Sababu (10) tata za kisheria uuzwaji wa Bandari ya Tanganyika

Nimekuelewa sana mtoa mada ingawa mimi sio Mwana Sheria.

Kwa upande wa Tanganyika, mkataba umesainiwa na Raisi wa Nchi au kwa niaba ya Raisi wa nchi mwenye nguvu ya kisheria na imetaja cheo chake Rais.

Ili kubalance ilitakiwa na wenye mkataba asaini pia Raisi wa nchi ya UAE na mkataba utaje cheo chake.

Hapa ni sawa na Nchi inaingia mkataba na msela mmoja wa mtaani wa nchi nyingine, huku mwenye nchi ile hana habari.

Yaani nchi ya Tanganyika inauza raslimali zake kwa raia wa nchi nyingine bila ridhaa ya mwenye nchi hiyo.

Safi sana mto mada tunasubiri KASORO ya pili.
Mwarabu safari hii haji kwa huu ujanja ujanja tutagawana fito.
Hapa mpaka kieleweke.
 
Asante kwa kumuelewa
 
Mbunge wa mtera atajuaje Sasa haya yote? Any way thanks in advance
ah ah.. you have made my day kwa kicheko, yaani nimecheka sana, huyu kibajaji ni think tank wa ccm, na ndio maana hii nchi inarudi backward kwa kuongozwa na wajinga.

Simpendi km nini huyo fupi nyundo
 
We nae ni mpotoshaji tu, kichwa cha habari tu kina utata, ni uuzwaji au ukodishwaji??? Mda wote tumuogope Mungu jmn
hakuna kitu nilichoandika kwa utpotoshaji au kwa bahati mbaya, ulipashwa kuuliza je bandari imeuzwa au imekodishwa?

document inayotembea mtaani ni mkataba, kisheria tunaita ( a contract is a legal document), yaani ni nyaraka ya kisheria, hivyo basi tafsiri uliyonayo wewe ni mkataba, lakini kwa mwanasheria ni nyaraka ya kisheria (legal document) kwa interpretation ya vitu unavyoviona wewe kwenye makaratasi na mwana sheria ni vitu viwili tofauti, ukisoma wewe utaona gazeti lakini kwa mwanasheria anatoa tafsiri ya kisheria,

kwa nini nimetumia neno kuuzwa?
nimetumia neno kuuzwa sababu, nikisoma kama mwana sheria kuna ardhi (land) bandarini ambayo ndio subject matter ya kwanza, hivyo utoaji wa ardhi kwa unayoitetea tunaiita (lease) yaani kupangisha au kukodisha. in order to lease one must comply na condition za ownership, ( tafuta mwanasheria akusaidie, what is a condition of sine quo none ya leasing as opposed to ownership)

kwangu, kwa tafsiri yangu ya sheria bandari imeuzwa, kama umekodishwa nipe ushaidi wa kisheria na mimi nijifunze
 
Kudadeki
 
Kuna shida gani ya kuonesha kifungu kilichouza Bandari? Mbona maneno mengi sana we mtu?
 
Kuna shida gani ya kuonesha kifungu kilichouza Bandari? Mbona maneno mengi sana we mtu?
wewe umejiandika lord denning, nadhani humjui hata Lord denning ni nani, tafuta hata mtoto aliyesoma certificate ya sheria akuambie lord denning ni nani?

kwa muktadha wa Lord Denning ndio maana nimekuandikia rejea usome, na kama unataka zaidi ya hapo basi siwezi
 
Kiuhalisia Sisi sote wenye vipande vya ardhi kt hii nchi kisheria ni kuwa tumekodi kwa miaka mu5, 33, 66 mpaka 99 ambazo zinakua subject to renewal, km kweli ni kuuza basi this is extraordinary
 
Kiuhalisia Sisi sote wenye vipande vya ardhi kt hii nchi kisheria ni kuwa tumekodi kwa miaka mu5, 33, 66 mpaka 99 ambazo zinakua subject to renewal, km kweli ni kuuza basi this is extraordinary
Mkataba unasema Mwarabu wa Dubai amekodishiwa bandari yetu milele, na hatutakiwa kugeuzwa chochote kwenye huo ukodishwaji milele. Hapo unailewa nini?
 
Ukiangalia kwa mbali Bungeni utawaona watu machahari sana wenye nia ya dhati na Nchi yao., ila ukisogea kwa karibu daaaah ha ha haaaaa utagundua wenye akili ya kufanya upembuzi yakinifu ni 10% waliobaki nikugonga Meza tu.
 
