Mkandara, Kikwete kazi imemshinda tusimtafutie visingizio. Kiongozi ukiwa imara na mfuatiliaji, walioko chini yake wote wananyooka na kuwajibika. Lakini kiongozi akiwa mzembe, mvivu, asiyefuatilia walioko chini yake, mpenda anasa, porojo na vingi vinginevyo vya aina hii, walioko chini yake nao wanaharibika mara dufu. Serikali ya Kikwete ni kama iko holiday, kila mtu anafanya lake binafsi maana hakuna kiongozi wa kuwafuatilia majukumu yao. Lazima Watanzania tukazane kumuondoa JK kwa njia yoyote ile kama tunataka nchi iendelee na kuacha kumtungia visingizio.