Sababu gani Wazanzibari wako kimya juu ya fujo za Tanzania bara?

Na ule mwaka 2001 Watanganyika walikuwa wanakula mema ya Zanzibar kwa msaada wa jeshi letu na vyombo vya usalama?
Zenji mna nini nyie tofauti na kuliwa nyuma na watalii
 
Wazanzibar wameshiriki kutekeleza mauaji ya Watanganyika kwa ukatili wa kutisha kupitia jeshi lao la KMKM.

Nahisi wanataka mwenzao aendelee kushika usukani ili wazidi kufaidi rasilimali za Tanganyika
Vipi pale mwaka 2001 Watanganyika walipowaua Wazanzibari mukakaa kimya
Zenji mna nini nyie tofauti na kuliwa nyuma na watalii
Dalili ya kuishiwa hoja. Ajidhaniaye kasimama, aangalie asianguke.
 
Vipi pale mwaka 2001 Watanganyika walipowaua Wazanzibari mukakaa kimya
Hatukujua broo.
Hiyo ni miaka 24 iliyopita, hakukuwa na mitandao kama sasa, isingekuwa rahisi kwa wengi kupata taarifa, maana hizo hazitangazwi na TBC, ITV, STAR TV, nk.

Pili, wahusika wakuu wa hayo kote Zenji na bara ni ccm, mngelipiza kwao. Sasa mlichofanya mmeshirikiana na madhalimu kuuwa wananchi wengi wasio na hatia. Wengi mlioua sasa, 2001 walikuwa wachanga au hawajazaliwa
 
Huenda unazungumzia mambo mengine. Huu uzi unaulizia sababu za Wazanzibari kuwa kimya wakati wa fujo za Tanzania Bara. Michango ya wengi humu ikawa ya kulaumu na matusi kwa Wazanzibari wote. Ndiyo nikauliza kile kimya chao mwaka 2001 chini ya Mkapa na 2020 chini ya Magufuli vipi? Kiliashiria nini? Mtu akijiona yeye ni bora na wengine si chochote, hujibiwa kwa namna hiyohiyo. Tuchunge sana maneno kwani kila mtu anajua kusema.
 
Wazanzibari ndiyo wameua Watanganyika ili Mzanzibari Mzanzibari mwenzao aendelee kuitawala Tanganyika. KMKM ni Wazanzibari tupu hakuna mtanganyika kwenye jeshi hilo.
Kumbuka tu kuwa 2000 MKapa alipeleka jeshi kuua zanzibar ili aweze kutawala na Magufuli pia alipeleka jeshi zanzibar 2020 kuua ili atawale. Kwa hiyo ingawa kilichotokea bara sasa ni cha kusikitisha na hakikustahiki kutokea lakini isiwe "mkuki kwa nguruwe kwa binaadamu unauma"
 
Wazanzibar ni washenzi ndiyo wanao hua watanganyika na kuiba mali za Tanganyika...
 
Wazanzibar ni washenzi ndiyo wanao hua watanganyika na kuiba mali za Tanganyika...
Kama ilivyo kwa Watanganyika walivyo washenzi wamewaua Wazanzibari miaka ya 2000, 2001, 2005, 2015 na 2020. Leo wanalialia kilio cha mamba. Kama shubiri ni dawa kunywa nawe utapoa.
 
Kumbuka tu kuna zama na zamu ilikua Zanzibar sasa ni tanganyika poleni sana hizo ndio gharama za kupambana na maccm
Tatizo wazenji sasa hivi wanashabikia ccm ...tofauti na wabara walikuwa wanapinga ccm kupokonya ushindi wa CUF kule zenji hakuna mbara aliye furahia ccm kupora ushindi popote ila leo wazanzibari wanashabikia na kumtetea sa100.
 
Tatizo wazenji sasa hivi wanashabikia ccm ...tofauti na wabara walikuwa wanapinga ccm kupokonya ushindi wa CUF kule zenji hakuna mbara aliye furahia ccm kupora ushindi popote ila leo wazanzibari wanashabikia na kumtetea sa100.
Wacha kudanganya watu. Nyinyi ndo muloshabikia na kushiriki kuwaua Wazanzibari kwa mamia ili
muitawale na kuwatawala Wazanzibari kwa visingizio vya kuzuia siasa kali.