Aibu kubwa sana kwa Taifa letu, Rais amedhalilishwa. Urais umedhalilishwa, Taifa limedhalilishwa. Sijui walipewa kilevi gani?
 
Ukiangalia kwa mbali Bungeni utawaona watu machahari sana wenye nia ya dhati na Nchi yao., ila ukisogea kwa karibu daaaah ha ha haaaaa utagundua wenye akili ya kufanya upembuzi yakinifu ni 10% waliobaki nikugonga Meza tu.
Hawa wabunge wote, asirudi hata mmoja bungeni katika uchaguzi ujao 2025. Hilo linawezekana. Kama iliwezekana kuwaweka, inawezekana kuwatoa.
 
Kama hizo sababu 9 zilizobaki unazieleza kama ulivyoeleza hii, bora usiendelee tu. Umeandika utumbo tu mwingi saaaaana. Kwa kifupi hii sababu so far haina shida yoyote wala haibatilishi chochote. Na cha kukuongezea tu, huyo Mwanasosholojia Ahmed Mahbob Musabih amesaini mikataba mingi sana ya namna tena na nchi zenye akili kuliko hizi zilizojaa utapiamlo. Ni mmoja watendaji anaeheshimika na kukubalika sana katika anga za bandari na forodha huko kwao.
 
hakuna kiongozi yeyote wa wa United Arab Emirate au Dubai Emirate aliyetajwa kwa jina ameweka comitment katika power of attorney ile, ni uhuni tu

Wasio kuelewa naambatanisha ushahidi wa hoja yako.

Kimsingi Viongozi wa DPW wametumia Serikali yao kuupa nguvu ya Kimaifa Mkataba wa Maelewano (MoU) kati yao na TPA uliosainiwa tarehe 28/2/2022, kupitia Mkataba wa Ushirikiano (IGA) usio na ridhaa ya Viongozi wa Dubai na Falme za Kiarabu (UAE). Ni utapeli mtupu wenye harufu ya ufisadi wa kimataifa.

Inasikitisha Bunge lenye Wanasheria nguri, Madkatari wa Falsafa (PhD) na Maprofesa wameridhia kwa mbwembwe. AIBU
View attachment 2658255
 

Attachments

  • Screenshot_20230615_074641_Drive.jpg
    41.7 KB · Views: 4
  • Screenshot_20230615_074703_Drive.jpg
    39.3 KB · Views: 4
Nipe kifungu kinachoeleza bandari imeuzwa?
Sakata la Bandari limekuja kubainisha kuwa elimu yetu hasa ya juu inahitaji reform kubwa. Watu wanaongea kwa hisia tu. Ukimuuliza anaanza kurukaruka kama sungura. Watu na PhDs zao hawaelewi kilichopelekwa Bungeni ni nini na hata aina ya uwekezaji unaotarajiwa ni upi? Wanapiga kelele za kuuzwa tu, ukiwauliza tumeuzwaje, anakupa vitabu usome! Achana nao hawa wala maharage.
 
Mm nashangaa sana Hv ni kweli usalama wetu utakuwa rehani na je vyombo vinavyolinda usalama wa nchi vinasemaje hasa kwenye mazingira hatarishi ya nchi kama haya,je ni kweli vyombo Hv vya ulinzi na usalama vinasuburi tatizo litokee kwanza ndio viweze kureact na je ni halali Raisi kuachiwa kiasi hiki hata asielekezwe kwamba kuuza mpaka wa nchi ni hatari kwa usalama wa Taifa,faida tunayoitafuta ni ndogo sana kuliko hatari inayokuja.
 
Kwa hiyo hutaki kusoma?sasa ww si wa kuongea na wasomi hapa kwenye great thinkers kaa kimya maana huelewi chochote anayekwambia soma si ndio anataka uelewe na usibwabwaje hapa ila uongee kwa facts sasa hapo mla maharage na punguani ni nani? Wabunge wako wa CCM ni wavivu kama ww unayeogopa kusoma ila unaweza kusaini vitu hovyo hovyo.Elimu yetu ina shida kubwa sana na ww umedhihirisha hilo.hutaki kusoma??hahaaaaaa Taifa gumu sana hili la mambumbumbu.Ushauri ninaokupa ni kwamba usiendelee kuchangia hapa ww ni mdogo sana.
 
hata kama nitafanyaje zaidi ya 2025 kumpigia mgombea wa chadema japo bado haitasaidia kitu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…