Real Patriotist
JF-Expert Member
- Feb 6, 2016
- 296
- 697
Hapa kila mtu anakuja na lake, Kikwete aliacha umeme wa gas ukiwa mbioni kumalizika ukiwa umeshachukua matrilioni ya fedha za walala hoi wakiaminishwa mradi utakuwa suluhu ya matatizo ya umeme kwa zaidi ya mamia ya miaka ijayo lakini alipokuja mrithi wake akasema hapana tuwekeze kujenga bwawa maana umeme wa maji ni nafuu kuliko wa gas nae anachukua matrilioni ya fedha bila shaka ataondoka bado hatujakamilisha aje tena mwingine nae atuhamishie kwenye solar ama upepo huku wakituachia madeni makubwa nchi hii. Hivi tumerogwa sie hata tushindwe kuona na kuamua? Watawala wanapokosolewa mipango yao hii wakosoaji wao huwaona kama ni wakwamishaji na wafitini wasiolitakia taifa mema wakitumia mamlaka zao kuwashambulia wakosoaji wao na hata kuwaua lakini mwisho wa siku hawa hawa wanaosifia mipango yao leo kesho akija mwingine na mipango tofauti ndiyo hao tena wa kwanza kunanga waliotangulia. Tuna shida mahala tukubali tujirekebishe watanzania tusonge mbele badala ya kupiga mark time.