S.H Amon apoteza jengo la ghorofa nane Kariakoo

S.H Amon apoteza jengo la ghorofa nane Kariakoo

Aombe mapitio ili mahakama iamuru waliokuwa wamiliki wa awali ambao wamerudishiwa umiliki wao wamlipe gharama za jengo au aruhusiwe kulivunja jengo lake ili wao wabaki na kiwanja chao.
Wamlipe vipi wakati kanunua eneo kimakosa na kawasababishia maisha ya tabu na mateso kwa kipindi cha miaka 20 (na wao wataomba fidia ya hasara waliyopata tangu kiwanja chao na nyumba yao kuvunjwa)
 
Milioni 105 angeweza kupata kiwanja njia ya Tegeta na kujenga kwa nafasi, mji unapanuka. Pole zake.
Kariakoo wakinga,waha n.k wamedhulumu sana nyumba za watu kimtindo huo, wanaingia mkataba na familia halafu mkataba ukibaki miaka kadhaa anakiuka baadhi ya vipengele vya mkataba kwa maksudi,wanafamilia mkienda mahakamani ndio imekula kwenu hiyo,kama mkataba ulibaki miaka 4 mchukue chenu basi kesi itaendeshwa hata miaka 10 na zaidi huku jamaa akiendelea kufanya biashara eneo lenu na nyie hata 100 ampati,hapo huyo amon asharudisha hela yake na faida kibao
 
Hivi kwa mfano akiamua kubomoa ghorofa lake anaruhusiwa ? Maana si ni mali yake, kama tu vyombo vya ndani ?
 
Mungu ni mwema sana.
Hivi ndivyo haki inavyokua haipotea, ingawa inaweza tu ikacheleweshwa.
Miaka kuanzia ya 2014 kurudi nyumba, wafanya biashara/wanasiasa walionekana kua wenye mguvu kuliko hata serikali, na hii ndio matokeo ya sheria zilizo pindishwa na wenye fedha/mamlaka enzi hizo
Mkuu nimerudiarudia kusoma kisa hiki naona kama kuna hila na udhulmati kwa wana familia warithi.

Kwa sababu, mbona sioni popote katika majumuisho ya majaji katika hukumu hiyo wakitaja namna gani wana familia hao walinufaika kwa kuiuza hiyo nyumba yao ya urithi kwa mtu mwingine na kuja kugeuka kutotambua zoezi lao hilo zima la uuzaji wa nyumba hiyo kwenye mnada wa hadhara!
 
... benki hawawezi kuendesha mnada bila idhini ya mahakama nadhani. Lazima shauri lipelekewe mahakamani kwamba umeshindwa kulipa mkopo wao kwa mujibu wa mkataba (umekiuka mkataba) then mahakama itatoa hukumu ya nyumba yako kuuzwa. So, mnunuzi atakuwa ameinunua kwa utaratibu sahihi kuja kumgeuka itakuwa ngumu sana.
Kuna kipindi kulikuwa na figisu figusu za watu kukopa hela kwa hati zisizozao yaani dudus ndio mkopaji lakini hati inapelekwa ya kwangu kama mkopaji na kwa vigezo vya bank unakuta sina hata shughuli ya kueleweka ambayo inaonyesha mzunguuko wa fedha. Nyumba inauzwa na mahakama, anaibuka mke kusema hakushirikishwa wakati mumewe akikopa na hajaona chochote kuhusu huo mkopo
 
Mmoja ana jengo mwingine ana uwanja wakae tu chini waungane wafanye business plan jinsi ya kugawana mapato
Bahati mbaya kiwanja ndicho kinaitambulisha nyumba hivyo mwenye kiwanja akisharejeshewa vyote vilivyomo ni vyake japokuwa kiuhalisia sio vyake, mfano tuache isssue ya hilo ghorofa, nije nimwage mchanga, kokoto na matofari kwenye kiwanja chako yaani hapo moja kwa moja hivyo vitu vinakuwa vyako
 
kwa maoni yangu hii hasara inapaswa ilipwe na Serikali

S.H.Amon alinunua Nyumba iliyouzwa kwa Amri ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu

kama Raia mwema hanna sababu ya kutia wasiwasi nyumba iliyouzwa kwa amri ya Mahakama …haikuwa amri ya Bank so kama upotoshaji basi mahakama ya Kisutu ndio ilipotosha na hasara lazima iibebe
 
Niliwahi kuonana na mmoja wa wanafamilia ambaye ni msimamizi wa mirathi, mawakili wa sh.Amon walikuwa wakimweleza ukweli hana haki lakini alikuwa anawaambia mbele ya pesa kuna haki? Alikuwa akihonga kuchelewesha kesi lakini hawakukata tamaa hatimaye haki imepatikana.
 
