Rwanda yaongoza kwa Watu wake kuishi Umri Mrefu kwa Nchi za Afrika Mashariki

Rwanda yaongoza kwa Watu wake kuishi Umri Mrefu kwa Nchi za Afrika Mashariki

View attachment 2533425

Utafiti wa #UmojaWaMataifa (UN) na #BenkiYaDunia (WB), umeonesha maisha marefu yanategemea mambo 3 makuu: Maumbile, Jinsia, na Mtindo wa Maisha unaojumuisha Usafi, Chakula Bora na Mazoezi, Upatikanaji wa Huduma Bora za Afya, na Viwango vya Uhalifu.

Hadi kufikia mwaka 2023 umri wa Binadamu kuishi ni miaka 70 kwa #Wanaume na miaka 76 kwa #Wanawake sawa na wastani wa miaka 73.4 huku matarajio ya maisha yakitofautiana kulingana na eneo au Nchi. Kwa #Afrika umri wa chini ni miaka 57.7 na miaka 82 kwa #Ulaya.

Umri wa kuishi umeongezeka kutoka miaka 5.5 kati ya mwaka 2000 na 2016 hadi miaka 10.3 kwenye baadhi ya Nchi za Afrika. Sababu ni Kuboreshwa kwa kiwango cha Maisha ya Watoto wenye Miaka 0-5 na upatikanaji wa Matibabu ya kurefusha maisha kwa wenye #VVU na #UKIMWI.

DATA: UMOJA WA MATAIFA/ BENKI YA DUNIA
Ni kweli kwa Tz wastaafu wengi hawatoboi 70
 
Lakini mtu anayeishi Ulaya leo anategemewa ataishi miaka 100. Kwa hiyo unasemaje? Japan huko life expectancy itafika 100 plus
Kuzidi na kupungua kupo
Kuna wengi tu hawafiki hata 50 au 40

Huo ndio wastani, hayo mategemeo ya 80 na 100 yapo pia
 
Muudy alikuwa mzee wa kukopi na kupesti!
Mtu ambaye alikua hajui kusoma wala kuandika atakopi wapi?
"Hasemi kwa matamanio yake, hayakuwa haya anayoyasema ila ni ufunuo kwake"

Yaani ni wahyi kutoka kwa mola wake na hicho ndio cheo chake

Sasa ukiona huwezi kukubali haya unapita tu haina haja ya kashfa wala matusi
 
Hiyo ni topic ya Population kama sikosei form 3 Geography. Infant mortality rate ni idadi ya vifo kugawanya kwa idadi ya vizazi hai mara 1000 kwa mwaka wa kwanza wa kuzaliwa.
IMR = (no. of deaths from live births ÷ no. of live births per population) × 1000 per year.

Mtoto akizaliwa amekufa haesabiki kwenye mortality rate, mtoto akivusha mwaka mmoja akifa ahesabiki. IMR hulenga kupima utoaji wa huduma za afya kwa watoto wakishazaliwa, akivuka mwaka mmoja probably huduma zilikuwa nzuri akifa baadae ni sababu nyingine isioambatana na huduma bora za uzazi.

OP kaleta vitu viwili tofauti, life expectancy kwenye aya ya kwanza na IMR kwenye aya ya pili akaichanganya
Mimi nilitaka jinsi life expectancy at birth inavyopatikana.
 
Back
Top Bottom