Nawaza sana nchi ndogo mnoo kama Rwanda ambayo kieneo ni ndogo kuliko hata mkoa wa Pwani hapa Tanzania (huenda kieneo haifiki hata nusu ya mkoa wa Pwani), inawezaje kuwa na nyumba rasmi za ibada maelfu kwa maelfu. Yaani kama Kanisa Katoliki pekee Rwanda lina Parokia zaidi ya 231 (Kanisa katoliki ni mfano mzuri zaidi katika kujipanga kiutarabu wa kujenga nyumba zake za Ibada), hizo ni nyingi mnoo katika eneo la nchi kama Rwanda. Mleta mada anaeleza mpaka sasa Rwanda imeshafungia zaidi ya nyumba za ibada 10000.
Kwa utiriri huo, tukubali tu, Afrika (Rwanda ikiwa ni mfano halisi) tuna shida kubwa mnoo kuhusu ulevi wa kidini, tumegeuza dini kuwa kishaka cha kulewa ili kujisahaulisha matatizo yetu.