Uchaguzi 2020 Sababu 11 kwanini Lissu atapata ushindi wa asilimia ndogo kuliko wote tangu 1995

Lipumba na Membe na Lissu wote hata wakiungana hawatakuwa na impact yoyote. Ndio maana nimemtaja ambaye unadhani anauwezo wa kusababisha shinikizo la damu kwa wanaomuamini
Ujinga ni majaliwa ya kudumu.
 
5: "Wakati wananchi wanameaminishwa MABEBERU ni watu wabaya",

Nani aliyewaaminisha hivyo? serikali ya CCM? Mbona wanapokea misaada, mikopo na uwekezaji kwa mabilioni kutoka kwao? Baniani mbaya kiatu chake.........
Tuache unafiki. Tanzania inategemea sana unyonyaji wa Ubebebru. Labda hamuelewi maana ya neno hilo. Hakuna chama cha siasa hapa Tz ambacho kimetangaza kupinga ubeberu. Wote sawa ndio maana hawachoki kutembelea mabalozi wa kibebebru
 
Lipumba na Membe na Lissu wote hata wakiungana hawatakuwa na impact yoyote. Ndio maana nimemtaja ambaye unadhani anauwezo wa kusababisha shinikizo la damu kwa wanaomuamini

Si wekeni tume huru na wala msimzi ie sauti anapoongea
 
Hujui siasa, usitegemee eti Tundu Lissu aanze kutaja aliyofanya ndio achaguliwe. Pia usitegemee ukabila na ukanda kushinda, hilo ndio tatizo la ccm na watashangaa hawashindi kwasababu ya kutegemea kura za kikabila. Ukabila ni jipu kubwa ndani ya kichwa cha jiwe.
 
Siku zote CCM hawalali wanaomba usiku na mchana upinzani usiungane, hadi sasa wamefanikiwa.

Siku upinzan wakiungana historia itaandikwa upya.
Kwani 2015 kilitokea nini? Wapinzani siyo watu makini wanatumia maneno mengi kuliko akili kudeal na CCM. Hahitaji akili nyingi kujua uchaguzi wa 2020 umeisha na kuna watu CCM wameanza mipango ya 2025. Hivi unajua jinsi upinzani ilivyojiharibia kujitoa kwenye chaguzi ndogo za serikali za mitaa na madiwani? Utajua matokeo yake kwenye chaguzi za wabunge na u rais.
 
hakuna ukabila hapo mkuu. Kanda ya ziwa kuna kila mtu wa kutoka kila kona, ila takwimu zinaonyesha ndio mahala ambapo watu wengi hujitokeza kupiga kura. Usiulishe uzi maneno mkuu
 
Si wekeni tume huru na wala msimzi ie sauti anapoongea
Kuna mahala pengi tu duniani ambapo palikuwa na hiyo inayodhaniwa tume isiyo huru lakni siku watu waliochoka serikali ziliondolewa bila kujali kuna tume huru au tume fungwa.

Hii sio hoja nzuri mkuu, usiitegemee sana
 
Huu ushauri aufanyie kazi na asihangaike na kupigwa risasi a focus na future zaidi.
 
Kwa Maoni yangu Kila chama (Ccm na Chadema) kinapaswa kutafuta kura zao (walizopata na walizopoteza ) 2015 ziliko !
Hiki ndicho kipimo halisi cha kuanzia.

Niinavyo 2020 Act inachoweza ni kupunguza kura za ccm kupitia Wana ccm Wanaopenda Bernard na. Wapizani Wanaopenda Zitto lakini 2015 walimpa Magufuli kwa hasira ya Lowasa na Dr Slaa. Kwa hiyo huu sio uchaguzi wa kushinda saa nne asubuhi kwa sababu kura hutafutwa.
Halafu Fahamu jambo moja duniani kote; Ushindi wa kura hauji kwa sababu umeleta maendeleo.!
 
Kama huwezi kujua maendeleo huletwa na kodi yako na Ni serikali ndio husimamia acha kuongea. Tundu Lissu alikuwa mbunge Kama alivyo Ndugai kwahiyo wote ukipima maendeleo kwenye majimbo yao Kuna baadhi yametekelezwa na siyo wao waliotoa fedha Bali Ni serikali kwa Kodi yetu. Hakuna mahali Magufuli ametoa fedha mfukoni kutekeleza mradi. Acheni ujinga
 
Lissu amekaa kama mtu anayetakiwa kusumbua mfumo sio kuwa kiongozi wa mfumo wa kuwasaidia watu. Maneno yake, Bodylanguage yake haimfanyi mpiga kura aone kuwa hapo kuna jamaa mwenye utisho wa kuwa kiongozi wa nchi. Angalau membe kidogo.πŸ‘ˆ Hapo umenena sahihi kabisa.
 

: Kwa sasa JPM haonekani kama Kiongozi wa nchi tu bali pia kama Kiongozi wa Kiroho. Kuna watu leo wanamuamini JPM kuliko hata viongozi wao wa kidini maana Alionyesha utegemezi mkubwa kwa Mungu ktk Corona kuliko hofu za viongozi wao. Sio suala la miezi miwili kumtolea mtu imani.πŸ‘ˆ Kweli kabisa. Kwenye Korona hata wakuu wa dini kawazidi imani kwa kuwaaminisha waumini kutokuwa na hofu.
 
mkuu mimi sina wasiwasi hata wanaopinga wanapingia vidoleni tu huku moyoni wanajua ukweli
 
Hili ndio andiko bora hapa JF kabla ya kuingia kwenye uchaguzi October 2020.
 
Umesahau kingine. Tume imepanga kumpatia Lissu kura asilimia kidogo.
 
Interview ya Leo KTN tulitegemea kusikia Foreign Policy ya Chadema, tunaambulia makelele tu yale Yale.
mental programming yake haijatoka kwenye upingaji kwenda kwenye uongozi wa taifa lenye changamoto kubwa kama hili.
Hii kazi akiipuuza akabaki na maneno ya tuhumatuhuma atakuja kudhani watanzania ni wasaliti kumbe kajisaliti kwa kinywa chake mwenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…