Rwanda yaijibu barua ya bunge la Marekani dhidi ya kesi ya Rusesabagina

Rwanda yaijibu barua ya bunge la Marekani dhidi ya kesi ya Rusesabagina

MakinikiA

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2017
Posts
5,104
Reaction score
6,827
Rais Kagame alisema kwamba mpinzani wake mkuu Paul Rusesabagina alidanganywa akajileta mwenyewe nchini Rwanda.

Rais Kagame alisema kwamba mpinzani wake mkuu Paul Rusesabagina alidanganywa akajileta mwenyewe nchini Rwanda.

Waziri wa Sheria nchini Rwanda amemjibu mjumbe wa bunge la Marekani ambaye alikuwa amemwandikia Rais Paul Kagame akimtaka Paul Rusesabagina aachiliwe huru , mkosoaji mkuu wa serikali ya Rwanda , ambaye yuko gerezani nchini Rwanda kwa madai ya ugaidi.

Waziri Jonhnston Businjye amesema kuwa Rwanda ni nchi huru na haichukui maagizo kutoka mahali kwingine.

Wakati huohuo familia ya Rusesabagina imesema itaishtaki kampuni ya ndege ya kibinafsi ya Ugiriki kwa kuongoza njama ya utekaji na kupelekwa kwake nchini Rwanda.

Waziri wa sheria wa Rwanda Jonhston Businjye amejibu barua iliyoandikwa wiki iliyopita na Carolyn B. Maloney , mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Uchunguzi na Mageuzi ya Marekani, akimwandikia Rais Paul Kagame kuwa mwezi Agosti , Rusesabagina alisafiri toka Dubai kwenda Burundi na ndege hiyo kutua Kigali ambapo viongozi wa Rwanda walimkamata.

Mbunge huyo alisisitiza kwamba Rusesabagina alikamatwa katika mazingira ambayo bado ni ya kutatanisha na kwamba alitekwa nyara na vyombo vya sheria vya Rwanda na kuzuiliwa kwa misingi ya kisiasa kutokana na msimamo wake wa kutetea haki za binadamu.

Waziri wa sheria wa Rwanda Johnston Busingye, amejibu barua hiyo kwa kusema kwamba Rwanda ni taifa huru lisilopokea maagizo kutoka kwa nchi yoyote na kwamba Paul Rusesabagina alikuwa mikononi mwa vyombo vya sheria kulingana na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka na kuwa baadhi ya ushahidi ulikuwa wazi akikumbusha mashambulio yaliyoendeshwa na kundi lake katika vijiji kadhaa vya kusini magharibi mwa Rwanda na pia kuwa hadi leo Rusesabagina mwenyewe hajakanusha ushahidi huo.

Paul Rusesabagina

Kesi ya dhidi ya Paul Rusesabagina itaanza kusikilizwa mwezi Januari Rwanda imesisitiza kwamba Rusesabagina anakozuiliwa anapata haki zake zote ikiwa ni pamoja na kuonana na mawakili wake, madaktari bingwa wanaoangalia afya yake na pia kuzungumza mara kwa mara na familia yake.

Nayo familia yake ikitangaza kuishtaki kampuni ya ndege ya kibinafsi ya Ugiriki kwa kuongoza njama ya utekaji na kupelekwa kwake nchini Rwanda.

Anasema mnamo mwezi Agosti alikuwa amenuia kuzuru Burundi kwa shughuli za kanisa lakini ndege ya kibinafsi aliyokuwa ameabiri kwenda Dubai badala yake ilimpeleka Rwanda.

Kesi iliyowasilishwa mbele ya mahakama mjini Texas inadai kuwa kampuni ya ndege hiyo , GainJet, ilikubali kufanya safari hiyo kutokana na uhusiano wa karibu kati yak e na maafisa wa Kigali.

Ni madai ambayo serikali ya Rwanda ilikanusha ikisema alijileta mwenyewe mjini Kigali.

Paul Rusesabagina's trial for terrorism charges will start in January

Kesi ya Paul Rusesabagina dhidi ya mashtaka ya ugaidi itaanza kusikilizwa mwezi Januari

Kesi dhidi ya Paul Rusesabagina imepangwa kusikilizwa rasmi tarehe 26 mwezi wa kwanza mwaka 2021 yeye pamoja na watu wengine 19 waliokuwa katika kundi la FLN ambalo ni tawi la kijeshi la vuguvugu la MRCD ambalo Rusesabagina alikuwa kiongozi wake.

Mkosoaji mkuu wa Rais wa Rwanda Paul Kagame ambaye anazuiliwa gerezani kwa mashtaka ya ugaidi amesema ataishtaki kampuni ya ndege ya kibinafsi ya Ugiriki kwa kuongoza njama ya utekaji na kupelekwa kwake nchini Rwanda.