Ni nani alikemea Wazanzibari kuuliwa mwaka 2000 na 2001 chini ya Mkapa? Ni nani alinyanyua sauti wakati mashekhe wa UAMSHO wananyanyaswa chini ya utawala wa Kikwete? Ni nani alionesha angalau huruma mwaka 2020 wakati Wazanzibari wanauliwa kwa kumuweka Mwinyi madarakani na kupora nafasi za ubunge chini ya Magufuli? Unadahani tumesahau? Tuna kumbukumbu zote, hata zile usizozijua. Watanganyika, mara zote, mulikuwa kimya. Nyinyi ni wabaguzi sana na munadhani muna akili sana kwa kujidanganya.
 
Kuna kanuni mbili mashekh wa uamsho wanapigania nini ? Kuhusu mauaji ya zanzibar watu walipia sana kelele labda unajizima data ...wote wanao ichukia ccm walipiga kelele ........kwa hiyo wewe logic yako ni wazanzibar kuwaua wabara wasio usika na mauaji kwa kutumia polisi walio usika na mauaji zenji? Kwanini msilipe kisasa kwa polisi waliotenda uovu bali mnawatumia kuua watu .....kama hoja yenu ingakuwa ya kweli basi Samia angepambanq na polisi walio husika kwenye hayo mauaji na viongozi waliowatuma....pia kama hoja zenu ni za kweli samia angevunja muungana kwa nafasi aliyo nayo .....na nyinyi mngemuhimiza avunje muungano mbona mpo kimya ? Kwani samia ajawakamata walioua Zanzibar walq kuwa laani midomoni ? Sijawai kumsikia samiq akikemea mauaji ya wazanzibar hayo unayo yahubiri wewe......
 
Zanzibar wana haki ya kukaa kimya, ufala na uzoba wa Watanganyika wao hauwahusu. Kwanza wao ni nchi kamili yenye president na flag yao, Tanganyika acha wayaone kwani mengi ni ujinga wa kujitakia. Wahenga walinena kuwa ukubwa wa pua si wingi wa kamasi, leo watu more than 60 million wanalialia dogo Abdul anawateka na kuwaua.
 
wamesema wamelipiza kisasi Cha 2001, ila tunawahakikishia kitawalamba wapemba wote mnaoenjoy hewa safi huku tanganyika
 
Kuhusu mauaji ya zanzibar watu walipia sana kelele labda unajizima data ...wote wanao ichukia ccm walipiga kelele ......
Nipe mfano, ni nani alipiga kelele. Vinginevyo husemi kweli.
kwa hiyo wewe logic yako ni wazanzibar kuwaua wabara wasio usika na mauaji kwa kutumia polisi walio usika na mauaji zenji? Kwanini msilipe kisasa kwa polisi waliotenda uovu bali mnawatumia kuua watu ....
Hatuzungumzii kulipa kisasi. Wewe na mimi na wengine tunazungumzia mauaji ya raia yaliyofanywa kwanza Zanzibar na sasa Tanganyika. Yote ni mauaji. Kwanini nawe usiwalaumu askari waliofanya hivyo, badala yakr unawalaumu Wazanzibari kwa ujumla wao? Wewe umepata wapi uhalali huo ambao mimi sistahiki? Kumbuka unazungumza na mtu mwenye akili timamu.
kama hoja zenu ni za kweli samia angevunja muungana kwa nafasi aliyo nayo .....na nyinyi mngemuhimiza avunje muungano mbona mpo kimya ?
Kwanini avunje muungano Samia ambaye anatoka sehemu ambayo nyinyi munasema lazima idhbitiwe isilete siasa kali? Wazanzibari tulipojaribu tulifungwa, tukanynyaswa na kupigwa, mfano ni mashekhe wa UAMSHO. Sasa ni wakati kulitekeleza hilo nasi tunasubiri kwa hamu.
Kwani samia ajawakamata walioua Zanzibar walq kuwa laani midomoni ? Sijawai kumsikia samiq akikemea mauaji ya wazanzibar hayo unayo yahubiri wewe......
Ni hoja za kitoto sana! Hivi angewakamata wapi wakati mambo hayo yalipotokea hakuwa na mamlaka?

Alichofanya Samia ni kuzuia fujo, wizi na unyang'anyi kwani yaliyotokea nyuma hayamhusu.
 
Wapinzani wote walipiga kelele kwani ujui kuwa hata CUF IPO BARA NA ZENJI ...Nilikuuliza walio waua wazanzibar ni kina nani na watumishi wa nani mbona samia ajawatuhumu kwa kuua wazanzibar wala kuwachukulia hatua ...nilini umemsikia Samia akizungumzia kuwashitaki hao wauaji ? Bali kinyume chake kapitisha sheria ya polisi kuua bila ya kushitakiwa .tumia akili achakutumia majini ya mudi boy.
 
Mambo ya ndani haya wataingiliaje? Wamewapa kichapo inatosha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…