Sababu (10) tata za kisheria uuzwaji wa Bandari ya Tanganyika

Sababu (10) tata za kisheria uuzwaji wa Bandari ya Tanganyika

UTANGULIZI:

Bila kugusia maudhuni yalivyoandikwa, au kukosoa kilichoandikwa, nimeandaa sababu 10 tata za kisheria ambazo zinatambainisha kwa nini mkataba wa uuzaji wa Bandari ya Tanganyika ni batili na ni wa aibu kwa nchi ambayo inawasomi wengi wa sheria;

Katika sheria za kimataifa za uwekezaji (international investment law), wawekezaji wanaokwenda kuwekeza nchi za kigeni (foreign investors), wanapashwa kulindwa na sheria za kimataifa, aidha baina ya nchi na nchi, yaani,(bilateral investment treat) kwa kifupi (BIT) au mjumuisho wa nchi mbalimbali (Multilateral investment treat) kwa kifupi inaitwa (MIT)., au baina ya nchi na mwekezaji, kwa hiyo basi endapo nchi hizo hazina, zinaweza kukubaliana kutengeza mkataba huo. kama walivyofanya JMT na Emirate of Dubai, ndio huu kwa sasa tunauita mkataba wa awali; ambao unanipeleka kwenye sababu yangu ya kwanza;

1. instrument used to endorse the document, (power of attorney), kwa Kiswahili ( Nguvu ya kisheria)

mkataba wa nchi na nchi ( a contractus cum states), utahesabika kuwa umeridhiwa na nchi hizo endopo, watia saini ni viongozi waliotajwa katika ibara ya 7(2) (a) ya sheria za Mikataba ya Kimataifa ( Vienna Convention on the Law of Treaties, 1969) inataja wakuu wa nchi, wakuu wa serikali, au mawaziri wa nchi za nje ( foreign affairs), 7 (2) (b), inawataja mabalozi wawakilishi wa nchi zao, 7(2) (c) wawakilishi wa nchi wa taasisi za kimataifa.

Kinyume na ibara ya 7 (2) ya sheria za mikataba za kimataifa (Vienna Convention on the Law of Treaties), ibara 7 (1) ya sheria hizo, inatoa nafasi kwa waliopewa nguvu ya kisheria wanaweza pia kusaini mikataba baini ya nchi zao na nchi zingine.


(a) Nguvu ya kisheria ni nini? ( what is power of attorney), (full power) (instrument)
(is document that gives power to another person, to perfom duties on his/her behalf that other person would have done ), yaani ni nyaraka inayotoa uwezo, nguvu, mamlaka, kwa niaba ya mtoaji uwezo huo, kufanya kazi ambayo mtu anayeitoa nangeweza kuifanya.

watiaji saini, wa mkabata wa uuzwaji wa bandari ya Tanganyika, wanaangukia Ibara ya 7 (1) ya sheria za mikataba ya kimataifa, ( the vienne Convention, on the law of treaties, 1969), kwa maana nyingine wanatakiwa waonyeshe nani kawapa nguvu ya kisheria (power of attorneys, or full power), kuziwakilisha nchi zao, ili kukidhi takwa kuonyesha wazi kuwa nchi ndio imetoa ridhaa, (consent) kuruhusu wao wasaini mkataba/mikataba huo/hiyo.

(b)characterization of the power of attorneys, full power: (mchanganua wa nguvu ya kisheria)

nguvu ya kisheria (power of attorneys) ina sehemu kuu mbili; yaani ni lazima pawepo na mtoaji, au kisheria tunamwita (Donor ,or the giver) na sehemu ya pili, lazima pawepo na mpokeaji, yaani ( Donee, or the recepient). hawa lazima wawepo kwa majina na vyeo vyao. au ni lazima waeleze uhusiano wao na document wanayotoa nguvu ya kisheria kwa mtu mwingine.

(c) utata:

Upande wa Tanzania;

Ukisoma nyaraka zinazotembea na ambazo hazijakanushwa kuwa ni feki, utaona pasipo shaka kuwa, nguvu za kisheria, kwa upande wa JMT zimekidhi vigezo , kwa maana Mtoa ni nchi, na kiongozi mkuu wa nchi anatoa kwa kwa niaba ya nchi yaani Rais wa JMT, na anayepokea ni mbarawa, katika nafasi yake kama Waziri.

kwa Upande, wa the Emirate of Dubai
wakati kwa upande wa Emirates of Dubai, mtoaji aidha ni Emirate of Dubai, au United Arab Emirate , au Emirate of Dubai na United Arab Emirates, hayo atayaona kwenye kichwa (heading) ya appointment letter, mstari wa pili wa power of attorneys, na kwenye footing, yaani signature, ( kwa hiyo signature (saini) watoaji ni wawili, heading mtoaji ni mmoja, second line, watoaji ni wawili) (Emirate of Dubai, na United Arabu Emirates),

anayetoa nguvu ya kisheria, hatajwi kwa jina wala kwa nyadhifa yake, au cheo chake, au uhusiano wake na serikali hizo mbili na nguvu alizozonazo kisheria, kumpatia mpokeaji. ( kwa tafsili nyepesi, hakuna mtoaji wa nguvu ya kisheria kwa upande wa serikali zote mbili tajwa katika power of attorney hizo.

ila, takwa la pili kwa maana ya mpokeaji anatajwa, kwa maana ya H.E. Ahmed Mahboob Musabih, ambaye ni Chief Executive Officer of the Ports, Customs and Free Zone Corporation ( being referred to as agent).