Paul Rusesabagina - ambaye jukumu lake wakati wa mauaji ya kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994 iliangaziwa katika filamu ya Hollywood ya Marekani kwa jina Hotel Rwanda - alikuwa akiishi mafichoni nchini Marekani na Ubelgiji.

Anasema mnamo mwezi Agosti alikuwa amenuia kuzuru Burundi kwa shughuli za kanisa lakini ndege ya kibinafsi aliyokuwa ameabiri kwenda Dubai badala yake ilimpeleka Rwanda.

Kesi iliyowasilishwa mbele ya mahakama mjini Texas inadai kuwa kamuni ya ndege hiyo , GainJet, alikubali kufanya safari hiyo kutokana na uhusiano wa karibu kati yak e na maafisa wa Kigali.

Kesi sawa na hiyo inatarajiwa kuwasilishwa katika mahakama nchini Ubelgiji ambako Bw.Rusesabagina ana uraia wake. GainJet haijajibu ombi la BBC la kupata tamko lake kuhusiana na madai hayo.
2px presentational grey line

Mapema mwezi Septemba alipozungumza mara ya kwanza kuhusu kukamatwa kwa Rusesabagina, Rais wa Rwanda Paul Kagame alisema kwamba Bwana Rusesabagina hakutekwa, alidanganywa akajileta mwenyewe nchini Rwanda.

Rais Kagame alisema lazima Rusesabagina awajibishwe kuhusu mauaji dhidi ya raia wa Rwanda kufuatia mashambulio ya makundi ya waasi anayoongoza yaliyofanywa dhidi ya maeneo ya Rwanda miaka miwili iliyopita.

''Kumamatwa kwa Rusesababiga ambaye ni mmoja wa waliopanga mashambulio yaliyotoka Burundi ni moja ya njia ya kutekeleza hayo uliyoyasema kwamba unataka haki itendeke kwako na kwa wengine waliopoteza wame na mali zao, hatuwezi kukurusidia mume, lakini kile tunachoweza kukifanya ni kuhakikisha unapata haki yako ya kisheria'', Rais Kagame alimjibu mmoja wa wanawake waliomuuliza kwa njia ya simu kupitia televisheni kuhusu ni vipi anaweza kumsaidia baada ya kifo cha mume wake ambaye aliuawa katika mashambulio.

Baraza la kimataifa la Haki za binadmu kwa ajili ya Rwanda linadai kwamba mtuhumiwa huyo ambaye ana uraia wa Ubelgiji amenyimwa haki ya kutembelewa na ubalozi wan chi hiyo, Shirika la msalaba mwekundu mbali na kwamba pia hawezi kuwasiliana na familia yake.

Paul Rusesabagina yagaragaye mu rukiko yambaye umwenda w'abafungiye muri gereza zo mu Rwanda
Maelezo ya picha, Paul Rusesabagina anazuiliwa nchini Rwanda

Familia ya Rusesabagina imewachagua mawakili 6 wataalamu wa sheria za kimataifa za haki za kibinadamu kumuwakilisha katika kesi inayomkabili nchini Rwanda, kutoka Rwanda, Ubelgiji, Astralia, Marekani na Canada.

Rusesabagina alifahamika kufuatia filamu ya Hotel Rwanda ikielezea jinsi alivyookoa maisha ya watutsi waliokuwa wamekimbilia katika hoteli moja mjini Kigali aliyokuwa meneja wake mwaka 1994.
Rais Paul Kagame amesema kikubwa sio ushujaa wa Bwana Rusesabagina au vitendo vyake wakati wa mauaji ya kimbari akisema kinachoangaliwa kwa sasa ni yeye.

kuwajibishwa kuhusu kwa vitendo alivyotaja kuwa vya mauaji dhidi ya raia wa Rwanda. Bwana Kagame amesema kwamba hajali kuhusu hadithi ya Bwana Rusesabagina kwamba yeye ni shujaa wa mauaji ya kimbari na kwamba ''hilo si jambo ambalo litakalomkabili mahakamani''.

"Kuna maswali ambayo lazima atayajibu.kuna wanaomsaidia wakiwa Ulaya,Marekani na kwIngineko na ambao walimpandisha cheo na kumpa majina ya ushujaa.awe shujaa au la ,mimi sina wasi wasi na hilo.
 
Hapa kwa kuwa kapata umaarufu kupitia sinema, basi lazima anyanyaswe na abadilishiwe kibao mpaka umaarufu wote uwe ni fedheha. Hizi roho za viongozi wetu!
 
Ile filamu yake niliingalia hadi nikalia bila kujielewa.
 
Back
Top Bottom