiliana na mataifa ya magharibi, Japan akawa wa Kwanza kujifunza kwa watu wa magharibi wakaanza kuzivamia China na Korea na Mataifa mengi ya Pacific... lakini Wachina na Wakorea hawakuridhika wakaanza nao kuwa kama mataifa ya Magharibi

Leo Japan, China na Korea hawatishani.

Kwa Afrika Mashariki Tanzania itabaki na kuendelea kuwa taifa kubwa na lenye nguvu..

Miaka 5 iliyopita Kenya Airways, Rwanda Air ways ndio yalikuwa mashirika Maarufu ukanda huu lakini leo tunavoongea ATCL inatakribani ndege 16 ambazo ni nusu ya KQ (40).

2013, Kenya, Uganda na Rwanda waliaamua kuunzisha umoja wao ili kujenga SGR leo tunavoongea ni Tanzania na Kenya ndio tumeweza kuanza na Tena Tanzania tumejengwa way more better than anyone.

Ikija kwenye Kutumia Urani, Only Tanzania na Kenya ndio wanaweza kuanza haraka na ndani ya muda mfupi, Rwanda is too overrated

NOTE: Hakuna Taifa dhaifu linazongukwa na Taifa lenye nguvu.
Watanzania wanahofu kwa vitu ambavyo hata havipo..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unajisikiaje kuwa mmoja wa watu wa kueneza propaganda mitandaoni wakati mama zako na ndugu zako kule vijijini wanapata shida ya huduma bora za afya pamoja na shida ya maji katika maeneo yao??miaka 60 sasa wapo na shida hizo..Huoni kama unawasaliti?
Acha tu jombaa, wakishashiba wao baasi tena!! Ubongo unakuwa shonde
 
Ukubw
Mkoa wa Tanga ni mkubwa kuliko Rwanda. Kwa maana nyingine Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima ni level ya president wa Rwanda
Hizi fikra ni za kubadilisha,
Ukubwa wa nchi siyo ukubwa wala uimara wa taifa, kuna vinchi vidogo kwa eneo lakini wanauwezo mkubwa
 
Rwanda inaingia mara ngapi kwa Tanzania?
Kieneo na idadi ya watu?
Assume Tanzania ingekuwa Dar es salaam labda na mikoa kama Pwani na Morogoro,unafikiri tungekuwa wapi kimaendeleo?
Hela yote inayokusanywa Dar inaishia kuwahudumia ndugu zako walioko huko madongo poromoka.
Wakati mwingine unapoibua hoja basi tumia logic.
N.B:Logic ni aina ya hesabu ambazo hazina namba waliosoma hesabu Kama kozi wanajua.
Hesabu hizo hukusaidia kufikiri sawasawa.
Hiyo Dar yenyewe zaidi ya asilimia 70 ni unplanned area na uswazi!

Maeneo ka Tandale, Buza, Tandika, Mbagala , Buguruni, Keko hivyo ni vijiji au kwasababu viko Dar unadhani sio vijiji.
 
Mwamba umetisha Sana unauelewa wa vitu vingi Tena kwa upana

Wapo watakaokubeza lakn ukwel mchungu binafs hoja yako zakujenga zaidi

Tungepata watu 10 top leaders wenye mawazo Kama haya hakika tungekuwa mbali

Kudos bro
Huyo msomi amejibu kiu yangu na nimejifunza. Kitu kutoka. Kwake. Na ni ukweli mtupu lakini tatizo sio viongozi tu hata sisi wananchi kuna sehemu hatuko sawa vichwani kuna jamaa mmoja alimnunulia mchepuko wake simu ya raki 3 huku akiwa na.deni LA kodi ya nyumba na ilihali yy. Mwenyewe simu yake ni kiswaswadu
 
Hiyo Dar yenyewe zaidi ya asilimia 70 ni unplanned area na uswazi!

Maeneo ka Tandale, Buza, Tandika, Mbagala , Buguruni, Keko hivyo ni vijiji au kwasababu viko Dar unadhani sio vijiji.
Achana na mambo hayo tunaonglelea kipato.Masuala ya squatters hata South Africa yapo pamoja na maendeleo yote waliyonayo.Kujenga kinu cha Nyuklia yahitaji pesa.Pesa zote zinazokusanywa na serikali zinaishia huko madongo poromoka,vinginevyo Tanzania ingekuwa mbali sana kama sio ukubwa wa nchi na wingi wa watu!
 
Una kichaa wewe umeambiwa zaidi ya asilimia 70 ya dar haijapimwa !

Niambie ni mji gani South Africa wenye wastan wa kutopimwa kwa asilimia 70. Unaongea pumba tu.

Sent from my CPH1803 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom