Rwanda yapitisha mpango kujenga Kinu cha Nyuklia!

Hapa kila mtu anakuja na lake, Kikwete aliacha umeme wa gas ukiwa mbioni kumalizika ukiwa umeshachukua matrilioni ya fedha za walala hoi wakiaminishwa mradi utakuwa suluhu ya matatizo ya umeme kwa zaidi ya mamia ya miaka ijayo lakini alipokuja mrithi wake akasema hapana tuwekeze kujenga bwawa maana umeme wa maji ni nafuu kuliko wa gas nae anachukua matrilioni ya fedha bila shaka ataondoka bado hatujakamilisha aje tena mwingine nae atuhamishie kwenye solar ama upepo huku wakituachia madeni makubwa nchi hii. Hivi tumerogwa sie hata tushindwe kuona na kuamua? Watawala wanapokosolewa mipango yao hii wakosoaji wao huwaona kama ni wakwamishaji na wafitini wasiolitakia taifa mema wakitumia mamlaka zao kuwashambulia wakosoaji wao na hata kuwaua lakini mwisho wa siku hawa hawa wanaosifia mipango yao leo kesho akija mwingine na mipango tofauti ndiyo hao tena wa kwanza kunanga waliotangulia. Tuna shida mahala tukubali tujirekebishe watanzania tusonge mbele badala ya kupiga mark time.
 
Tunazungumzia commercial farming, kilimo cha miaka 50 unayosema ni kilimo cha jembe la mkono ambacho zaidi ya kuzalisha kwa ajili ya kula hakuna cha zaidi, Tz ina diversity nzuri ya hali ya hewa, tuelekeze nguvu humo.
Hicho kilimo tumelima for more than 50 yrs!! Hukui kufika kwene nyuklia n far away kuliko kuhangaika na kusema kilimo.....tz cyo Somalia hatuna shida ya njaa labda useme tulime kwa ajili ya kuexport
 
Kuwa muelewa huu umeme kwa sasa sasa hata wakijitajidi sana wanazadhilisha kama MW 1000. Sasa hivi tunaelekea kuwa nchi ya uchumi wa kati. Kwa hiyo manufacturing industries zitaongezaeka. Usiseme huu umeme na vyanzo vyote unatosha. Hujui baaada ya miaka mitano mahitaji yatakuwaje. Kwa hiyo kupeleka pesa na kwenda kujenga JNHPP ni viable kwa uchumi wetu. Maana hata Sgr ikianza operations utatumika na kutakuwa na mabadiliko makubwa sana.
Ni kweli kilimo kimeajiri 70+ ya nguvu kazi lakini serikali imekipa kipa umbele. Ndio maana kuna benki ya maendeleo ya kilimo ambayo inawasaidia wakulima. Bado kuna mikakati mingi tu ambayo serikali imeifanya ili wakulima wanufaike na ndio maana unaona Tanzania ni food basket ya East Africa. Nashangaa sana Irrigation schemes kama Kapunga na zingine nyingi unajifanya huzijui wakati zinazalisha mpunga mpaka ndugu zako huko Rwanda wanaliashwa na Tanzania.
 
Acha ujinga na upuuzi wa kukariri. JNHPP inakamilika 2022. We ulitaka miradi kama ya kinyerezi ya kuzalisha MW 100 kwa phase moja. Ina maaana miaka 10 ndio mpate 1000 MW wakati JNHPP ni mradi mmoja 2100 MW kwa mkupuo.
 
jiwe dah ..na ss tujengee na kinu kimojaaa!! wapinzani tuwaweke mleeee!!
 
Mkuu hili swali unalikwepa sana

Multiplier effect ya kuongeza MW 2000 na kuwekeza 100% kwenye kilimo kinachoajiri 70% ya labor force, ipi ni viable zaidi?

Narudia tena mpaka 3rd quarter ni 15% pekee ya bajeti ya maendeleo kwa wizara za kilimo na mifugo/umwagiliaji ilipatikana. Je kwako hili ni sawa?
 
Acha ujinga na upuuzi wa kukariri. JNHPP inakamilika 2022. We ulitaka miradi kama ya kinyerezi ya kuzalisha MW 100 kwa phase moja. Ina maaana miaka 10 ndio mpate 1000 MW wakati JNHPP ni mradi mmoja 2100 MW kwa mkupuo.
Mkuu huyo jamaa kaongea kitu cha msingi sana kwamba nchi haina dira ya pamoja ila inaendeshwa kwa matakwa ya kiongozi mmoja.

