Rwanda wanajiandaa kwa SGR itakayowafikia ya kwanza kati ya Tanzania na UGanda


Mumesubiri miaka hamsini tangu uhuru, bado tupo na tunaendelea kutanua.
 
Mumesubiri miaka hamsini tangu uhuru, bado tupo na tunaendelea kutanua.
Mnatanua nini...mambo yanawaendea fyongo nyie baada ya kuangaliaa mnarekebishaje mnakuja bishana na watoto wa magu hakyamungu mtakoma hii miaka kumi ya magu tutaona vingi ..
 
Mumesubiri miaka hamsini tangu uhuru, bado tupo na tunaendelea kutanua.
Hivi ukiweka nchi zote za kibepari duniani, sijuwi South Korea, Japan Australia, western Europe, Canada etc. Kenya mnajilinganishaje na hao wenzenu? Kwanini nchi kama Malaysia au Singapore wametumia ubepari wao wakafika wanakotaka kufika lakini Kenya bado inashindana na Tanzania na Ethiopia tena iko hatarini kuachwa.
 

Kenya ukilinganisha na majirani zetu sote, sisi ndio nchi tajiri.
Ethiopia wale wapo raia zaidi ya milioni mia moja, hivyo tukiingia kwenye per capita hawana lolote mbele yetu, pamoja na kwamba nchi yao kubwa utadhani bara lingine.
Ila wao nafuu kidogo sio mivivu kama nyie.

Sasa ukiaondoa hao Ethiopia, nyie wengine wote mliotuzunguka bado mnatajwa kwa nchi maskini was kutupwa. Hata DRC ambao nao wana liinchi likubwa zaidi yenu, lakini mnatajwa nyote kwenye kundi moja.

Sisi ubepari wetu ndio umetuwezesha kufika hapo tulipo, kwamba ukilinganisha na maitaifa yote ya ukanda huu
Kenya ndio muwekezaji mkubwa Tanzania, Uganda, Rwanda, Burundi, DRC, Sudan n.k.

Leo hii tungekua hata mbali zaidi tatizo tumezungukwa na mivivu hivyo yanatuchelewesha, inatubidi muda mwingi kupunguza kasi ili kuendana nyie, lakini tungezungukwa na mataifa kama Malaysia, Singapore aisei ligi yetu ingekua mbali.

Hii Africa bora wangeweka pamoja nchi za wachapa kazi kama Ghana, Botswana, Kenya, Rwanda n.k.
Halafu mivivu kama Tanzania na wenzake wasindikwe kwenye kundi moja, lakini sasa hilo haliwezekani, inabidi kuwavumilia, tumeunganishwa na nyie kwenye kiuno hivyo tunaishia kuwaburuza kote tuendako.
 
Vipi MK254 yale mahindi ya msaada kutuliza njaa Kenya yashawasili Mombasa? Hapa ni kupiga hela tu (kwa sauti ya MK254)
 
Hayo ya kuita mara equal partner mara ndugu mara swahiba ndio hulka yenu, sisi ni wabepari tunapiga hela hatujui huo upuzi. Tunapiga mahesabu ya mulaa, mbeca, money.... Mambo ya undugu peleka kijijini lakini mjini ni mkao wa kukwapua.
naona muzungu mweusi katika ubora wako!!!eti wabepari.....
 

Umeongea pumba nyingi bila maana yoyote, ni jambo la ajabu sana kwa nchi kama Kenya kujita ya kibepari halafu ina uchumi wa $70 billion tuu. Angalau sisi tumepitia zama za kila aina zenye majaribu lukuki. Huku vita na Uganda, kule ukombozi wa kusini mwa Afrika, mara sera za East-West. Kenya mtatoa sababu gani kuhalalisha uchumi wenu kuwa chini ya $100 billion? Kwanini hamko sawa au zaidi ya Afrika kusini? nchi iliyokuwa haina marafiki hapa Afrika (zaidi ya Kenya) huku wana vikwazo vya uchumu?
 
