Saalah (Silent Ocean): Anavyotakatisha na kutorosha pesa nchini, Uhujumu Uchumi, Kuteka na Kutesa watu, anavyolindwa na viongozi

Ninapodili na wewe na kukuamini inakubidi uwe makini sanaa la sivyo itakugharimu, natoa pesa zangu nyingi kuwekeza kwenye biashara yako na unapoteza umakini na ushahuri nakupa bure na unashindwa kuufanyia kazi narudia tena itakugharimu

Kila mtu mzuri ana ubaya wake hakuna mzuri wa 1 Kwa 1

Katika kesi ya hao jamaa hakuna la kumsaidia yeyote hapo kwani ni ndani na nje ya makubaliano ya biashara yao wenyewe ukiweka wazi juu ya uzembe wa jamaa aliyewekezewa pesa kwenye biashara yake na akaleta mzaha wa kumuamini kijana mwenzake kupelekea kupoteza kila kitu

Kikubwa, awe makini anapoinuka tena au anapoaminiwa na mtu mwingine kwa kuwekeza pesa kwako aongeze umakini zaidi asirudie kosa, na sikuona sababu yeyote ya kukubali kupewa au kukopeshwa pesa na huyo jamaa angeendelea na kazi yake ile ile ya MARKETING na ukusanyaji wa pesa ilikuwa inamtosha sana

Kuhusu jamaa kuchunguzwa na serikali ni jambo muhimu ila sio lenye manufaa sana WAFANYABIASHARA wana mambo mengi sana katika biashara zao haswa hao wafanyabiashara wakubwa

Kukwepa kodi kama sio kukimbia kabsa,hiyo kusafirisha pesa, kuexchange pesa ,kudhulumu na kudhulumiana kuhusu umafia kwa wenye pesa ni kawaida sanaa

Lazima ujilinde kana kwamba mtu asikuzoee zoee kwenye mambo yako yaani mtu asiingilie plan zako akaziharibu ikitokea mtu anataka kuingilia mipango yako na kuiharibu unatakiwa umpotezee mbali sana asionekane hata dalili ikitokea watataka kumtafuta

Kuna vijana sita walipotea kariakoo wauza simu mwaka juzi kama nna kumbu kumbu vizuri na mpaka sasa hakuna taarifa ya kupatikana na vyombo vilitangaza Kama walikamatwa na police na walipelekwa mpaka kituoni na mpaka sasa hakuna taarifa yeyote kuhusu wao, so ni mambo hayo hayo tu ya kudhulumiana na kupotezana

Be careful unapodili na mtu anayejiweza yaani wanakuwa mahesabu yao kupata na sio kupoteza hasara inaweza ikawa ya kibinaadamu lakini yeye akaona kama umeisababisha kwa makusudi - kama Tajiri umekutana nae tu juu kwa juu na akataka mfanye biashara inabidi uwe makini sana ila kama unafahamiana siku nyingi mnaweza mkafanya kitu na kikaenda vizuri

Asantum
 
Saalah anasema IGP Wambura ni mshikaji wake wa Pete na kidole.
 
Ila pia sisi Waafrika tujifunze uaminifu mzizi wa huu ugomvi uko kwa huyu kijana Pius.Haikuwa vizuri kumwibia Eliud na pia kwa Salah ni vyema ukafanya haki kumpa Eliud anachostahili maana ni haki yake chukka chako mrudishie chake
 
Masikitiko hatunae jpm. Wale hawakuelewa aliposema utawala wake tajiri anaweza kufanywa lolote ni matajiri kama huyu salaah. Chini ya samia hawa wanaweza mfafanya raia yoyote wa kawaida lolote.
Tuombe mungu utawala huu uweze kumkomesha salaah.
Inawezekana nae JPM alishirukiana na Boss Salah kuficha zile pesa za pre bargain CHINA
 
Masikitiko hatunae jpm. Wale hawakuelewa aliposema utawala wake tajiri anaweza kufanywa lolote ni matajiri kama huyu salaah. Chini ya samia hawa wanaweza mfafanya raia yoyote wa kawaida lolote.
Tuombe mungu utawala huu uweze kumkomesha salaah.
Hizi tuhuma zote cyprian musiba alishazisema kwa utofauti kipindi cha magufuli na hawakufanywa chochote tatizo lenu watanzania ni wasahaulifu
 
Afanse umeamua kujilipua ovaa Mungu akulinde 🙏eliud alikuwa mzembe kujigeuza mhasibu kisa aliwah fanya kazi ya uwakala wapesa😅akajiona mhasibu mbobezi😅na akamwamini maamuna mwenzie Pius kudeal na pesa mingi hivyo,bado elimu Ina nafasi yake wandugu angeajiri professional accountant yasingetokea haya,hapo ndo mzungu anatupiga gap,ila Salah anafanya kazi ya uhujumu uchumi na mamlaka husika zinajua,hata maza anajua,na kama alivyosema hakuna wa kumfanya lolote🙏hii ndo Tanzania tuijuayo,isitoshe jamaa anamiliki silaha ya Moto isivyo halali manake hayuko kwenye records za wamiliki silaha kama alivyosema😅yawezekana alitambua gap la umaamuna wa eliud na akamtumia Pius kupiga hizo hela,afande kuwa makini watakuwinda manake wanamkono mrefu hao,watch your back dude,hata mkuu wako Yuko kwenye payroll yao usiahangae,mi5 Tena kwa mama akeee😅😅🙅🏃
 
Ila pia sisi Waafrika tujifunze uaminifu mzizi wa huu ugomvi uko kwa huyu kijana Pius.Haikuwa vizuri kumwibia Eliud na pia kwa Salah ni vyema ukafanya haki kumpa Eliud anachostahili maana ni haki yake chukka chako mrudishie chake
Ni sahihi kabisa. Pia Salaah angekuwa na utu angethamini kazi ya Eliud na angempa muda wa kuendelea kufanya kazi kumlipa hasara na sio kutaifisha mali zake na kumuacha hana pa kushika.

Ni kweli vijana wa Kitanzania tuwe waaminifu. Mtu akikuamini aminika sio kumuingiza matatizoni.


Naamini hata hizo biashara alizofungua na baba yake mdogo zitakufa maana kuna mtu ananung'unika.
 
Cha kufanya mngeenda kwa mzee Yusuf Makamba nadhani atawasaidia ikiwa atakubali

Mzee Yusuf Makamba ni miongoni katika waTanzania wachache wenye nguvu sana ndani ya CCM na nchi hii kiujumla na kama unabisha ungeweza kumuuliza Hayati JPM angekuambia
Ndio sema naye mtu wao si unaona aliwauzia kiwanja Cha CCM ambacho technically ni kiwanja Cha serikali,manake viwanja vya Tanu then CCM ni Mali ya serikali,vilitolewa buree enzi hizo 🙏
 
Nipe taarifa za hiyo silent ocean, niishugulikie kama serikali inaogopa. Lakini kabla ya kuisafisha hii takataka lazima nifanye uchunguzi wa haya maneno kama ni kweli au laa, mana nisije nikaimaliza silent ya watu kumbe ninyi ndo chanzo Cha matatizo haya.
 
Unajua Payroll?
 
😳😳😳😲😲😠😠😡OOOVaaaaaaaa.....!! Ni muda sasa wakusubili ili tujue hii serikali yetu ni ya aina gani🤔🤔 Au mkuu usikute kesi ya ngedere ndio tunaitupa kwa nyani.
Naamini hapa ndio tutaona vyongozi wetu walivyo waajabu na ovyo!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…