Inawezekana ndugu wenyewe walusuka hilo dili

Tatizo la ngozi nyeusi akipata pesa hudharau wasomi kisa tu wasomi pesa hawana kama wao!! Wakati wanajua vitu kibao zikiwemo.vya kisheria
Hupo sahihi huyu mzee namfahamu vizuri sana na nimeshafanya naye kazi, KWANZA,hataki ushauri na ana dharau sana alafu ni mtu wa dhuruma sana.
 
kwa maoni yangu hii hasara inapaswa ilipwe na Serikali

S.H.Amon alinunua Nyumba iliyouzwa kwa Amri ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu

kama Raia mwema hanna sababu ya kutia wasiwasi nyumba iliyouzwa kwa amri ya Mahakama …haikuwa amri ya Bank so kama upotoshaji basi mahakama ya Kisutu ndio ilipotosha na hasara lazima iibebe
Bank watamlipa fidia akifungua shauri.
Mahakama na serikali havihusiani na mahakama ya kisutu Haina amri ya mwisho.
 
Unaweka pingamizi taratibu za mnada zinaendelea, nusura nipoteze nyumba, hakimu anawaambia madalali ni busara kusitisha mnada
 
Nani kakwambia jamaa akiamua anaweza akavunja akachukua material zake za ujenzi usikariri akabaki kumuachia jamaa kiwanja chake
The Court of Appeal said in its recent decision that Amon bought the house while aware that the property was until then jointly owned by Tatu and her relatives.

“The second respondent (Amon) having purchased the property without prior inquiry into the extent of the title of the judgment debtor (Tatu) on the suit property, cannot qualify as a bonafide.

“This is because in the circumstances of this case, any reasonable man would have expected the second respondent to (S.H. Amon Enterprises), before purchasing the suit property, inquire and find out in the relevant authorities what interests, if any, the said fourth respondent (Tatu)’s relatives had in the suit property.

“Her unreasonable omission to make an inquiry, put her to constructive notice or imputed notice of the appellant’s ownership interests on the suit property.
The court rejected Mr Amon’s complaint that he has invested huge amount of money on the property unworthy of being considered.

“Since it is clear from the record that she had been aware of the dispute on the property right from the beginning, whatever investment she injected on the suit property, was at her own risk,” said Judges Mwanaisha Kwariko, Issa Maige and Abraham Mwampashi.

They went on: “We cannot order demolition of the of the current buildings n the suit property as we see nothing wrong with the building itself. In any event, such order will not benefit either of the parties and it will have adverse effects to the national economy".
 
The Court of Appeal said in its recent decision that Amon bought the house while aware that the property was until then jointly owned by Tatu and her relatives.

“The second respondent (Amon) having purchased the property without prior inquiry into the extent of the title of the judgment debtor (Tatu) on the suit property, cannot qualify as a bonafide.

“This is because in the circumstances of this case, any reasonable man would have expected the second respondent to (S.H. Amon Enterprises), before purchasing the suit property, inquire and find out in the relevant authorities what interests, if any, the said fourth respondent (Tatu)’s relatives had in the suit property.

“Her unreasonable omission to make an inquiry, put her to constructive notice or imputed notice of the appellant’s ownership interests on the suit property.
The court rejected Mr Amon’s complaint that he has invested huge amount of money on the property unworthy of being considered.

“Since it is clear from the record that she had been aware of the dispute on the property right from the beginning, whatever investment she injected on the suit property, was at her own risk,” said Judges Mwanaisha Kwariko, Issa Maige and Abraham Mwampashi.

They went on: “We cannot order demolition of the of the current buildings n the suit property as we see nothing wrong with the building itself. In any event, such order will not benefit either of the parties and it will have adverse effects to the national economy".
Sheria ni msala...
 