Hivi mtu tajiri anaweza kuongoza ukanda huu kwa njaa?, mtu tajiri anaweza kuongoza kwa slums?, mtu tajiri anaweza kuongoza kwa unemployment?, mnachoongoza hapa EA ni ukabila, rushwa, umasikini wa kipato na mauaji ya raia yanayofanywa na vyombo vya dola, nchi lenu linafilisika mnakimbia na kutawanyika dunia nzima, kama Ethiopia, Somalia, Yemen na Syria wanavyotawanyika.

Utasemaje ninyi ni wachapakazi wakati 20% ya ardhi yenu inafaa kwa kilimo lakini ipo mikononi mwa mabepari wachache wanalima maua na kufuga wanyama matokeo yake mnatia aibu katika ukanda huu kwa kuwa nchi pekee inayopewa msaada wa chakula miaka 54 baada ya kupata uhuru bado mnapewa msaada wa chakula, na bado vichaa wanasifia ubepari.

Mimi sielewi mtu anajisifia kwamba ni tajiri lakini hana chakula, hana Hospitali bora, hana ajira kwa wananchi wake, maji ya kutumia ni mgao, hana nyumba bora kwa watu wake bado watu wanaishi kwenye slums, anashindwa kuimarisha usalama kwa wananchi wake. Hivi nani ana bahati mbaya kati ya Kenya na Tanzania kwa kuwa majirani?, Kenya inaitegemea Tanzania kupata chakula, kupata eneo la uwekezaji, na kupata nchi ya kujificha kwa muda kunapotokea machafuko ya kisiasa na ukabila, Tanzania inafaidika nini toka Kenya, msilazimishe mambo kwa kusema umeshikanikwa kiunoni wakati bila Tanzania hamuwezi kuishi, South Sudan, Somalia na Ethiopia, zote ni majirani zenu, mbona hamuendi huko na kusema muefunganishwa kiunoni?, Mungu amewalaani kwa ukabila wenu, kila siku mnauana imefikia hatua nchi inagawanyika katikati, na bado mtazidi kuuana na huku hatuwaruhusu bila passport.
 
hehehe,wah utafanya wajinyie maana jamaaa wana mawazo taka kweli
 

Sababu nimetoa tosha kwamba tulizungukwa na wavivu, lakini pia kuna kipindi tumepitia kigumu chini ya CCM ooops! Nimegusa jina ambalo likitajwa huwa unahisi kulia, ndio tumepitia wakati mgumu chini ya chama kilichotunyanyasa kama CCM inavyofanya Tanzania miaka yote.

Lakini cha msingi, ukanda wote huu sisi ndio tunangoza kwa kila kitu, kielimu, kijeshi, kiafya, kiuchumi yaani orodha ndefu, hayo ni matunda ya uchapa kazi pamoja na kwamba kainchi ketu kadogo na zaidi ya nusu yake kame tupu. Nyie liinchi lote hilo, kwanza nchi mbili zilizounganishwa kiusanii, mna kila kitu lakini mivivu wa kutupwa, umaskini balaa na ushirikina wa kuwatafuna albino.

Hapo awali ningewaelewa maana mlijitetea kwamba mlicheleweshwa na kiherehere chenu cha kuingilia ugomvi wa nchi za Kusini, na pia ujamaa uliowalemaza kiakili, lakini leo hii hamna chochote kimewakwamisha zaidi ya uvivu tu.
 
Bado unaruka ruka hutaki kusema ukweli. Nimekupa nafasi ujieleze sababu kwanini Kenya ipo ilipo sasa na sio mbali zaidi lakini naona unaogopa kusema ukweli.

Ngoja nikupe ukweli, usitafute mchawi mara sijuwi majirani zetu wavivu, mara tungekuwa karibu na Ghana Nigeria tumgekuwa mbali. Hizo ni sababu za uwongo. Tatizo la Kenya haliko mbali na Kenya liko halo hapo Kenya tena kwenye ofisi kuu ya nchi. Rais wenu wa kwanza ndio aliwauza kwa kujilimbikizia mali peke yake na familia yake na marafiki zake, bila kusahau kabila lake. Kenya ni nchi yenye rasilimali asili kidogo sana kulinganisha na nchi zingine za Afrika, mtaji mkubwa ulikuwa ni rasilimali watu. Lakini hakuna alikubaku kuwaendeleza watu watakao kuja kudai mali ya nchi kitu ambacho kitapunguza utajiri wa bwana Fulani.

