Wamekuambia kwamba wameuona huko Rwanda na Uganda au nao wanatumia mwandamo wa nchi zingine?!
Kama kutumia mwandamo wa nchi zingine, hata Tanzania wapo wanaosali Eid leo hii, tofauti ni kwamba BAKWATA inatumia kanuni ya kuonekana kwa mwezi locally, na hao wengine inawezekana wanatumia kanuni ya mwezi ukionekana Saudi Arabia!
Kwa taarifa yako tu, kuna makundi matatu:-
1. Kuna nchi ambazo wao lazima waone mwezi wenyewe au uonekane anywhere kwenye kanda yao
2. Kuna nchi ambazo wanaangalia endapo Saudia Arabia wametangaza mwezi kuonekana, na
3. Pia zipo nchi zinazoangalia ikiwa Turkey wametangaza kuonekana kwa mwezi
Kundi la kwanza, halitaki kubadilishwa na mabadiliko ya teknolojia, na wao wamesimamia pale pale kwamba "fungeni na fungueni kwa kuuona mwezi"
Kundi la pili, wanaendeshwa na mabadiliko ya sayansi na teknolojia kwa sababu, nchi kama Saudi Arabia, wana-spot mwezi kwa njia tatu:-
1. Kwa kuuona wenyewe kwa macho,
2. Kwa kutumia binoculars, na
3. Kwa kutumia Wanajimu!!