2. what does it mean? ina maana gani kisheria
jibu ni jepesi, hakuna ridhaa (consent ) ya serikali ya Emirate of Dubai, au United Arab Emirates, iliyoridhia kusainiwa mkataba huo.
.......................................................................................................................​
Naunga mkono hoja, hili nimelitaja kwenye bandiko langu hili Japo Bunge Limeridhia, DPW Kuendesha Bandari Zetu, ni Makubaliano Tu, Tukithibisha Kuna Matatizo, Tunarekebisha Mkataba wa HGA, Kazi Nzuri Iendelee!
Wanabodi,
  1. Mkataba wa IGA na HGA wa state parties inaingiwa kati ya serikali na serikali za nchi na nchi, hivyo ukisoma documents za makubaliano utaona ni kati ya serikali ya Tanzania na serikali ya UAE, lakini signatories kwa serikali ya Tanzania ni serikali kweli, lakini kwa serikali ya UAE, signatories ni Mwarabu wa Dubai wa DP World na sio serikali ya UAE, kwenye mkataba wameandika serikali ya Dubai, Dubai is not a state, hivyo hapa kunauwezekano tunatapeliwa!. Serikali yetu inaingizwa mkenge kuingia mkataba na a private company disguised as a government of UAE kumbe ni kampuni binafsi!.View attachment 2653406
  2. Mkataba Kati ya serikali ya Tanzania na Dubai ni batili kwenye sheria za kimataifa. Maana Dubai sio nchi, a sovereign state kama ilivyo Tanzania, Dubai hapa inajitambulisha kama a State Party, Dubai is not a state hivyo haiwezi kuwa a state party, it has no the capacity to transact as an international state IGA, haiwezi kuingia mikataba ya kimataifa na nchi na nchi!, inaweza kuingia mkataba wa kimataifa wa nchi na kampuni au kampuni na taasisi kama ilivyoingia na mamlaka ya Bandari, taasisi kwa taasisi, kama ilivyofanya hapa View attachment 2653409ambapo DP World iliingia mkataba na Mamlaka ya Bandari TPA, mkataba ambao Rais Samia aliushuhudia ukisainiwa kule Dubai during Expo Dubai.
  3. Sasa kampuni hii ya DP World iliyoingia mkataba na mamlaka ya Bandari, sasa inajigeuza nchi, sovereign state of Dubai, imeingia mkataba wa kimataifa wa state party na serikali yetu!, huku ni kututapeli!. Dubai is not a state, it's not a nation na nchi isiyo na sovereignty!. DP World is not a state, it's a private company, hapa imejigeuza ni nchi!. Huu sio utapeli?. View attachment 2653458
  4. Mikataba ya kimataifa ya state parties, inaingiwa kati ya nchi na nchi, hapa nchi inayotambuliwa ni Falme ya Kiarabu, UAE, ndio inayotambulika kwenye sheria za kimataifa as a state, na sio Dubai ambayo ni sehemu ya UAE, sio state, hivyo hapa kuna utapeli!. Due diligence ingefanyika, hili lingeonekana!.
  5. Status ya Dubai kwe UAE ni sawa na status ya Zanzibar ndani ya JMT, Zanzibar has no capacity to transact an international treaty kwasababu Zanzibar sio sovereign state, haina sovereignty. Dubai pia sio sovereign, hivyo mikataba yote ya kimataifa ya Zanzibar, inaingiwa na JMT kwaniaba ya Zanzibar, IGA na HGA inapaswa kuingiwa kati ya Tanzania na UAE na sio Tanzania na Dubai!.
  6. DPW ni kampuni kama inavyoonyesha hapaView attachment 2653462
  7. Wanasheria wanapoamua kufanya magumashi ya kisheria, wanakuzuga kwa maneno ya kweli kwenye mkataba, mfano hapa Dubai inatambulishwa kama nchi,View attachment 2653466lakini mkataba wetu hii iliyoandikwa kama nchi, sio nchi kweli bali ni kampuni ya DPW!.
  8. Kwa vile kwa upande wetu ni serikali yetu, ili kuonyesha IGA ni kati ya serikali mbili, hapa wameitaja kampuni ya kiserikali ili kuiserikalisha kampuni binafsi ya DPW kuwa ni serikali View attachment 2653471
  9. Hivyo mikataba ya HGA utaokuja kuingiwa na serikali yetu, sio mkataba wa kimataifa wa kiserikali kati ya serikali yetu na serikali ya UAE, lakini hakuna chochote cha UAE bali kampuni binafsi ya DPW iliyoserikalishwa na kujifanya ni serikali!.View attachment 2653477View attachment 2653481
  10. Kwa vile mikataba ya kimataifa inahusisha state parties, HGA inayokwenda kuingiwa ni HGA kati ya nchi ya Tanzania ambayo ni state na kuingia na DPW iliyo ji stetisha kama a state ambapo huu pia sio utapeli?.
Paskali.
 
Back
Top Bottom