Angalia Gavana wa Mombasa anavyo lalamika kazi za Mombasa zinahamishwa kwenda Naivasha kwa akina bwana Fulani.
Fear over loss of jobs as SGR takes on cargo

Wewe unaona Kenya imefikia uchumi wa $70 billion unachekela. Bila hata majirani zenu kuwa imara, mgekuwa mbali kama wanachi wote wangeshirikishwa kwa kutoa haki sawa kwa kila raia. Tatizo muda umewapa kisogo, nchi zingine zimesha amka. SGR iliyotakiwa kujengwa Kenya tokea 1980s wakati uchumi ulikuwa mzuri, mnajenga leo tena iko hatarini kuwa tembo mweupe maana soko linahama.
 
Endelea kuota ndoto za mchana, zaidi ya umasikini, rushwa, ukabila, unemployment na sifa za kijinga, hamuifikii Tanzania kwa lolote, mtabaki na mawazo yenu ya kizamani wakati tunaongoza kwa kasi ya kukua kwa uchumi katika ukanda huu, tunahospitali nyingi na bora kuliko ninyi, wakenya wanajazana kuja kutibiwa Ocean road Hospital, KCMC, na Hospital ya Moyo ya Jakaya Kikwete, tumejenga barabara za lami nyingi na ndefu zaidi yenu, tumesambaza maji kwa wananchi wengi zaidi yenu, ninyi hata Nairobi haina maji, tumeunganisha umeme kwa wananchi wengi zaidi yenu, hatuna njas kama ninyi. Sema kitu gani cha maana Kenya imeizidi Tanzania?
Ninyi uchumi unaporomoka, utalii umewashinda, manufacturing industries inakufaa, KQ ipo ICU, akili zenu ndiyo hivyo hazina uwezo wa kufikiria nje ya box zaidi ya kuwategemea wazungu wawaambie nini la kufanya, Tanzania is the anchor of EA, chochote tunachokataa hakifanyiki, na tunachotaka ndicho kinafanyika, mifano ni mingi kuanzia EPA, Uganda pipeline, na sasa hivi SGR, bakini na ukabila wenu msituambukize.
 
Hayo ya kuita mara equal partner mara ndugu mara swahiba ndio hulka yenu, sisi ni wabepari tunapiga hela hatujui huo upuzi. Tunapiga mahesabu ya mulaa, mbeca, money.... Mambo ya undugu peleka kijijini lakini mjini ni mkao wa kukwapua.

Mabepari???mmepigwa mimba na wachina kwenye SGR,unajitapa humu eti maberi!mna akili ndogo sana hadi huruma.
 

Nimekupa majibu, tatizo unataka ujibiwe utakavyo au ulivyoaminishwa na kukaririshwa hapo Lumumba, sasa hilo haliwezekani maana kila mtu ana uhuru wa maoni yake.
Mwisho wa siku pamoja na kwamba kainchi ketu kadogo na nusu kame, sisi ndio mibaba wa kusema ukanda wote huu, miinchi mikubwa kama hilo lenu mnaishi nyuma yetu na mtabaki hapo kwa muda mrefu sana. Tunawashinda nyie na DRC na kila nchi yoyote iliyowazunguka na kutuzunguka, tumeshinda hata Msumbiji, kwa kifupi zungusha macho yako yote uangalie nchi zote zilizowazunguka kuanzia Msumbiji, Malawi, Zambia uende hadi Uganda wote mpo chini yetu, na kumbuka sisi tumewekeza kote huko tena heavily na bado tunatanua.....
 
Sijawahi kuona nchi inayojiita middle income inasumbuliwa kisaikolojia na kiuchumi na nchi ambayo ni LDC kama hiki ambacho tz inaifanyia Kenya. Hongera tz! Hawa lower middle income safari hii hawataamini kitakachowakuta! Muda utasema.

Let the ball roll[emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…