Huyu h Amon ndio h maana aliuza nyumba pale sinza d kijiweni kwa mama bite muuza gogo karibu na havad hotel
 
Mbunge wa zamani wa Rungwe, Sauli Henry Amon amepoteza jengo la ghorofa nane lililoko Kariakoo jijini hapa, baada ya Mahakama ya Rufani kueleza kuwa nyumba hiyo ilijengwa kwenye kiwanja kilichouzwa kwa mnada isivyo halali.

Uamuzi huo umeirejeshea furaha na kuipa utajiri wa ghafla familia ya Bushiri Pazi, iliyopambana kwa zaidi ya miaka 20 katika mahakama mbalimbali kupigania kile ilichoamini ilikuwa haki yake.

Jengo hilo ni nyumba namba 113, kitalu namba 4 block namba 17, lenye ghorofa nane lililopo Kariakoo, Wilaya ya Ilala.

Amon, aliyekuwa mbunge kupitia CCM mwaka 2015 -2020 anayejulikana zaidi kwa jina la biashara la S.H. Amon, anamiliki kampuni ya S.H. Amon Enterprises Co. Ltd yenye maduka ya vipodozi jijini Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza, Arusha na Mbeya.

Amon aliinunua nyumba hiyo ya kawaida kwenye mnada Mei 13, 2001 kwa Sh105 milioni kupitia Kampuni ya S.H. Amon Enterprises Co. Ltd na kupewa hati namba 57275 iliyotolewa Machi 24, 2005, kwa jina la kampuni hiyo, kabla ya kuibomoa na kuporomosha ghorofa hilo.

Asili ya mgogoro

Awali kiwanja hicho kilikuwa na nyumba ya udongo ambayo iliuzwa baada ya familia ya watoto sita ya marehemu Pazi kupata fursa wakaingia ubia na mwekezaji (hakutajwa) aliyeivunja na kujenga nyumba nyingine ya kisasa kwa makubaliano ya kibiashara.

Mmoja wa wanafamilia katika nyumba ya udongo iliyovunjwa, Tatu Pazi, alikuwa anamiliki chumba kimoja alichompangisha mtu aliyetajwa kama Musa Hamisi Kazuba.

Lakini baada ya nyumba hiyo kujengwa upya, mahali ambapo palikuwa na chumba alipopanga Kazuba kwa ajili ya biashara pakageuka na kuwa njia.

Mgogoro ulianzia hapo baada ya Kazuba kung’ang’ania apewe eneo ambako chumba chake kilikuwa ili aendelee na biashara yake ya duka.Baada ya kukosekana maelewano, Kazuba alifungua shauri katika Baraza la ardhi la mkoa akidai Tatu amekiuka makubaliano.

Mdai alitaka baraza hilo liamuru arejeshewe kodi ya Sh1.8 milioni aliyokwishatoa pamoja na riba.

Kazuba pia, alitaka alipwe Sh900,000 kila mwezi kuanzia mwaka 1999 mpaka siku watakapokamilisha malipo hayo.

Baraza hilo lilimwamuru Tatu kumlipa mpangaji wake huyo riba ya Sh15 milioni zikiwa sehemu ya Sh1.8 milioni alizokuwa amelipa kodi ya pango baada ya kukubaliana na madai ya Kazuba.

Tatu hakukubaliana na uamuzi huo, aliamua kufungua shauri katika Baraza la ardhi la taifa. Hata hivyo, alishindwa baada ya Baraza hilo kuridhia uamuzi wa Baraza la mkoa.

Baada ya kuona amepata ushindi katika mabaraza yote, Kazuba alikwenda katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kukazia utekelezaji wa hukumu.

Wakati Kazuba akifanya hayo, wanafamilia ambao hawakuwa sehemu ya mgogogo kati ya Tatu na Kazuba, ambao nao walikuwa wamiliki, waliibuka na kudai hawakuwa wakijua kilichokuwa kinaendelea mahakamani.

Walikwenda Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kutambua uwepo wa mgogoro huo na kuweka mapingamizi kadhaa wakipigania haki yao.

Mnada kabla ya hukumu

Wakati mapingamizi hayo yako mahakamani, ushahidi unaonyesha kuwa madalali wa mahakama walianza kutangaza kupiga mnada nyumba hiyo siku kadhaa kabla hata ya uamuzi wa maombi ya Kazuba ya kutekeleza hukumu kuamuliwa.

Baadaye Mahakama ya Kisutu iliamuru nyumba hiyo ipigwe mnada na kutupilia mbali mapingamizi yaliyowekwa na wanafamilia wengine.