Mfano tulikua na sera ya kilimo kwanza ikatupwa, imekuja Tz ya viwanda ikifika 2025 utaskia Tanzania ya utalii yaani tuna shift focus kila baada ya kubadili utawala hivi hatutofika.

Kma ni gesi basi iwe gesi sio tunaaminishwa gesi keshokutwa bwawa keshokutwa umeme wa upepo!! Hizo projecy overlaps ni kwa faida ya nani?
 
Ok fine 15% ya bajeti ya maendeleo ilipelekwa kwenye kilimo, je output iko vipi kilimo? Hatuzalishi chakula cha kutosha? Na kuhusu swali lako nimeshakujibu mradi wa JNHPP ni viable sababu nchi yetu tunaelekea kuwa nchi ya uchumi wa kati. Kwa hiyo tunahitaji umeme mwingi zaidi ya huu uliopo sasa. Maana lazima tujikite kwenye viwanda . Na hata hayo mazao tunyozalisha hapa nchini lazima yaongezewe thamani hapa nchini kwetu.
 
Asikutishe kitu kilimo kwanza ilikuwa awamu ya kwanza ya JK na awamu ya pili ilikuwa maisha bora kwa kila mtanzania. Atoe tathimini kama serikali haikuthubutu katika utekelezaji wa hizi kauli mbinu sio kulalama tu.
Na unaposema uchumi wa viwanda sio kwamba eti kilimo na biashara hauvipi kipaumbele.
 
Kwani kilimo cha kisasa ni kwa ajili ya chakula au biashara? Hvi unafahamu viwanda vikubwa hapa nchini vinaagiza sukari ya viwandani hadi ngano nje ya nchi kwa madai ya kwetu haina quality inayohitajika? Then tunaona hakuna changamoto kwenye kilimo bado?

Issue hapa ni kwamba kuliko wakulima kila mwaka walie lie mvua au watumie kilimo cha mkono kwanini msiwekeze huko wakulima wakawa na mbinu za kisasa na waweze kuzalisha kwa tija na tukauza nje ya nchi? Haya yote huyaoni ila issue ni kwamba miradi ya umeme ndio Tz ya viwanda!!

Tuna shida ya vipaumbele sana
 
Mnaposema Tz ya viwanda mna maana kuwekeza kwenye amenities zitakazovutia na kuwezesha uwekezaji iwe SGR, mabarabara, cjui Ndege, umeme n.k ambayo ni sawa ila inakera pale ambapo wabunge wakipiga kelele kuhusu wizara ya kilimo kupewa 15% pekee alafu utaskia miradi fulani inapewa pesa kwa wakati.

Siku mkiamua kuwa serious kwenye kilimo ndio tutasahau umaskini. Hta India sio kma wana manufacturing industry kubwa ila wao waliwekeza kwenye service zaidi na unaweza ona imewapandisha kiuchumi so tusikariri kuwa viwanda pekee ndio vitainua hadi uchumi wa kati.
 
Nani aliesema viwanda pekee vitainua au kuimarisha uchumi? Hadi sasa sera ya nchi ya viwanda inatekelezwa huku kilimo na biashara vinapewa kipaumbele.
 
Umeme ni kila kitu, viwanda ni moja ya sekta muhimu zinazotegemea viwanda. Serikali imeweka mazingira rafiki ili wakulima waweze kujikwamua na kufanya kilimo cha kisasa. Kama wewe unaona TADB haiwezi kuwasaidia wasingefika hapo. Wenyewe wanaona kuna hatua wanapiga.
 
Sawa Mkuu lakini pia haina maana kulima eka mia,ukapata thamani sawa na mazao ya eka kumi. Mega projects kama ya stigglers gorge itarahisisha bei ya umeme hivo akuwezeshe viwanda vingi na pia kuongeza thamani ya mazao tutayouza. Sgr tunaihitaji,kwa geografia tulipo nchi nyingi zilizoko Magharibi yetu zinategemea kupitishia mzigo yao.Hela nzuri na iliyo karibu ipo kwenye Mega projects
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…