Rwanda: Waziri wa Sheria atimuliwa

Rwanda: Waziri wa Sheria atimuliwa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Rais wa Rwanda, Paul Kagame amemfukuza kazi Waziri wa Sheria ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu, Johnston Busingye

Amefukuzwa kazi kwa kufanya kazi kwa kufuata matakwa yake badala ya kufuata sera za Serikali

1614627067294.png
 
Haya ni matokeo ya interview ya AlJazeera aliyofanya waziri juu ya Rusesabagina’s case. Sasa hapa Kagame anamuangushia jumba bovu waziri maana siri zote zishajulikana.
 
Si bora basi hata angetoa maoni yake binafsi. Yeye kasema ukweli mtupu. Na ukweli kwenye hii kesi ni embarassing to Rwanda, bora hata asingefanya interview.
kafanyaje? kasema nini?
 
kafanyaje? kasema nini?
Kwanza alijichanganya akatuma bahati mbaya video ya ushahidi inayothibitisha Rwanda kuwa ndiyo ilikodi ndege iliyomleta yule jamaa wa hotel Rwandan (hii ikathibitisha kuwa kweli serikali ilimteka tofauti na madai yao kuwa alikuja mwenyewe). Katika kujitetea akaamua kuwambia aljazeera kuwa siyo waliokidi ndege ila walimtumia agent wao ambaye alikuwa karibu na jama wa hotel Rwanda hivyo Rwanda haikuhusikaa moja kwa moja
 
Afanye toba, aandike wosia, aache wasifu wake vizuri, asali sana kwa sababu saa yake imekaribia!

Maskini ukweli hujitenga, jamaa walimteka!

Everyday is Saturday.............................. 😎
 
Hivi waziri akitoa maoni yake binafsi kama yako tofauti na mlengo wa serikali anafukuzwa?
Anafukuzwa saa mbili asubuhi. Kuna kitu wao wanakiita eti “collective responsibility” hata kama kiukweli ni maamuzi na matakwa ya kiongozi mkuu.

Kwa Tanzania I think it is even worse kwa sasa. Jaribu kufikiria tu itokee mama Ndalichako ahojiwe na BBC na kusema watoto wa kike waliopata mimba shuleni wana haki ya kufreeze masomo ili baadae warudi shule kwa miongozo iliyopo
 
Kwanza alijichanganya akatuma bahati mbaya video ya ushahidi inayothibitisha Rwanda kuwa ndiyo ilikodi ndege iliyomleta yule jamaa wa hotel Rwandan (hii ikathibitisha kuwa kweli serikali ilimteka tofauti na madai yao kuwa alikuja mwenyewe). Katika kujitetea akaamua kuwambia aljazeera kuwa siyo waliokidi ndege ila walimtumia agent wao ambaye alikuwa karibu na jama wa hotel Rwanda hivyo Rwanda haikuhusikaa moja kwa moja
Hivi kwa akili yako Rusesabagina ajipeleke Kigali kibwege tu namna hiyo.

Tuongee Timming aliyoliwa, kwamba alijipeleka ni Big No.

Kuna Twagiramungu mpinzani wa PK toka 94 yupo Belgium na Tundu karibia mwaka wa25 sasa.

Hata kwa Bunduki haendi pale Kigali anajua kitachompata.

Rusesabagina aliliwa timming tu na hakuna kesi ni ile tu kamusi ya miafrika tulivyo, "kwanini awe hero wakati sisi ndio tulikomboa nchi"
 
Back
Top Bottom