Sasa hayo madhehebu wameiga kutoka kwa nani?
Mapokeo, kukosa elimu na kujitambua..
Habari ni ndefu, nitajaribu kufupisha kqa kile nikijuacho, ila mola wangu ndio mjuzi zaidi.
Wakat mtume (saw) anakaribia kufa, alisema ameikamilisah dini(uislam) maana yake mafunzo kamili, jinsi ya kula, kulala, kuswali, kufanya biashara, kuoa, usafi, masuala ya kiuchumi, mikopo, historia, elimu n.k n.k yaani kila jambo unaloliongelea wewe uislam umetia neno lake..
Baada ya kifo cha mtume ikabdi apatikane kiongozi wa kuongoza hapa ndio mifarakano ikaanzia..
Wa kwanza akawa abubaqar swadiq(r.a) ambae ndio alikuwa swahiba wa mwanzoni wa mtume, moja kati ya watu walikuwa wakimuani mtume mnoo.. Akisikia hili kasema mtume yeye hapingi, hata safar ya miiraji, alipofikishiwa taarifa na abuu jahal, kwamba swahiba wako kapata uchizi, kasema ndani ya usiku wa jana kasafiri mpaka masjid al aqsa.. Yeye akajibu kama kasema hivyo basi ni sahihi.
Kisha akaja umary(r.a)
Kisha uthman bin affan(r.a)
Kisha Ali (R.A)
Suni hawana tabu na huo mtiririko, kuna baadhi ya hadithi pia zinaomesha hata yeye sayidina ali hakuwa na tabu na hao wawili wa mwanzo..
SHIA kama shia hawawataki woote hao wa mwanzo wanadai baada ya mtume kiongozi aliyepaswa kufwatwa ni sayidna alii..
Hapo ndipo waislam walipogawana makaburi..