Hapo ndipo nyumba iliuzwa kwa S.H Amon ambaye aliibomoa na kujenga jengo jipya la ghorofa nane.

Kufuatia uamuzi huo, mwaka 2004 wanafamilia watano wa mzee Pazi walifungua kesi Mahakama Kuu (Divisheni ya Ardhi) kupinga nyumba yao kuuzwa.

Waliiomba Mahakama itamke kuwa wao ndio wamiliki halali wa kiwanja hicho na nyumba iliyokuwemo.

Waliitaka itamke pia kuwa amri ya wao kukamatwa, nyumba yao kuuzwa, wao kuondolewa na kubomolewa haikuwa halali na ilitokana na udanganyifu mkubwa.

Wagonga mwamba

Baada ya kusikiliza shauri lao hatimaye Machi 9, 2012 Jaji Kakusulo Sambo alitupilia mbali maombi hayo na kutamka kuwa S.H. Amon Enterprises Co. Ltd ndiye mmiliki halali wa jengo hilo na maendeleo yote yaliyokuwa yamefanyika.

Ilisema kuwa wadai hao hawakuwa na haki ya kuchukua mali ya mtu mwingine bila ridhaa yake.

Uamuzi huo haukuwakatisha tamaa. Kupitia wakili wao, Melchisdeck Lutema walikimbilia Mahakama ya Rufani kupinga uamuzi huo mwaka 2019.

Waliokata rufaa hiyo ni Hamis Bushiri Pazi akiwa msimamizi wa mirathi na dada zake wawili, Stumai na Hatujuani pamoja na dada zake wengine wawili ambao ni marehemu, Neema na Mwajuma.

Wajibu rufani walikuwa ni S.H. Amon mwenyewe, S.H. Amon Enterprises Co. Ltd, Musa Hamisi Kazuba na Kassim Ally Omar kama msimamizi wa mirathi ya dada yake, Tatu ambaye pia ni marehemu.

Rufaa hiyo ilisikilizwa na jopo la majaji watatu, Mwanaisha Kwariko, Issa Maige na Abraham Mwampashi Aprili 13, mwaka huu.

Majaji hao walikubaliana na hoja za rufaa na kubatilisha umiliki wa eneo hilo pamoja na uwekezaji wote uliofanywa na S.H. Amon katika kiwanja hicho na kuimilikisha familia hiyo.

Majaji hao walisema ni jambo lisilobishaniwa kuwa eneo hilo na nyumba iliyokuwemo ilikuwa ikimilikiwa kwa ubia na wanafamilia sita, akiwamo mjibu rufaa wa nne (Tatu), akimiliki hisa moja kati ya saba (1/7).

Hivyo ikaona kuwa kuuzwa na kuhamishia umiliki wa nyumba hiyo kwa Kampuni ya S.H. Amon Enterprises Co. Ltd haikuwa halali na jambo lisilowezekana wakati kumbukumbu zinaonyesha S.H Amona alinunua nyumba hiyo akijua kuwa inamilikiwa na familia.

Wakaendelea kueleza kuwa kitendo cha kampuni hiyo kununua nyumba hiyo bila kutafuta na kufahamu kiwango cha umiliki wa mwanafamilia kumemfanya asiwe mnunuzi halali.

“Hii ni kwa sababu kwa mtu mwenye ufahamu katika mazingira ya kesi hii ingetegemewa kuwa kabla ya kununua mali hiyo, mjibu rufaa wa pili, S.H. Amon Enterprises alipaswa kwanza kuuliza katika mamlaka husika kuhusu kiwango cha umiliki wa (Tatu) mjibu rufani wa nne.

Mahakama hiyo imesema kwa kuwa uuzwaji wa nyumba hiyo haukuwa halali kwa upande wa wamiliki wengine waliokuwa wakimiliki hisa sita (6/7), inakubaliana na warufani kuwa Mahakama Kuu ilikosea kuamuru kuwa kampuni hiyo ilikuwa mmiliki halali na hasara inakuwa ya S.H. Amon.

Akizungumza kwa simu na gazeti hili, Amon ameeleza kushangazwa na uamuzi wa kulimilikisha jengo lake katika familia ya Pazi bila kujali uwekezaji alioufanya.

Source : Gazeti la Mwananchi
Jamani mambo ya ardhi hasa mijini ni shida sana
 
Back
Top Bottom