Uchaguzi 2020 Sababu 11 kwanini Lissu atapata ushindi wa asilimia ndogo kuliko wote tangu 1995

Uchaguzi 2020 Sababu 11 kwanini Lissu atapata ushindi wa asilimia ndogo kuliko wote tangu 1995

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
7,968
Reaction score
19,368
1: JPM anamengi yakuonekana aliyofanya kwa wananchi Lissu hata jimbo lake tu hakuna chochote cha kuonyesha.

2: Kila vita anayoingia JPM anapata ushindi au nusu ushindi (MAKINIKIA) wa kugusika, Lissu ni nusu ushindi au ushindi wa maneno.

3: Lissu amejipanga kutumia tuhuma kujinadi wakati JPM atakuwa na muda wa kutangaza na kuwaonyesha watanzania aliyowafanyia.

4: Taifa bado linamwangwi wa utisho wa kazi za JPM na maamuzi magumu kama KORONA, Lissu kaanza udalali wa kutaka kutuaminisha watu wanakufa korona kipindi ambacho kila kanisa linatoa ibada za shukrani kwa Mungu kutupa rais Jasiri.

5: Wakati wananchi wanameaminishwa MABEBERU ni watu wabaya, LISSU anaonekana kutegemea watu hao ambao wapiga kura wanaamini ni wabaya kama watu wake wa karibu.

6: Tangu amepata Janga la kumiminiwa vitu vinavyodhaniwa kuwa ni Risasi Kila akisimama kuongea anaongea yaleyale hadi anaboa. Wakati Tunategemea JPM atoe mambo mapya licha ya kuwa na mengi ya kusema.

7: Kanda ya ziwa huwa inaamua nani ashide uchaguzi kwa idadi kubwa ya wapiga kura, huko tumeshuhudia vitendo vingi vya maendeleo kuliko maneno ya kipinzani na malalamiko. Wanatarajia Lissu utawafanyia nini zaidi ya Meli, Busisi, Barabara, Viwanda, zahanati etc ila naona umejipanga kuwapelekea tuhuma na maneno ya kujirudiarudia.

8: Lissu maarufu mitandaoni ila katika uhalisia kwa wapiga kura Magufuli ni maarufu kuliko Lissu.

9: Lissu amekaa kama mtu anayetakiwa kusumbua mfumo sio kuwa kiongozi wa mfumo wa kuwasaidia watu. Maneno yake, Body language yake haimfanyi mpiga kura aone kuwa hapo kuna jamaa mwenye utisho wa kuwa kiongozi wa nchi. Angalau Membe kidogo.

10: Hakuna mtu wa kuvujisha taarifa za siri za kiserikali na kiCCM ili ziwape wapinzani kiki kama enzi za Dr Slaa. Karibu watu wote wanahofu hata tu kulitaja jina la JPM kimizaha. Kwa kipindi ambacho hakuwepo LISSU nchi imebadilishwa saikolojia kabisa jambo ambalo halihitaji miezi miwili kulirudisha.

11: Kwa sasa JPM haonekani kama Kiongozi wa nchi tu bali pia kama Kiongozi wa Kiroho. Kuna watu leo wanamuamini JPM kuliko hata viongozi wao wa kidini maana Alionyesha utegemezi mkubwa kwa Mungu ktk Corona kuliko hofu za viongozi wao. Sio suala la miezi miwili kumtolea mtu imani.
 
Kwa kumtaja tu Lissu, basi inaonekana anawapa shinikizo la damu.

Mbona huwataji akina Lipumba na Membe

Sent from my VFD 301 using JamiiForums mobile app
Lipumba na Membe na Lissu wote hata wakiungana hawatakuwa na impact yoyote. Ndio maana nimemtaja ambaye unadhani anauwezo wa kusababisha shinikizo la damu kwa wanaomuamini
 
Lipumba na Membe na Lissu wote hata wakiungana hawatakuwa na impact yoyote. Ndio maana nimemtaja ambaye unadhani anauwezo wa kusababisha shinikizo la damu kwa wanaomuamini
Mmeshaanza kula na mahindi barabarani na kununua kuku! Subiri TL awanyooshe vilivyo.

Mwaka huu badala ya push ups, mtaruka kichura chura!

Sent from my VFD 301 using JamiiForums mobile app
 
Siku zote CCM hawalali wanaomba usiku na mchana upinzani usiungane, hadi sasa wamefanikiwa.

Siku upinzani wakiungana historia itaandikwa upya.
 
Bado hajachukua fomu mko hivi siku akichukua fomu si mtatakiwa kuwa chini ya uangilizi hata wa RED Cross
Ni vizuri anachukua form akiwa na akili baridi za kujua anachokifanya sio kwa kujazwa upepo na wafuasi hewa.
 
Saa 24 zilizopita, post kuhusu Lissu ni nyingi sana kiasi ambacho wachanganuzi wanaelewa kwamba Lissu ni Shujaa.
 
Kwa alivyoanza huyo jamaa hiyo mouth diarrhea itaharibu kila kitu.

Robert Greene kwenye kitabu chake cha The 48 Laws of Power anakuambia,
Always say less than necessary.
 
Magufuli si ana mandege, mareli, mann???

Sisi tunataka Rais wakuwapa vijana ajira, Rais wakulinda nakuheshimu Katiba, Rais wa Kulinda Utu na haki za binadamu na kuwaishi wanadamu wote ktk msingi wa usawa, Rais Wakuongeza mishahara ya wafanyakazi, Rais wakumsaidia mkulima wa korosho, mbaazi, n.k, Rais ambaye Hawezi ona watu wake wanapotea na kukaa kimya., Rais wakutoa Mikopo kwa wanafunzi wote wa vyuo vikuu bila kujalisha kasomea Sekondar gan, Rais atakayehakikisha Elimu inakua bora, sio utopolo wenu uliopo sasa.

MTOA MADA, AYO ULOYAANDIKA, HATA AKINA MUSOLIN, WANAZI , GHADAFI, WALIYAFANYAAAAA .

Wewe jiulize, Pamoja na udogo wa nafasi yake , Lissu hajawah hata kua waziri, ni mbunge tu, Lakini umaarufu wake, watanzania waliojitokeza kumpokea .... Laxima ukubaliane namm kua LISSU NI MPANGO WA MBINGU.
 
Kwahiyo hapo namba 7 mmepeleka maendeleo kanda ya ziwa ili mchaguliwe kwa kishindo? Huu ni ukanda wa wazi kabisa na kipimo tosha kuwa nyinyi mnatugawa, hatuwapi kura na jiwe wenu!

SASA BASI
 
Interview ya Leo KTN tulitegemea kusikia Foreign Policy ya Chadema, tunaambulia makelele tu yale Yale.
 
Taifa bado linamwangwi wa utisho wa kazi za JPM na maamuzi magumu kama KORONA, Lissu kaanza udalali wa kutaka kutuaminisha watu wanakufa korona kipindi ambacho kila kanisa linatoa ibada za shukrani kwa Mungu kutupa rais Jasiri.
Hili pekee linatosha kabisa kumwangusha Lisu asipobadirika
 
Back
Top Bottom