Sababu gani zilifanya Jay Jay Okocha asitwae Ballon D' or enzi zake?

Sababu gani zilifanya Jay Jay Okocha asitwae Ballon D' or enzi zake?

Ina maana xavi,iniesta,Modric,Marcelo nk siyo mafundi

Ishu saizi ballon dor saizi wanatizama idadi ya magoli

Hata zizzou angekuwa enzi hii ballon dor angesikia kwenye bomba

Ballon dor ni kwaajili ya strikers siku hizi

Well said!
 
Hao ulowataja kipindi hicho wasingeambulia kitu kwa Aguero,Iniesta,diego costa,de maria,xavi,dybala,higuain,lewandosky,suarez n.k wengi tu...tena wangekuwepo kipindi hiki Cha Messi nakuhakikishia wasingepata hata harufu ya ballon d'Or wangekua na kazi ya kumpongeza mwenye kipaji chake....si mwingine bali Messi mwenyewe..mtoto aliyezaliwa na kipaji..


Asante sana Messi umetuletea burudani ambayo kwa muda mrefu sana hatukuipata tangia Mzee wa kazi astaafu soka Diego Armando Maradona a.k.a El pibe de oro...

Mtoto wa miaka 5 anamjua messi,anampenda messi,anapenda jezi ya messi,anapenda kulitaja jina messi,anapenda kusema natamani niwe kama messi.... messi anapendeka bana kuliko mchezaji yeyote...

Dah, sawa kaka
 
Mkuu unataka kuniambia suarezi,neymar, aguero , Diego Costa, lewandosk , n.k hawajui?? Wachezaji wanaofunga 20+ goals per season unawasahau mkuu....


Ngoja nikwambie kitu sio kwamba recently hakuna wachezaji wazuri la hasha... Ni bahati mbaya wametokea kipindi cha messi na neymar .... Messi msimu juzi laliga alifunga magoli zaidi ya 40 kitu ambacho hakijawahi kutokea tangu mungu kaumba huu ulimwengu ...
Hao uliowataja bado huwezi wafananisha na akna de Lima, Ronaldinho au Zidane na Messi au Ronaldo wangekuwepo kipindi hicho wasingeshnda kwa kupokezana na kaa ujue mpira kwa sasa ni umekufa ila tunaupenda tu ndo maana hatuachi kuangalia ila angalia world cup za miaka ya karibuni uangalie na za miaka 90 hadi the 02 utaona utofauti mkubwa sanaa ya wachezaji wa sasa na kipindi kile pia angalia ligi kuu kama Seria A na nyingine zote mpaka uingereza ni tofauti na miaka ile tena na Afcon ndo kabisa hakuna kitu kwa kweli wachezaji wa zamani na sasa ni vitu viwili tofauti wa sasa wengi ni pesa kubwa wanapokea viwango kawaida ni wachache wa sasa ambao ukiwaweka namagwiji wa zamani wanaweza pata namba mfano kati ya suarez na Ronaldo de Lima kwa kiwango yupi akae benchi? ?
 
Kaka naona unababaishwa na Ronaldo Xtian na Messi kuwa wanapokezana, ukweli ni kuwa kwa sasa hakuna mafundi wa soka Duniani, wako wachache sana na ndio kisa cha hawa wawili kupokezana,
Hebu kumbuka wakati Ronaldo de Lima, Rivaldo, Carlos, Mtume Gaucho, Decco, Figo, Zidane, Okocha, Chev nk hapo ilikuwa ni shughuli pevu kumchagua best player
Mimi nakupinga Mkuu, mbona Xavi, Iniesta, Sneijder wamecheza nyakati sawa na hao mafahali wawili.
 

1998 hakuchukua, Alichukua mtu mmoja wa kuitwa Mustapha Hadji, Wa pili ndo akawa Okocha, wa tatu akawa Sunday Oliseh. Get your facts right.

Inshort Austin Jayjay Okocha hana tuzo ya mchezaji bora wa africa kwa miaka yote aliyokuwa mchezaji mpira.

Inauma sana kuona mpira haujamtendea haki kama yeye alivyoutendea haki. Kwa mchezaji kama Okocha kukosa tuzo ya mchezaji bora wa Africa inaonesha ni namna gani unaweza usivune ulichopanda.
 
Alikua hana cha maana uwanjan zaid ya chenga na kupiga faulu Kali,,,na mbaya zaid sikumbuki kabeba kombe gan yule jamaa
 
Wakuu karibuni tujadili sababu zilizomfanya fundi wa soka toka Nigeria na Africa kwa ujumla, Austin Jay JAy Okocha kushindwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Dunia enzi zake akisakata kabumbu licha ya uwezo na kipaji maridhawa cha hali ya juu alichokuwa nacho.
Kuna mfaransa rafiki angu mnazi wa soka sana. tukiongelea mpira hafichi hamung'unyi huniambia kuwa Austin Jay Jay Okocha/ Yaya Toure kama sio "uafrika" wao kama sio mmoja wao kuchukua hiyo tuzo ya mchezaji bora wa dunia basi hata katika Tatu bora wangewahi kufika.

Ujue hizi tuzo pia ni biashara kubwa sana. kuna influence kubwa sana ya makampuni yenye ngawira. wanaangalia faida kwanza.1995 George Apong Weah aliwafanya mubashara
 
Kipindi hiko kulikuwa na wakali weengi sio kama sasa wanasemwa wawili tu Mesi Ronaldo........kipindi hiko Ronaldo de Lima,Roberto Carlos,Babangida......na wakali wengi tu hivyo asingeweza kupewa walikuwepo wakali zaidi yake enzi hizo ye alikuwa mkali ila si kwa kiwango hiko unachokisema japo kuna chenga ambazo alipiga enzi hizo hawakuweza kupiga.......mfano Ronaldo de Lima ye ilikuwa ni kupachika magoli tu na chenga au madoido kidogo sana
Okocha huwa namfananisha na kina Ronaldinho
Okocha ligi moja na akina Ronaldinho, Zidane , Laudrup,Pirlo ect
 
Kaka naona unababaishwa na Ronaldo Xtian na Messi kuwa wanapokezana, ukweli ni kuwa kwa sasa hakuna mafundi wa soka Duniani, wako wachache sana na ndio kisa cha hawa wawili kupokezana,
Hebu kumbuka wakati Ronaldo de Lima, Rivaldo, Carlos, Mtume Gaucho, Decco, Figo, Zidane, Okocha, Chev nk hapo ilikuwa ni shughuli pevu kumchagua best player
[emoji23] Mtume Gaucho
 
Back
Top Bottom